Rais Karume Kuutangazia Umma Leo

Junius

JF-Expert Member
Mar 11, 2009
3,181
139
Makamo Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Zanzibar, Rais Amani Abeid Karume leo anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika mkutano mkubwa ulionadaliwa na chama hicho kwa lengo kuelezea mazungumzo ya kisiasa yaliyofikiwa kati yake na Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi (CUF) Maalim Seif Sharif Hamad.

Mkutano huo ambao utakuwa ni wa mwanzo wa chama hicho kuzungumzia mazungumzo ya viongozi hao yaliobatizwa jina la ‘Maridhiano’ unatarajiwa kuwa wa aina yake katika viwanja vya Demokrasia Kibanda Maiti ambapo imeelezwa kwamba utapambwa kwa vikundi mbali mbali vya burudani kabla ya kuanza kwa mkutano huo.

Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na Umoja wa Wazazi wa Jumuiya ya CCM na kusainiwa na Naibu Katibu Mkuu wake, Yasmin Aloo na kusambazwa kwa vyombo vya habari imewataka wanachama na wafuasi pamoja na wakereketwa wa chama hicho wa mikoa yote mitatu ya Unguja kujitokeza kwa wingi kuhudhuria mkutano huo.

Wakati Chama Cha Mapinduzi (CCM) kikitarajiwa kuwatangazia wanachama wake suala la mazungumzo ya Rais Karume na Malim Seif tayari Chama Cha Wananchi (CUF) kimeshawaelezwa wanachama wake suala hilo na kuwaomba wanachama wote wa CUF na wazanzibari kuunga mkono mazungumzo hayo ambayo yana azma ya kuleta umoja na maridhiano kwa wazanzibari wote bila ya kujali itikadi za kisiasa walizonazo wanachama hao.

Mkutano wa CCM wa leo utakuwa ni mkutano wa kwanza kwa wafuasi wa chama hicho kupokea tamko la Rais wa Zanzibar Amani Abeid Karume tokea alipokutana Ikulu Unguja na kufanya mazungumzo na Katibu Mkuu wa CUF Maalim Seif Sharif Hamad Novemba 5 mwaka huu mazungumzo ambayo yameelezwa kuwa na nia ya kumaliza uhasama na chuki za kisiasa kati ya pande mbili hizo.

Ni siku moja tu baada ya viongozi hao kukutana Ikulu na kufanya mazungumzo ya faragha yaliochukua takriban masaa mawili mazungumzo ambayo hatima yake yamesababisha Chama Cha Wananchi (CUF) kuregeza msimamo wake wa kutomtambua Rais Karume kuwa ndiye Rais halali wa Zanzibar.

Akiutangazia umati mkubwa katika viwanja vya Demokrasia Novemba 7 mwaka huu Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi (CUF) Maalim Seif Sharif Hamad alisema uongozi wa baraza kuu umeamua kumtambua Rais Karume kuwa ndiye Rais halali wa Zanzibar kauli ambayo ilipingwa vikali na wafuasi wa chama hicho kwa upande wa Unguja na kumshutumu kiongozi wao kuwa amewasaliti wanachama wake.

Kufuatia kauli hiyo wafuasi hao walipiga kelele za kutotaka kutambuliwa Rais Karume huku wengine wakiangua vilio hadharani na kusema hawakubaliani na tamko hilo jambo ambalo lilisababisha Mwenyekiti wa chama hicho Professa Ibrahim Lipumba kupanda jukwaani na kuwaomba wafuasi hao wakubaliane na maamuzi hayo kwa kuwa hayo sio maamuzi ya Maalim Seif bali ni uamuzi wa baraza kuu la uongozi wa CUF.

Hata hivyo Professa Lipumba aliwaambia wafuasi hao kwamba Maalim Seif hajawahi kuwa msaliti katika historia ya maisha yake katika siasa, hivyo sio sawa kumuona kama amekisaliti chama na wafuasi wake na kuwataka wote wakubaliane na tamko hilo kwa lengo la kujenga umoja na mshikamano kwa maslahi ya wazanzibari wote.

Wakati hayo yakifanyika Unguja wafuasi wa chama hicho Kisiwani Pemba walilipokea tamko hilo kwa furaha na kuwapongeza viongozi hao kwa ujasiri mkubwa waliounesha kwa kukutana na kuweza kuzungumzia maslahi ya zanzibari na watu wake.

Wiki moja baada ya wafuasi wa CUF kumkatalia hadharani Maalim Seif kumtambua Rais Karume Umoja wa Wanawake wa CUF walitoa taarifa kwa vyombo vya habari kuunga mkono mazungumzo hayo pamoja na kuitisha maandamano makubwa yaliofuatiwa na mkutano ambayo ulimuomba radhi Katibu Mkuu wao kwa kitendo walichokionesha Novemba 7 cha kujiliza hadaharani wakisema wamekijutia kwa kuwa walikuwa hawajaelewa azma na lengo la mazungumzo ya viongozi hao wawili.

