Rais kikwete anasalitiwa na watendaji wake: | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Rais kikwete anasalitiwa na watendaji wake:

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Salas, Jul 22, 2011.

 1. Salas

  Salas JF-Expert Member

  #1
  Jul 22, 2011
  Joined: Feb 15, 2009
  Messages: 380
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Zaidi ya asilimia 50% ya watu waishio vijijini hawana huduma ya maji, ikiwa asilimia 8O% ya watanzania ndio inakadiriwa kuwa wanaishi maeneo ya vijijini. Kwa mujibu tafiti zilizofanywa na wizara ya afya na asasi nyingine zinaonyesha kuwa vifo vya watoto chini ya miaka mitano ni 20,000 kwa mwaka ikiwa ni sawa na mabasi 333 yanayopata ajali kila mwaka pasipo kuwa na mtu aliyesalimika kwenye ajali. Machache kama sio hakuna yamefanywa kufikia asilimia hii ya watu wanaokosa huduma hii muhimu.

  Tumeshuhudia wabunge wakiwa kidedea kusiamamia swala la umeme katika bunge lakini nguvu hizo pia zingeelekezwa kwenye sekta ya maji zingezaa matunda ambayo yangepunguza gharama kubwa inayotumika na wizara ya afya katika ununuzi wa madawa ya magonjwa yanasababishwa na ukosefu wa maji au matumizi ya maji machafu na athari kadha wa kadha katika ukuaji wa uchumi wa nchi kwa kupoteza nguvu kazi.

  Katikahali ya kukangaynya ikiwa ni muendelezo wa usaliti kwa muheshimiwa rais wetu ni ile hali ya Tanzania kukataa kupiga kura ili kutambua swala maji kama haki ya binadamu katika uchaguzi wa umoja wa kimataifa kutambua haki Maji uliofanyika tarehe 28 july 2010. Tanzania ikiwa nimiongoni mwa nchi 41 zilizopiga kura ya absentation ikiwa ni kuficha aibu ya kukataa haki hii istambulike ikiwa imeongozwa kidedea na USA na nchi nyingine na za ulaya na makoloni ya ulaya ikiwemo kenya. Licha ya hayo nchi 122 zilipiga kura ya kutambua haki hii right to water and sanitation.

  Katika Muendelezo huu wa aibu, ukiwa unafanywa kwa lengo ama la kumdhalilisha Mheshimiwa rais au kutowajibika kwa viongozi wa idara husika Mheshimiwa rais alishapitisha sheria ya maji na usafi wa mazingira sheria namba 12 ya mwaka 2009 inayotambua kuwa maji ni haki ya binadamu. Nita quote “ 4.-(1) The objective of this act is to promote and ensure the right of every person in Tanzania to have access to efficient, effective and sustainable water supply and sanitation services for all purpose”

  Nachelea kudadavua kuwa huu ni usaliti wa makusudi ambao pia umewahi kufanywa katika kipindi cha vijiji vya ujamaa ambapo jitahada safi za Mwalimu Julius Kambarage nyerere zilipotoshwa na walarushwa wachache katika kuhujumu mawazo sahihi ya Mwalimu ili kuweza kufikisha huduma za jamii kwa watu wake ikiwemo maji na nyinginezo. Tukumbuke pia mwalimu aliweza kufanya kazi katika miongo miwili kwa kauli mbiu ya maji kwa wote. Swali ni Je kwanini hawakusaini in favor ya right to water and sanitation na wakati sheria ziko wazi ??????

  Hizi ni hujuma kama zile zinazoendelea kwenye miradi ya vijiji kumi ambapo japo wizara husika haitaki kuweka bayana kuwa vijiji sio kumi tena ila vitatu kutokana na ubadhirifu wa wataalamu washauri ambao mashirika yameundwa kiuhuni ili kuhujumu nia safi ya Rais kuwapatia huduma ya maji watu wake. Gharama za mradi zimekuwa kubwa kushinda fedha na waziri mwenye dhamana anakiri hilo kwenye hotuba yake ya wiki ya maji ili hali anajua anajua kuwa sio mapendekezo ya wananchi yaliyopitishwa kwenye design ya hiyo miradi ni wizi wa wataalam washauri ili makampuni ya kijanja ya ujenzi yaje kukwapua hizo hela. Huu ni ufisadi mwingine kwa ajili ya kuja kumchafua mheshimiwa rais.

