Rais Kikwete ana SIRI! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Rais Kikwete ana SIRI!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Saint Ivuga, Jul 30, 2011.

 1. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #1
  Jul 30, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,465
  Likes Received: 19,844
  Trophy Points: 280
  [h=3]Rais Kikwete ana SIRI![/h]
  [​IMG]  Kuna siri nzito ambayo mh. JK anayo na ninaamini inamtesa sana. Siri yenyewe ni kama ifutavyo:

  Kwamba watu anatuongoza hatutoi msaada kwake. Ninavyoelewa mimi ni kwamba kazi ya Rais sio kufikiri kwa niaba ya watu anaowaongoza. Kazi yake ni kusimamia mahitaji na matakwa ya watu anaowaongoza. Lakini kwa Tz ni tofauti. Kazi ya rais imekuwa ni kufikiri kwa niaba yetu.

  Mwl. Nyerere wakati anadai uhuru, aliamini kuwa watanzania ni wanadamu wenye utashi. Akataifisha mali ya wageni na kuwakabidhi wazawa, akiamini tunaelewa kama yeye alivyokuwa. Akatukabidhi viwanda, mashamba, nk. Lakini badala ya kwenda mbele, vikafa. Akashangaa, allah! nilidhani hawa jamaa tu kitu kimoja, kumbe!, akaamua kung'atuka.

  Mh. JK akaja na style tofauti. Akasema ngoja niwachokoze, maana siwaelewielewi!
  Akaenda kutuombea vyandarua, akiamini kwamba tutalipuka na kusema, haiwezekani, yaani tuombewe vyandarua?! Alitegemea pia kwamba tunatambua kwamba hivyo vyandarua baada ya muda fulani, vitachanika na hivyo tutajiuliza swali, Je! aende kutuombea tena? Lakini cha ajabu, kimyaaa! wote kwa ujumla wetu! Sasa anajiuliza, atumie njia gani ya kutufikishia ujumbe kwamba alitutania/alituchokoza tu ili tuzinduke? Na HATUJAZINDUKA! TUMELALA USINGIZI MZITO! Hivi ni kweli tunafikiri kwamba vikichakaa ataenda tena kutuombea?

  Mwanadamu ameumbwa kwa mfano wa Mungu na tumeumbwa tuvitawale viumbe vyote(kulingana na maandiko matakatifu). Je! sisi watz tumo? Kama tumo mbona mbu ametushinda? Utashi wetu uko wapi? Kama malaria ndio inaongoza kwa kuleta vifo hapa nchini, tunashindwa nini kumdhibiti mbu na uchafu?

  Ukiangalia mbinu tunazotumia kukabiliana na maradhi, utashangaa kabisa! Kuna jamaa walijenga hospitali ya kipindupindu pale buguruni, ajabu! (sina uhakika, lakini inawezekana ni nchi ya kwanza dunia kukijengea kipindupindu ghala la kuhifadhia badala ya kukikomesha). Watanzania mpo!? Kweli mpo?!

  Hivi ni kweli tunajisikiaje, kila rais wetu akikaa na marais wenzake, yeye ni kulia kila siku malaria inatumaliza. Si wanashangaa kwamba nchini kwake hana watu? Ni bahati mbaya wengi wetu huwa hatukai chini tukatafakari. JK amekuwa akiuliza maswali kadhaa ambayotungekuwa makini, yangetuumiza. Mojawapo aliwahi kusema, hivi wataalam tunaowapeleka nje ya nchi kusoma, huwa wanasoma nini? Kama ulishawahi kupelekwa nje ya nchi, jiulize ulienda kusomea nini? Kila mtu ajiulize! Baada ya kurudi amefanya nini? Inawezekana vya darasani hukuvielewa, vya kuona pia umesahau? Watu wa mazingira, mpo! wa afya nanyi mpo? manispaa Je!? wa fani nyingine nanyi mliona nini? mliumwa na mbu kule? mliumwa malaria kule? Kama hamkuumwa, mlijiliza ni kwa namna gani mkirudi mtatatua hilo tatizo? Au niwatanie kwamba wengi wetu tukirudi fikra zetu zinabaki kuwaota wazungu na kutamani kuwa kama wao wanavyoonekana na si wanavyotenda. Ndio maana sasa hivi ukitafuta mtu halisi unaweza kupata wakati mgumu.