Tayari Chama Cha CUF kimeshafanya mikutano miwili ya hadhara kwa ajili ya kuwajulisha wafuasi wao kuhusu nia ya kumtambuwa Rais Karume kama kiongozi halali wa Zanzibar aliyeshinda katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2005.

Chimbuko la kutotambuliwa Rais Karume na Chama Cha Wananchi CUF ni mara baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2005 ambapo CUF kilikataa matokeo ya uchaguzi huo na kusema hakitamtambua kuwa ndie Rais halali kwa madai kuwa hajashinda katika uchaguzi huo kwa kuwa uchaguzi ulikuwa na hila na udanganyifu katika mchakato mzima wa uchaguzi wenyewe.

Kwa mujibu wa taarifa ya CCM imesema kwamba viongozi wote wakuu wa Chama Cha Mapinduzi Zanzibar pamoja na viongozi wa serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar watahudhuria mkutano huo na kuhutubiwa na Rais Amani Karume.

Awali kulikuwa na fununu kwamba Kamati ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi CCM kukutana Zanzibar siku moja kabla ya mkutano huo wa hadhara kuelezwa juu ya suala zima la mazungumzo na kutoa baraka zake kama ilivyofanywa kwa upande wa CUF kuwaita barza kuu la uongozi kuwaeleza suala hilo.

Akizungumza kwa njia ya simu Katibu wa Idara ya Uenezi wa CCM Zanzibar, Vuai Ali Vuai alisema hakuna kikao cha halmashauri kuu ya CCM Zanzibar kitakachofanyika zaidi ya mkutano ambao umeandalwia na chama hicho kufanyika leo Unguja.

Mkutano wa leo unatazamiwa kuhudhuriwa na wanachama na wafuasi wa wa CCM na wafuasi wengine wasiokuwa wa CCM wa mikoa mitatu ya Kusini, Kaskazini na Mjini Magharibi Unguja ambapo hadi haijaelezwa kama kwa upande wa Pemba mkutano kama huo utapangwa lini.

Nchi mbali mbali za Umoja wa Ulaya wakiwemo washiriki wa maendeleo wamepongeza mazungumzo yaliofikiwa Novemba 5 Ikulu Unguja kati ya Rais wa Zanzibar Amani Abeid Karume na Katibu Mkuu wa CUF Maalim Seif Sharif Hamad yenye lengo la kumaliza mivutano ya kisiasa na kujenga Zanzibar mpya yenye mashirikiano na umoja.

Hii itakuwa ni mara ya nne kuafikiwa kwa mazungumzo ya kutafuta mwafaka wa kisiasa ambapo awali mazungumzo hayo yalifanyika mwaka 1999 wakati wa utawala wa Dkt Salmin Amour Juma mazungumzo ambayo hayajatekelezwa.

Mwafaka wa pili uliafikiwa mwaka 2001 baada ya watu kadhaa kufariki dunia kufuatia maandamano yaliopangwa na Chama Cha CUF mara baada ya kukataa kuyatambua matokeo ya uchaguzi wa mwaka 2000.

Mwafaka wa tatu ulitangazwa na Rais Kikwete mara baada ya kuingia madarakani na kutangaza kuwa atamaliza mpasuko wa kisiasa Zanzibar mazungumzo ambayo yalidumu kwa miezi 14 ambapo pande mbili hizo kuvutana na mazungumzo hayo kusimamishwa ghafla.

source: zanzibar yetu web blog
 
Tusubiri tuone lakini msimamo wetu haubadiliki ni kwa ajili ya maslahi ya zanzibar tu na si kuwa tunampapatikia Karume na CCM mafisadi wenziwe.
 
Tusubiri tuone lakini msimamo wetu haubadiliki ni kwa ajili ya maslahi ya zanzibar tu na si kuwa tunampapatikia Karume na CCM mafisadi wenziwe.

Development so far?Tunavinjari out ,tujalia taarifa mpya.
 
Tusubiri tuone lakini msimamo wetu haubadiliki ni kwa ajili ya maslahi ya zanzibar tu na si kuwa tunampapatikia Karume na CCM mafisadi wenziwe.


Acheni uwongo huo!!!
Hii ni kwa maslahi yenu tu. Tunakujuweni vizuri sasa. Mshaona hapo mtafaidika.
Kwani maslahi ya Zanzibar ndio kwanza leo baada ya miaka 10 muyajuwe? Mmefika kuulisha wenzenu na leo mnasema kuwa ni kwaajili ya Zanzibar???
Kama kweli ni kwaajili ya Zanzibar kulikuwa na haja ya kuwapoteza wale wa Zanzibari wenzenu????
Acheni tamaa hizo!!!
CCM washakufixini kwa tamaa zenu na mwakani hata mkiibiwa kweli katika uchaguzi hakuna atakaekuaminini tena na wala msiwaendee mabalozi DSM kuwalilia tena!!!!!!
 
