Rais Kikwete afanya uteuzi mpya tume ya utumishi na usuluhishi.

MNYISANZU

JF-Expert Member
Oct 21, 2011
7,048
1,102
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, amefanya uteuzi wa Wenyeviti wa Tume ya Utumishi wa Umma na Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA).

Katika uteuzi huo, Rais amemteua Mhe. DKT. STEPHEN JAMES BWANA, Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani, kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Umma na BWANA EDRISSA R. MAVURA, kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA), Bw. Mavura ni Naibu Katibu Mkuu Mstaafu.

Sambamba na uteuzi huu, Rais amewateua Makamishna katika Tume hizo, ambapo Makamishna wa Tume ya Utumishi wa Umma ni:
(i)Bwana George D. YAMBESI, Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma.
(ii)Alhaj Y. F. MBILA, Katibu Tawala wa Mkoa mstaafu.
(iii)Bwana Mgeni Mwalimu ALLY, Kamishna wa Tume ya Utumishi wa Umma iliyomaliza muda wake.
(iv)Bibi Adieu H. NYONDO, Mkurugenzi wa Maadili mstaafu.
(v)Bibi Salome S. MOLLEL, Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu mstaafu, Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali
(vi)Bibi Evelyne ITANISA, Katibu Tawala wa Mkoa mstaafu.
Aidha Makamishna wa Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA) ni:
(i)Bwana Paul Herbert Kinemela, Kamishna wa Kazi, Wizara ya Kazi na Ajira
(ii)Bwana Mathias Bazi Kabunduguru, Mkurugenzi wa Uendeshaji Sera, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma.
(iii)Bwana Njaa Ramadhani Kibwana, Naibu Katibu Mkuu, Chama Cha Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa (TALGWU).
(iv)Bwana Jones Kyaruzi Majura, Naibu Katibu Mkuu, Chama Cha Wafanyakazi wa Sekta ya Biashara na Viwanda – (TUICO).
(v)Bwana Jaffari Ally Omari, Mwanasheria Kiwanda cha Sukari – TPC, na Kamishna wa Tume iliyomaliza muda wake.
(vi)Bibi Suzane Charles Ndomba, Afisa Sheria wa ATE na Wakili wa Mahakama Kuu.

Uteuzi huu umeanza tarehe 23 Februari, 2015.
 
Hivi vijana watapata lini kazi, kitendo cha kuwarudisha wastaafu kinaliingiza taifa kwenye matumizi yasiyo lasimi, mtu amestaafu yupo kwenye pension na kulea wajukuu wewe unampa majukumu mapya, hivi JK akistaafu kwenda Msoga Rais Mtarajiwa Tundu Lisu akimteua kuwa Msajiri wa Vyama vingi atakubali?
 
Mkuu hizo nafasi ni sahihi kabisa kupewa hao wazee. Ukipata matatizo kazino ndio utaekewa
 
Hivi vijana watapata lini kazi, kitendo cha kuwarudisha wastaafu kinaliingiza taifa kwenye matumizi yasiyo lasimi, mtu amestaafu yupo kwenye pension na kulea wajukuu wewe unampa majukumu mapya, hivi JK akistaafu kwenda Msoga Rais Mtarajiwa Tundu Lisu akimteua kuwa Msajiri wa Vyama vingi atakubali?

Mkuu hizo nafasi ni sahihi kabisa kupewa hao wazee. Ukipata matatizo kazini ndio utaelewa
 
Hivi vijana watapata lini kazi, kitendo cha kuwarudisha wastaafu kinaliingiza taifa kwenye matumizi yasiyo lasimi, mtu amestaafu yupo kwenye pension na kulea wajukuu wewe unampa majukumu mapya, hivi JK akistaafu kwenda Msoga Rais Mtarajiwa Tundu Lisu akimteua kuwa Msajiri wa Vyama vingi atakubali?

Hizo ni tume na huishi kwa vikao tu kijana sio ajira hizo....
 
mwache amalizie kuwapa nafasi waliompigia kampeni asibakiwe na deni mda mchache umebaki
 
nini tafsiri yake ki siasa na kiutawala katika kuelekea uchaguzi mkuu?
 
Dah!!vijana tutaendelea kufia tu mitaaani hata sehemu ya kupatia ujuzi hakuna
 
Lini baba yangu mzee Ogiro mkulima wa jembe la mkono kule Rorya atakuwa hata mfagiaji katika ofisi hiyo?.Keki ya taifa iende kwa kila kaya.
 
nini tafsiri yake ki siasa na kiutawala katika kuelekea uchaguzi mkuu?

Matumizi holela ya rasilimali zetu, kila siku uteuzi uteuzi haijulikani wateuliwa wanafanya kazi gani na wapi, ama kweli bomba letu la kuingiza maji ndani ni dogo kuliko linalotoa
 
wazee ndo hazina ya taifa lolote. ndipo zilipolala hekima. Vijana mna matamanio kama yule HUMAN RESOURCE MANAGER wa kampun ya SMILE COMMUNICATIONS pale ilkuwa hupati kazi bila kutoa uchi/ti.go
 
Jamani hizo kazi zingine kwa jinsi ninavyofahamu zinataka uzoefu wa muda mrefu, fresh from school hawezi kumudu majukumu kama hayo
 
wazee ndo hazina ya taifa lolote. ndipo zilipolala hekima. Vijana mna matamanio kama yule HUMAN RESOURCE MANAGER wa kampun ya SMILE COMMUNICATIONS pale ilkuwa hupati kazi bila kutoa uchi/ti.go
blessings kwa mfano joka lenye makengeza ana hekima gani?
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom