Rais Kagame asema atapunguza safari za nje kwa watumishi wa umma, amuunga mkono Magufuli

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Rais wa Rwanda Paul Kagame amesema hatavumilia matumizi holela ya fedha za walipa kodi nchini mwake, amesema anakubaliana na hatua anazochukua rais wa Tanzania, Dkt. Magufuli.

Amesema hayo akiwahutubia viongozi nchini mwake waliohudhuria semina maalum ya kujitafakari.

Amesema hatavumilia safari zisizo na tija, na atazipunguza kwa kiasi kikubwa.

Amesema fedha za safari zinatakiwa kutumika kwa ajili matatizo ya wananchi wake.

Pia amegusia mkutano wa wakuu wa nchi za Afrika Mashariki uliofanyika Arusha.

===========================

Pres.Kagame says he can't stomach excessive travel & will have the courage to cut it drastically like

Pres. Kagame says we can't afford all this travel,money needs to be solving our problems.Says he agrees with MagufuliJP cuts

Pres.Kagame touches on excessive government travel! Touches on EAC "meeting" excuses
 
Within and outside our borders, the secret is out. And, the secret is that JPM is the man of the moment. Those with ears you better hear right and those with eyes shouldnt say i don't see. If you are blind and deaf, look for hearing aids or visual aid whatever fits your situation.
 
Wanatengeneza urafiki tu, na kauanza magufuli, jumamosi ya mwisho wa mwezi, usafi, magu na kagame ni political agenda, mkija kukumbuka hii, 10yrs hizo, kagame nae anaongeza term nyingine ehehhe i'm curious na siasa zetu africa....
 
Katika semina iliyoitishwa na Rais Paul Kagame wa Rwanda aliyoipa jina la "Tujitafakari" ambayo inafanana na ile Semina Elekezi iliyoasisiwa na Kikwete, Rais huyo amewaambia viongozi wa ngazi za juu wa Rwanda kwamba ameambukizwa maradhi ya kubana matumizi na Rais Magufuli wa Tanzania.
Amesema ana mpango wa kuzuia safari zote za nje kwa watumishi wa serikali siku chache zijazo, na kwamba anakubaliana kwa asilimia 100 na hatua anazochukua Magufuli katika kubana matumizi ya serikali.
Amesema hatavumilia hata chembe matumizi mabaya ya pesa ya serikali na kwamba katika hilo atakuwa mkali zaidi ya Magufuli.
 
Nilisoma gazeti moja, lilisema kwa sasa Afrika imepata sehemu ya kuanzia kiutawala maana akina Nyerere waliiga vitu vingi kutoka kwa wakoloni ndo maana tulishindwa kusimama. Sasa tusubiri nchi nyingi kuja na mifumo hii.
 
Katika semina iliyoitishwa na Rais Paul Kagame wa Rwanda aliyoipa jina la "Tujitafakari" ambayo inafanana na ile Semina Elekezi iliyoasisiwa na Kikwete, Rais huyo amewaambia viongozi wa ngazi za juu wa Rwanda kwamba ameambukizwa maradhi ya kubana matumizi na Rais Magufuli wa Tanzania.
Amesema ana mpango wa kuzuia safari zote za nje kwa watumishi wa serikali siku chache zijazo, na kwamba anakubaliana kwa asilimia 100 na hatua anazochukua Magufuli katika kubana matumizi ya serikali.
Amesema hatawavumilia hata chembe matumizi mabaya ya pesa ya serikali na kwamba katika hilo atakuwa mkali zaidi ya Magufuli.
Wengi watajifunza sema sio wote wataokiri wazi wazi. Sio tu kwa nchi za Afrika.
 
Katika semina iliyoitishwa na Rais Paul Kagame wa Rwanda aliyoipa jina la "Tujitafakari" ambayo inafanana na ile Semina Elekezi iliyoasisiwa na Kikwete, Rais huyo amewaambia viongozi wa ngazi za juu wa Rwanda kwamba ameambukizwa maradhi ya kubana matumizi na Rais Magufuli wa Tanzania.
Amesema ana mpango wa kuzuia safari zote za nje kwa watumishi wa serikali siku chache zijazo, na kwamba anakubaliana kwa asilimia 100 na hatua anazochukua Magufuli katika kubana matumizi ya serikali.
Amesema hatawavumilia hata chembe matumizi mabaya ya pesa ya serikali na kwamba katika hilo atakuwa mkali zaidi ya Magufuli.
acha kumdhalilisha kagame wewe!!! unamfanannisha na magufuli???
 
Mkuu yulejamaa ukiaacha upuuzi Wa kuongeza mwaka mbanaji mzuri TU Wa matumizi nikiwa Kyle alitoka safari akaagiza ijumaa magariyote ya serikali yawe godown ya mawaziri manaibu akamaliza akakutananao akapeleka kampuni ya Toyota akasema chagua wapo waliochagua wakapelekewa mkataba Wa kusaini hayoo magari n yao wanalipa polepole wapo walienda kubadili aina baada ya kujua mkopo..anawapa mafuta ltr kadhaa KWA wiki imeisha utanunua we we kaziya ser iendelee....
 
Mimi nadhani hata kama ni urafiki, urafiki wenye tija kwa wananchi hauna tatizo. Ni heri kujifunza mema kwa rafiki au mtu yeyote mtenda mema kuliko kujifunza mabaya kwa watenda mabaya!! Kama Rais Magufuli kujifunza utaratibu wa usafi nchi nzima kutoka Rwanda na kipindupindu kikakoma, je kuna ubaya gani Rais Kagame kujifunza utaratibu mzuri wa matumizi ya serikali kutoka Tanzania?! Nadhani Afrika Mashariki na hata Afrika kwa ujumla inahitaji viongozi wa aina hii.
 
Sio kila siku sisi tuwe wa kuiga iga tu, sasa nao waanze kuiga kwetu hongera Magufuli.
 
Back
Top Bottom