Acheni uwongo huo!!!
Hii ni kwa maslahi yenu tu. Tunakujuweni vizuri sasa. Mshaona hapo mtafaidika.
Kwani maslahi ya Zanzibar ndio kwanza leo baada ya miaka 10 muyajuwe? Mmefika kuulisha wenzenu na leo mnasema kuwa ni kwaajili ya Zanzibar???
Kama kweli ni kwaajili ya Zanzibar kulikuwa na haja ya kuwapoteza wale wa Zanzibari wenzenu????
Acheni tamaa hizo!!!
CCM washakufixini kwa tamaa zenu na mwakani hata mkiibiwa kweli katika uchaguzi hakuna atakaekuaminini tena na wala msiwaendee mabalozi DSM kuwalilia tena!!!!!!
Baada ya 2010 na deal hili li-bauns..which is most likely to happen with CCM ninao wafahamu CUF ndio kwisha habari yake...kitakachotokea ni kati yafuatayo:-
a) wanachama watagombana na viongozi (lipumba kashasema hii ni pata potea)
b) kutakuwa na mpasuka mkubwa kwenye chama cha upinzani na haya ndio malengo ya CCM kuwagombanisha viongozi wa CUF na wanachama
c) Makundi hayo yatakuwa makubwa na wenye kutofautiana misimamo..that will be end of strong CUF..tusibiri tuone.
 
Tusubiri tuone lakini msimamo wetu haubadiliki ni kwa ajili ya maslahi ya zanzibar tu na si kuwa tunampapatikia Karume na CCM mafisadi wenziwe.

Mkuu haushutuki kidogo kwamba huku kupatana kwa CCM-Z'bar na CUF kuna kuja mwaka mmoja kabla ya uchaguzi wa raisi? Tena una kuja mwaka ambapo incumbent anaondoka? Haiku shtui kwamba miaka yote ya mikutano ya "muafaka" leo hii ghafla wana patana? Je una amini kabisa kwamba hakuna makubaliano ya nyuma ya mlango kama Karume na Seif wanavyo dai? Ila ilimradi mmekubali wenyewe tusisikie kelele za faulu next year.

Halafu mimi hili swala la "kwa ajili ya maslahi ya zanzibar" ina nipaka utata sana. kwani CCM na CUF ni vyama vya Zanzibar tu? Vyama hivi si vina takiwa kutetea maslahi ya taifa na wananchi wote? Wenzenu CCM tayari wana nguvu Bara lakini CUF ikiendelea kuonyesha kuwa ni chama cha kutetea Wazanzibar tu mtaona madhara yake baadae.
 
Wakuu,
Nawashukuru kwa maoni yenu ila siku zote CUF imekuwa mstari wa mbele kuhakikisha kuwa kuna kuwa na mazingira ya siasa za ushindani wa kistaarabu,kupingana bila kupigana. Hali hii tumeendelea nayo muda mrefu bila ya wenzetu kutuelewa,tumefanya kila jitihada kuhakikisha, rejea makubaliano yaliyopita vyanzo na mtokeo yake, zanzibar kuna amani na utulivu au tanzania kwa ujumla, wakati wote.
Hapa hatudanganyi, tunajuwa kuwa katika siasa maslahi ni kuaminiwa na kukubalika na umma,na CUF hilo halina shaka, inakubalika na umma.
Ninacho wahakishieni kuwa CUF inajuwa inachokifanya na haijakurupuka kumtambua rais Karume na hii si kwa kauli ya Katibu Mkuu bali kwa kauli ya Chama kwa ujumla kuwa hatujachemsha na injini ipo o.k,
Wakuu, tunaposema maslahi ya zanzibar tunarejea hali ya mitafuruku inayotokezea kila wakati wa uchaguzi zanzibar na jambo ambalo halina maslahi kwa wananchi na kwa taifa kwa ujumla.
Hatuna haja ya kushituka kwa kuwa siasa siku zote ina kanuni maalumu ya kizama kuwa hakuna adui na rafiki wa kudumu...tunajuwa kuwa tumefikia hatua hii huku kumbukumbu zetu zikirejea katika Muafaka wa mwanzo na mwisho,tukijuwa ugeu geu wa chama tawala na nguvu zao za kidola, ila kwa mikakati ya kichama iliyopangwa tupo pamoja na wananchi ambao ndio wahanga wakubwa itokezeapo rabsha na machafuko. we will not be the first to raise up arm against others...mantaining our right to defence simultenously
 
Vipi, hotuba bado inaendelea??
Zimebaki simulizi tu...rais kaweka wazi na katambua kwa Maalim Seif ni Kiongozi mwenye kuthubutu na jasiri...kasema kweli au vipi?!!
 
Zimebaki simulizi tu...rais kaweka wazi na katambua kwa Maalim Seif ni Kiongozi mwenye kuthubutu na jasiri...kasema kweli au vipi?!!


Amesema ukweli na amefanya la msingi, wazanzibari wanajua zaidi maana ya hili agano kuliko mtu mwingine yeyote!!

Nashkuru waliopewa dhamana ya amani wamegundua wajibu wao na wanautekeleza kwa vitendo
 
Back
Top Bottom