  Ninasisitiza kuna haja ya kila mtu kusimama kwenye nafasi yake katika kuleta maendeleo ya hii nchi, maisha bora yatafikiwa pale tu kila mtu mmoja mmoja atakapofanya kazi kikamilifu katika nafasi yake.

  hakika kikulacho kinguoni mwako huu ni muendelezo wa usaliti dhidi ya rais wetu Mtukufu wa Jamuhuri ya Tanzania.
   
 2. d

  dotto JF-Expert Member

  #2
  Jul 22, 2011
  Joined: Sep 29, 2010
  Messages: 1,720
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Alyewachagua kuwepo hapo nani?. Na nani mwenye kuwachukulia hatua? usitudanganye!. Richmond > Dowans>Symbion ya mtendaji gani mdogo?
  Mikataba ya Barrick, IPTL, na nyingine nani mtendaji mdogo aliyesaini?. Rais Mtukufu (mtakatifu)!!!!! ha ha ha ha ha ha !!! pole.
   
 3. M

  Marytina JF-Expert Member

  #3
  Jul 22, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 7,034
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  mleta sredi ana akili za kijinga sana
   
 4. H

  Haki Yetu Senior Member

  #4
  Jul 22, 2011
  Joined: Apr 28, 2011
  Messages: 162
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Umeongea vizuri sana. Pia nakubaliana na wewe kwenye mambo mengi uliyoyaainisha.

  Lakini napingana na watu wa aina yako kwenye hoja kuwa Rais anasalitiwa na watendaji wake. Kwangu mimi hoja hii ni ya kipumbavu kabisa. Ni nani anayewateua hao watendaji wa Serikali? Kama imefika wakati wanamsaliti kwanini anaendelea nao. Tanzania ina watu zaidi ya milioni 40, kwani ni lazima kwa yeye kuendelea na hao watendaji wasaliti?

  Tuache ushabiki wa kijinga. Tulifanya makosa ya kuchagua mtu mdhaifu asiyekua na sifa za uongozi. Udhaifu wake ndo unafanya nchi yetu inakumbwa na majanga ya kujitakia likiwemo hili la mgao wa umeme. Wakati hali si shwari yeye anakwenda ziarani nje ya nchi na kuhimiza watu waje wawekeze nchini.

  Kiongozi anayesalitiwa na watendaji wake aliyewaweka yeye mwenyewe na huku hachukui hatua yeyote hatufai hata kidogo.
   
 5. kibakwe

  kibakwe Senior Member

  #5
  Jul 22, 2011
  Joined: May 10, 2011
  Messages: 171
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Huyo marafiki zake ni mafisadi na yeye pia ni FISADI
   
 6. Salas

  Salas JF-Expert Member

  #6
  Jul 22, 2011
  Joined: Feb 15, 2009
  Messages: 380
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Rais hakurupuki yuko very strategically anapanga maamuzi mazito, yeye sio mropokaji..... huu ni mwanzo tu mengi yatatokea.....leo hii basil pesa mbili mramba nini kinamtokea na wakati aliwatukana wananchi wote ng'ombe akiwemo rais aliyekuwa madarakani kipindi kile... kwani uongo ndio alisema .....si alisema hata watanzania wakila majani ndege ya rais itanunuliwa...

  simple logic

  Ng'ombe hula majani
  Watanzania wale majani
  Watanzia ni wawe Ng'ombe
   
 7. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #7
  Jul 22, 2011
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  JK anajisaliti mwenyewe na hakuna wa kumuangusha .Tuache uongo hapa ukweli utasimama daima .
   
 8. Salas

  Salas JF-Expert Member

  #8
  Jul 22, 2011
  Joined: Feb 15, 2009
  Messages: 380
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Hakika kweli wewe umenena kwani umeshindwa hata kudurusu nakuona linalozungumziwa hakika wewe ni mshabiki na sio mfikiriaji
   
 9. Joss

  Joss JF-Expert Member

  #9
  Jul 22, 2011
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 729
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Kwani nani aliyemchagulia hao watendaji wake? Tatizo liko kwake, hebu fikiria juu ya majibu kama haya kutoka kwa rais wako wakati matatizo ni serious;

  Natamani ningegeuka wingu ili ninyeshe mvua kwenye bwawa la mtera.

