Ghazwat
JF-Expert Member
- Oct 4, 2015
- 23,718
- 66,267
Kwenye taarifa ya kuadhimisha miaka minne ya utawala wake, alisema kumekuwa na mafanikio mengi kuliko yaliyofanywa tangu Kenya ipate uhuru.
"Ninajivunia kuwa ugatuzi sasa umetekelezwa kikamilifu. Ninaamini historia itamkumbuka wajibu wa utawala katika kipindi hiki cha mageuzi kwa nchi yetu", alisema huku akikumbuka Aprili 9 kama siku muhimu kwake alipoapishwa kama Rais.
"Juhudi zetu ziliongozwa na utekelezaji wa kiapo changu kuheshimu, kulinda na kutetea Katiba yetu na pia kwasababu ninaamini ugatuzi kama muundo bora wa uongozi".
Hata hivyo viongozi wa upinzani walipuuzilia mbali mafanikio yaliyotajwa wakisema wananchi wamezidi kutaabika chini ya utawala wake. Naibu Kiongozi wa Wachache Bungeni Bw. Jokoyo Midiwo alisema utawala huu utakumbukwa tu kwa ufisadi na ubaguzi wa kikabila katika utoaji wa vyeo Serikalini.
"Kuanzia masuala unyakuzi wa ardhi hadi sakata kubwa la kiuchumi, na jinsi Rais mwenyewe alivyokiri hajui la kufanya kukabiliana na ufisadi, hii Serikali imefeli kabisa", alisema Midiwo
Chanzo: TaifaLeo