  Nywele kama wazungu! Rangi kama wazungu! Ni hayo tu ndio nayaona tumefanikiwa sana! Wenzetu walishajitambua thamani yao na ndio maana wakajipambanua na kujitofautisha na wanyama wengine kwa sababusi class ya wanyama wengine.

  Tukichukua mfano, jiulize kwanini taka zimezagaa kila mahali hasa kwenye miji mikubwa. Taka za kuzagaa zinatakiwa zionekane zile tu zinazozalishwa na mijusi au viumbe visiyokuwa na akili. Wewe mwanadamu unatakiwa utumie akili yako na kuhakikisha kuwa taka unazozalisha huzitupi ovyo. Sasa angalia ambavyo hatutumii akili. Zile taka unaitupa ovyo ukidai huoni dustbin. Taka zile zinazagaa, zingine zinaanguka na kujaa kwenye mitalo. Mvua ikinyesha, maji machafu yanazagaa na kutuletea magonjwa. Tukienda hospital dawa hamna, tunalalamika. Lakini CHANZO CHA TATIZO NI WEWE MWENYEWE! Hapo ndipo wenzetu wanapotucheka, hawa jamaa vipi? utashi wao uko wapi?Ukiwaambia magari yote ya abiria yawe na dustbins, utaambiwa ooh! magari ya wakubwa. Sasa wakubwa si ndio hasa wanatakiwa watuonyeshe njia? Kuliwahi kutokea tangazo la tigo la jamaa kuachwa na gari wakati akichimba dawa, na watu hatukuona tatizo/udhalili wa lile tangazo. Hivi kweli walishindwa hata kusema jamaa akiachwa akimshangaa pundamilia!!!

  Niliwahi kuongea na Mh. mmoja kwamba wajitahidi kuwaelimisha watu na kusimamia taratibu zilizowekwa kwa kuwa sasa hivi tuna vituo vingi vya TV na radio, akaniambia ni gharama! Nikashangaa! Tangu lini elimu ikawa rahisi? Au kwa sababu tulisoma bure?Basi tujaribuni ujinga kwa kuwa elimu ni gharama!!!
  Tufike mahali tujitambue thamani yetu na kusema tumechoshwa na kunyanyaswa na magonjwa badala ya kila siku tukiumwa, tunakimbilia hospitali bila kujiuliza kwanini tunaumwa. Kauli mbiu ya miaka 50 ya uhuru, kwamba tumethubutu, tumeweza, sijui nini! Huwa najiuliza, tumeweza katika sekta ipi? Vitu vya wachina kujaa madukani ndio kuweza? Used cars za wajapan zilizojaa barabrani ndio kuweza? Elimu down, umaskini juu, magonjwa juu, uchafu juu, vifo juu, michezo down, viwanda down, njaa juu, tumeweza wapi? Kama tumeshindwa hata kufagia, tunaweza nini? Kama unashika ganda la muwa au chungwa na ukalitupa tu ovyo, unaweza nini? Utashi wako uko wapi? Tumelogwa, au ni pepo!?

  Kwa mtazamo wangu, badala ya kusema tumeweza, tulipaswa kusema tumetambua tulipoangukia, sasa tunasimama na kuanza hatua ya kwanza. Jamani tutokomeze maradhi kwa kuweka mazingira safi. Kila mtu ajione ni mjinga pale anapotupa taka iwe ni dirishani mwa gari, iwe ni kwenye mtalo, iwe ni kukojoa ovyo, nk. Bila kujitambua sisi wenyewe na kuacha tabia za uchafu kwa mtu mmoja mmoja, magonjwa yataendelea kututesa daima na juhudi zinazofanywa na mamlaka za kufanya usafi kila Jumamosi ya mwanzo wa mwezi hazitaweza kufanikiwa kwa kuwa unaweza ukafagia sasa na mimi nikatupa uchafu dakika 2 zijazo na kufanya usafi uliofanya ukawa bure. Tuwe tunathubutu kuwakumbusha wenzetu pale tunapoona wanakwenda kinyume.

  Tatizo kubwa ninaloliona ni kwamba tunaogopa kuthubutu. Kwa mfano jiji la Dar, utaambiwa ni jiji kubwa hivyo ni vigumu. Mimi naona ni rahisi sana. Hivi tukiwachukua wale vijana wanaopiga debe, tuwakawapa vitambulisho na kuwakabidhi hilo jukumu la kuwawajibisha watu, unadhani watashindwa? Cha muhimu ni kuwajulisha wahusika kwamba hao vijana watakuwepo mtaani kwa ajili ya kazi hiyo na kila mtu ajue hivyo. Baada ya hapo ni utekelezaji.Nadhani hawawezi kushindwa.Wanachohitaji ni kibali tu na waambiwe wakimkamata wachukue kiasi gani kwa huyo mtu na akibisha wampeleke wapi.