  Matatizo ya umeme tumeyakuta, ukame tumeukuta, tatizo la umeme ni ukame.

  Sijui kwanini nchi yangu ni maskini.

  Mkigoma mtarudi wenyewe kwenye meza ya mazungumzo mkiwa na bandeji/pop.
  .
  .
  .

  Sasa mtu kama huyo akiteua watendaji wa chini yake unategemea waweje?. Utambeba na kumtetea rais wako mpaka lini rafiki yangu?
   
 10. Dume la Mende

  Dume la Mende JF-Expert Member

  #10
  Jul 22, 2011
  Joined: Mar 23, 2011
  Messages: 419
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  wacha matusi bana
   
 11. Shedafa

  Shedafa JF-Expert Member

  #11
  Jul 22, 2011
  Joined: May 21, 2008
  Messages: 802
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  Mod turudishieni yale madole ya kuonyesha kama thread ni crap, ukweli nasikitika imechafua mchana wangu. Mtoa mada kama huna cha kuandika bora usome za wenzio tu.
   
 12. M

  Mr.Mak JF-Expert Member

  #12
  Jul 22, 2011
  Joined: Feb 23, 2011
  Messages: 2,635
  Likes Received: 496
  Trophy Points: 180
  hata kama aliwachagua yeye hakujua kama watamtenda ivo. Ni ukweli mtupu hata wale usala wa taifa na wasaiwasi kuwa wanamzunguuka kumfanya achukiwe na watu
   
 13. Mwana Kwetu

  Mwana Kwetu JF-Expert Member

  #13
  Jul 22, 2011
  Joined: Jul 12, 2011
  Messages: 617
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 60
  Mtoa mada ameongea pointi ila ameharibu kwa kumtetea JK. Kama mkuu wa kaya ana nia nzuri basi tungetegemea ile nia yake ingeonekana kwa kuwaondoa wale wanao dumaza juhudi zake nzuri za kuwasaidia wa Tanzania. Dawa ya obstacles ni kuziondoa na si kuzichekelea kama anavyofanya.
  Hii ni sawa na kusema familia yenye baba aliye strict basi ukute watoto wako wako na ni wazembe in every faculty. Hii haipo ukweli ni kwamba kama baba ni strict au smart kuongoza familia lazima na watoto na member wote wa familia watakuwa na descipline. Tunachokiona katika ngazi za chini ni reflection ya aina ya rais tuliyenaye na si vinginevyo wakuu tusidanganyane.
   
 14. Mzalendo80

  Mzalendo80 JF-Expert Member

  #14
  Jul 22, 2011
  Joined: Oct 30, 2010
  Messages: 2,385
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 160
  Jamani Kwani Kikwete amekuwa ndio rais wa Hii nchi yangu? Huu Mshikaji anatahakikisha nchi inakuwa ombaomba kama alivyo yeye, huu ndio urithi wake
   
 15. Mo-TOWN

  Mo-TOWN JF-Expert Member

  #15
  Jul 22, 2011
  Joined: Oct 11, 2010
  Messages: 1,629
  Likes Received: 140
  Trophy Points: 160
  Mtoa hoja unaposema JK anasalitiwa na watendaji wake I hope you are not suggesting kwamba JK hajua alichopaswa kufanya au kusimamia kama raisi.
   
 16. n

  ngokowalwa Senior Member

  #16
  Jul 22, 2011
  Joined: Jul 22, 2011
  Messages: 155
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Salas, ni mpaka tutakapoondakana na hii dhana potofu ya Utukufu " Rais Mtukufu , Bunge Tukufu " ndipo tutakapotambua umuhimu wa kujiangalia wapi tumepotoka na tufanye nini kwenda mbele , otherwise kila kitu kitakachofanyika chini ya himaya tukufu hata kama ni takataka tutakisafisha kwa kuwabebesha walioko chini mzigo huku watukufu wakipunga upepo.
  Amkeni
   
 17. Researcher

  Researcher Senior Member

  #17
  Jul 22, 2011
  Joined: Dec 15, 2010
  Messages: 187
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Hapo kwenye red sidhani..majibu yake kwa maswali ya msingi kama janga la umeme yananipa hofu juu ya hilo.
   
Loading...