theHAVARD_product
JF-Expert Member
- May 4, 2012
- 297
- 211
Atawezaje wakati zimempungua kwenye hicho kitu alichokitwisha juu ya shingo analiita kichwa.
Kuna waliosema mheshimiwa rais hatoboi 2015 yaani angekuwa amengatuka mapema,baada ya kumtuhumu kuwa mambo mengi ameyafumbia macho.
Na unaona mahali ambapo Yeye kikwete na wewe na wengine wa aina yenu wanapo-capitalize?
Imebakia miaka 2 tu akamilishe safari ngumu na nzito,basi mimi nimeona nimtakie kazi njema na yenye mafanikio,kiukweli anastahili sifa.
Unapotoa credit kwa kitu fulani ni lazima unafanya ulinganishi(comparison) ya hiyo kitu na kitu kingine chenye uhusiano au ufanano.Mheshimiwa Rais Jakaya Kikwete anastahili sifa,mimi kama Mtanzania nampa pongezi rais Kikwete kwa kuongoza nchi katika hali ya amani na utulivu.
Kuna waliosema mheshimiwa rais hatoboi 2015 yaani angekuwa amengatuka mapema,baada ya kumtuhumu kuwa mambo mengi ameyafumbia macho.
Unajua nchi haiongozwi kwa jinsi tunavyotaka sisi.Kiukweli nchi ilifika mahali iliyumba ila mwanaume wa shoka rais kikwete alituliza akili zake akafumua uongozi mambo yakaenda shwari.
Wapo waliomuombea mabaya ila rais hakuwajali sana alijitahidi mpaka hapa tulipofika.
Imebakia miaka 2 tu akamilishe safari ngumu na nzito,basi mimi nimeona nimtakie kazi njema na yenye mafanikio,kiukweli anastahili sifa.
Unaweza kukuta. Mleta mada ni mbunge wa ccm
Unaweza kukuta. Mleta mada ni mbunge wa ccm
mungu mkubwa wote waliokuja na silogani ya nchi haitatawalika. Sasa wanaona aibu kila kona wanayopita, sasa wamebaki kulalama na katiba mpya, katiba ambayo wenyewe waliichekelea pale ikukummheshimiwa alipowapa nafasi ya kuwasikiliza.
Mheshimiwa Rais Jakaya Kikwete anastahili sifa,mimi kama Mtanzania nampa pongezi rais Kikwete kwa kuongoza nchi katika hali ya amani na utulivu.
Kuna waliosema mheshimiwa rais hatoboi 2015 yaani angekuwa amengatuka mapema,baada ya kumtuhumu kuwa mambo mengi ameyafumbia macho.
Unajua nchi haiongozwi kwa jinsi tunavyotaka sisi.Kiukweli nchi ilifika mahali iliyumba ila mwanaume wa shoka rais kikwete alituliza akili zake akafumua uongozi mambo yakaenda shwari.
Wapo waliomuombea mabaya ila rais hakuwajali sana alijitahidi mpaka hapa tulipofika.
Imebakia miaka 2 tu akamilishe safari ngumu na nzito,basi mimi nimeona nimtakie kazi njema na yenye mafanikio,kiukweli anastahili sifa.
Unapotoa credit kwa kitu fulani ni lazima unafanya ulinganishi(comparison) ya hiyo kitu na kitu kingine chenye uhusiano au ufanano.
Unapompa sifa Rais kikwete kuwa ameongoza vizuri, ila tu kwa sababu moja tu, amani na utulivu inakubidi ulinganishe na awamu zilizopita, binafsi natilia shaka hizi sifa kama ni sifa za dhati toka moyoni au ziko corrupted.
Je, rais ametimiza ahadi alizoahidi kwa kiwango gani?, Je, wewe unadhani aliingia madarakani kwa ajili ya kuleta utulivu na amani tu?
Tangu nchi yetu ipate uhuru, ni kipindi cha JK pekee ambacho tumeshuhudia ukosefu wa amani na utulivu kama vile mauaji ya albino, kutekwa na kuumizwa kwa watu maarufu, mapigano ya kidini yaliyosababisha mauaji sanjari na kupigwa risasi na kuuawa kwa viongozi wa dini. Haya mambo yametokea katika kipindi hiki cha JK na katika tawala zilizotangulia hatukuwahi kuyashuhudia.
Leo wewe unasimama hadharani tena mchana kweupe na kusifu kuwa ameongoza kwa amani na utulivu, huoni aibu?
Kiukweli nchi ilifika mahali iliyumba ila rais kikwete ..........................
Nimerudia tena kusoma post yangu, hakuna sehemu nimesema kuwa wenzangu ni majuha na mimi nina uwezo mkubwa wa kufikiri, ila tu nilikuwa namkumbusha mleta mada alinganyishe utawala ya JK na tawala zilitangulia halafu aseme ni wapi amani imepotea?.Sasa ulitaka asemeje rafiki? Ila binafsi nakushukuru kwa kumtambua kwamba yeye ni Rais,kwani kufanya hivyo ni uthibitisho tosha sifa anazopewa anastahili na ndizo anazo.
Hivi usipomsifu kiongozi wako wa nchi yako, utamsifu kiongozi wa nchi gani?.Na kama utamsifia kiongozi wa nchi fulani,je ulikwisha wahi kuishi huko? Na kama ulikwisha wahi ishi huko,ni kitu gani kilikuleta nchini Tanzania?
Ndugu yangu,jenga utamaduni wa kusifia cha nyumbani na kama kuna mapungufu ni bora ukatoa mapendekezo/maelekezo yenye tija kuliko kuwakatisha tamaa wenzako,mbaya zaidi kuwaona wenzako ni majuha ila wewe ni bora mwenye upeo mkubwa wa kufikiri.
Hii post imesababisha nimecheka peke yangu.Hata mimi nina mashaka na hili mkuu unaweza kuta huyu ni Nchimbi ati.