  TAFAKARI NA UCHUKUE HATUA!
   
 2. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #2
  Jul 30, 2011
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 444
  Trophy Points: 180
  He is just remotely controlled
   
 3. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #3
  Jul 30, 2011
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 444
  Trophy Points: 180
  Alidhani Ikulu ni mahali pakucheka cheka hovyo
   
 4. p

  pimbika Member

  #4
  Jul 30, 2011
  Joined: Apr 19, 2011
  Messages: 75
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ngojangoja huumiza matumbo. bado matatizo yanazidi kuja ndo kwanza mwaka wa kwanza.
   
 5. mashikolomageni

  mashikolomageni JF-Expert Member

  #5
  Jul 30, 2011
  Joined: Jan 5, 2010
  Messages: 1,565
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Comedian
   
 6. Adrian Stepp

  Adrian Stepp Verified User

  #6
  Jul 30, 2011
  Joined: Jul 1, 2011
  Messages: 2,222
  Likes Received: 596
  Trophy Points: 280
  kukenua!! alidhani tunataka magego yake kama mndengereko!
   
 7. ndetichia

  ndetichia JF-Expert Member

  #7
  Jul 30, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 27,641
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  anataka kutoa hitimisho la uongozi wake..
   
 8. ndetichia

  ndetichia JF-Expert Member

  #8
  Jul 30, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 27,641
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  <br />
  <br />
  tena joti asienamaono kama masanja..
   
 9. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #9
  Jul 30, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,465
  Likes Received: 19,844
  Trophy Points: 280
  someni thread kabla ya kuchangia....mishale haiendi kwa jk inakwenda kwenu nyinyi watanzania.............kumbe watu mnachangia kabla ya kusoma eee
   
 10. TUKUTUKU

  TUKUTUKU JF-Expert Member

  #10
  Jul 30, 2011
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 11,852
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Au mahali pakuuza sura!!
   
 11. malkiory

  malkiory JF-Expert Member

  #11
  Jul 30, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 272
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ni article nzuri sana, lakini angalia upande mwingine wa shillingi. Mazingira ya nyumbani ni frustrating, hata mtu angekuwa na PhD 20 baada ya kurudi tanzania ni lazima PhD yake itaota kutu. Nchi ambayo haina sera chanya za kuleta maendeleo unategemea wasomi hao wangefanya miujiza bila kuwezeshwa na serikali. Ukombozi wa kifikra inabidi uanzie kwa viongozi, waache ufisadi na waweke maslahi ya taifa mbele. Rais Kagame ni mfano wa kuigwa, lakini siyo raisi wetu uliyemtaja hapo kwenye article yako, hana hiyo vision.
   
 12. Mtoboasiri

  Mtoboasiri JF-Expert Member

  #12
  Jul 30, 2011
  Joined: Aug 6, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 94
  Trophy Points: 0
  <br />
  <br />


  Siamini ana intellectual capacity kufanya ulicho post hapa. Ila nakubaliana na wewe kuwa kuna haja ya kuchukua hatua individually
   
 13. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #13
  Jul 30, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,465
  Likes Received: 19,844
  Trophy Points: 280
  kama huoni wengine wataona
   
 14. TUKUTUKU

  TUKUTUKU JF-Expert Member

  #14
  Jul 30, 2011
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 11,852
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Mkuu naomba utuome radhi,ninachofahamu mimi watanzania walijitahidi,wamejitahidi na wanaendelea kujitahidi kufanya kazi kwa juhudi lakini tatizo kubwa wanalokabiliana nalo ni kukosa mazingira mazuri ambayo yangewekwa vizuri na serikali yao basi wangekuwa mbali sana.Kwa mfano wakulima wanajitahidi kulima mazao mbalimbali lakini kwa bahati mbaya wamekosa masoko ya uhakika ya kuluza mazao yao au wakipata masoko hulazimika kuuza mali ghafi ambayo mwisho wa siku upata fedha kidogo sana na kuwadidiza kimaendeo na kuwaongezea ufukara.
  Serikali imeshindwa kusambaza mbembejeo na madawa ya wadudu kwa wakulima na kwafanya washindwe kupata ufanisi mkubwa katiak shughuli zao za killimo.Kwa upande mwingine serikali imeshindwa kuboresha mazingira ya utalii na kusababisha fedha nyingi za kigeni kupotea,ukitaka kujua hili linganisha mazingira ya utalii ya Tanzania na yale ya kenya,pia jaribu kulinganisha ni nchi ipi iana vitutio vingi vya uatalii kiasili.
  Serikali hiyo hiyo imeshindwa kutengeneza miundombinu ya uhakika ambayo ingelaisisha kuchochea maendeleo,mfano unategemea mkulima wa Kigoma hakauze mazao yake wapi wakati mkoa wakeumejitenga na mikoa yote kutokana na kukosa miundo mbinu ya uhakika?
  Madini na rasili mali nyingine zinaibia na kutoa mchango mdogo sna katiaka maendeleo ya nchi yetu,unategemea mwananchi afanye nini wakati serikali yake inafanya vitu vya ajabu?
  Hitimisho:Kwa hayo machache niliyoyazungumzia bado yanaonyesha kwa kiwango kikubwa umasikini na ufukara umeshabaishwa na ulegelege wa serikali ya CCM!
   
 15. Speaker

  Speaker JF-Expert Member

  #15
  Jul 30, 2011
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 6,357
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Kua na siri kunalisaidiaje taifa letu?
  kama anasiri anasubiri nini kuitoa?

  so tumuite raisi wa siri? (secret president ) huh?

  nakumbuka pia anasiri ya wauza madawa ya kulevya
  nakumbuka pia anasiri ya majambawazi
  nakumbuka pia anasiri ya wachungaji wauza mihadarati
  nakumbuka pia anasiri ya mafisadi
  nakumbuka pia anasiri ya umasikini wa Tanzania
  nakumbuka pia anasiri ya mgao wa umeme
  nakumbuka pia anasiri ya kujivua magamba

  anasiri nyingi sana,swali ni lini zitatoka hizo siri au kuzitunza kwake kunamanufaa gani?
   
 16. Mtoboasiri

  Mtoboasiri JF-Expert Member

  #16
  Jul 30, 2011
  Joined: Aug 6, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 94
  Trophy Points: 0
  &lt;br /&gt;<br />
  &lt;br /&gt;<br />
  Saint Ivuga, suala sio mimi kuona (which implies wewe unaamini jk ana intellectual capacity unayom-credit nayo ila mimi nimeamua kutoiona lakini wengine wataiona). The matter of fact is angekuwa na uwezo huo he would have done things differently. Unless unataka kutuambia unaridhika na uongozi wake
   
 17. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #17
  Jul 30, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,465
  Likes Received: 19,844
  Trophy Points: 280
  siriziki na uongozi wake hata kidogo .. na siwezi kumkubali Lowasa hata siku moja .. wote hao ni wamoja...lakini kwa nini tutake kutafuniwa kila kitu? Kikwete hana tatizo hata moja.. tatizo ni watanzania and even small kid can prove this i swear
   
 18. Mark Francis

  Mark Francis Verified User

  #18
  Jul 30, 2011
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 605
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Article nzuri sana kwa sababu inauma pande zote 2 za serikali na raia wa kawaida. Ili kupata maendeleo inabd tujitambue na kutumia akili na utashi wetu wa kibinadamu katika kutenda mambo mbalimbali. Kwa upande wa serikali, inaonesha wazi imelala kwa sababu jukumu lingine la serikali ni ku-enforce sheria, sasa kama wenyewe ndio wavunjaji wakubwa wa sheria unafikiri nani mwingine atakayeweza. Serikali inabd iwe kioo cha jamii kwa kutenda yale yanayotakiwa na jamii itajifunza kutoka kwao. Tukiishi hivyo kwa kila mtu kutimiza wajibu wake vizuri, tutasonge mbele.
   
 19. Zing

  Zing JF-Expert Member

  #19
  Jul 30, 2011
  Joined: Jun 24, 2009
  Messages: 1,780
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0
  Kuna ile ya EPA sijui nayo ni siri au kwa kuwaaliwaruhusu warudishe taratibu sio siri tena. Je ni kina nani ha waliorudisha. Nayo anayo.
   
 20. Jigsaw

  Jigsaw JF-Expert Member

  #20
  Jul 30, 2011
  Joined: Jun 17, 2011
  Messages: 1,817
  Likes Received: 152
  Trophy Points: 160
  Sijaona siri yoyote ya ikwete hapa...!!
   
Loading...