Rais Joseph Pombe Magufuli: Mzee Kikwete umeniachia kazi ngumu

"Haiwezekani, unaenda huku unakuta wafanyakazi hewa, ukigeuka huku unakuta balabala hewa, ukitizama kule unakuta wanafunzi hewa...yaani kila kitu ni hewahewa tu, kwa kweli mzee wangu Kikwete umeniachia mzigo mzito", haya ni maneno ya Rais wetu H.E JPM akimweleza mtangulizi wake tena bila kupepesa macho, kweli Rais tunae, hana chembe ya unafki, sasa ninazidi kumwelewa na niko tayali kumuunga mkono hata nikikosa sukari maana najua kutoka moyoni anatuwazia mema.

Nashauri tu asiyetaka kumwelewa Rais kwa sasa ahame tu nchi maana ni kama wiki sasa naona akina Ben Saanane wamekazana kumdhihaki, kama mnadhani watanzania tunahaja na Rais anayejua kuzungumza kingeleza kwa ufasaha basi tungeenda kumchukua mwingeleza atuongoze, go JPM go wataelewa tu.

maneno yako ni kweli kabisa
 
Kutoka moyoni mwangu raisi wetu tumepewa na Mwenye Enzi Mungu Mwenyewe....

Mwanzo 12:3 ubarikiwe sana sana raisi wetu JPM
 
Na ni kweli kabisa ni kazi ngumu sana kuongoza watu wanafiki kama watanzania wakati wa kikwete walilalamika maisha magumu ufisadi kaua uchumi wa nchi leo hii mtu anakuja bila hata aibu anasema wakati wa kikwete maisha yalikuwa mazuri kwa lipi?
 
Sema ukweli jappo ni miezi 7 tu. Maishga ya sasa unayaonaje ?? Kila kitu kiguumu watu sasa hawajengi na wako wanafunga biasharra zao
 
Wewe kuanzia lini maisha yamekuwa mazuri mahospilini dawa hakuna tangu enzi zile huduma za kijamii mbovu tangu enzi zile halafu anakuja mtu anasema maisha yalikuwa mazuri toka mjini uwatembelee na huko vijijini huduma mbovu kabisa tusidanganyane kuwa maisha yalikuwa mazuri hapana
 
Magu ni mzigo w Taifa! Hana suluhu kazi yake kulalamika! Alienda mwenyewe kuchukua form aliombwa? Au alidhania ni kukariri km za lami? Kama ameshindwa atoke hatukumfuata kumuomba! Alienda mwenyewe!! Tunataka suluhu ya mambo mtambuka sio kuja kulalamika! Mwananchi afanye nini kama yeye mtu wa mwisho kuamua analalamika? Hatutaki cheap politics
 
Anacheka lakini moyoni anaumia.
usidhani jk hamjui magufuli anamjua vizuri tu,ili uelewe alichokua anakisema magufuli lazima uwe bright kichwani.
Maana wengine mnajudge kama kwamba jk ndo aliwafundisha watanzania tabia za utapeli tapeli,
wakujilaumu ni watanzania wenyewe,jk angetaka kuwabadili mgelalamika kuwa eti ni dikteta,lakini kwa magufuli mtanyooka tu,maana yeye hana mambo ya kidiplomasia sana au sijui sheria sana,atakaeleta vyokovyoko anavyokolewa,
atakaegoma goma atakwenda kwao.
Mnalamlaumu kikwete kwa tabia mbaya za watanzania sasa inatakiwa mfurahi kwani tumempata mtu wa kuinyorosha nchi
na mtanyooka kweli kweli
 
We kweli kichwa Nazi kinavuja uteute sa huyo unaemuona ana uchungu na Nchi hi anafanya nini cha maana ambacho utasema Tz inapiga hatua zaidi ya kupiga mayowe ka ameshikwa sehemu mbaya
Bavicha hakuna hoja yamebaki matusi tu
 
Wewe utakuwa mtoto wa zinaa ndo maana huna adabu, Jpm hakuwa na maana hiyo mnayotaka kuzusha hapa, jpm anaamini amepewa urais na jk, thus y anasema amempa kazi nzito, si mara moja si mara mbili husema hivyo
Dogo punguza mikurupuko, na ujifunze adabu maamuma wewe.

Leo umekuwa msiri wa Ngosha mpaka kufahamu nini anawaza wakati akihutubia??

Au ni mahaba kwa JK yanakusumbua??
 
Huyu rais hajui afikeje anakotaka,haeleweke anaenda wapi wala kutupeleka wapi.Jk alilaumiwa kwa uzembe na ulegelege lakini hali ya maisha ilikua nafuu
 
teh teh teh.

Uzuri wa Kikwete hakuumbwa na aibu, hata umpige madongo hadharani anaishia kucheka cheka tu, kesho yake akimwalika hata kwenye kamsiba ka mtoto wa balozi wa nyumba kumi anatia timu tena kwa mbwembwe zote.

Huyo ndio JK mswahili pure......
Ila hii ya leo hajacheka aisee hata hotuba aliyotoa alikua amekaza sana mood
 
teh teh teh.

Uzuri wa Kikwete hakuumbwa na aibu, hata umpige madongo hadharani anaishia kucheka cheka tu, kesho yake akimwalika hata kwenye kamsiba ka mtoto wa balozi wa nyumba kumi anatia timu tena kwa mbwembwe zote.

Huyo ndio JK mswahili pure......
Ila kwa mara ya kwanza leo nimeona JK hajacheka wakati JPM anamwambia amempa kazi ngumu,
Nahisi ameanza kuchoka kuonekana kama vile hakufanya kitu
 
"Haiwezekani, unaenda huku unakuta wafanyakazi hewa, ukigeuka huku unakuta balabala hewa, ukitizama kule unakuta wanafunzi hewa...yaani kila kitu ni hewahewa tu, kwa kweli mzee wangu Kikwete umeniachia mzigo mzito", haya ni maneno ya Rais wetu H.E JPM akimweleza mtangulizi wake tena bila kupepesa macho, kweli Rais tunae, hana chembe ya unafki, sasa ninazidi kumwelewa na niko tayali kumuunga mkono hata nikikosa sukari maana najua kutoka moyoni anatuwazia mema.

Nashauri tu asiyetaka kumwelewa Rais kwa sasa ahame tu nchi maana ni kama wiki sasa naona akina Ben Saanane wamekazana kumdhihaki, kama mnadhani watanzania tunahaja na Rais anayejua kuzungumza kingeleza kwa ufasaha basi tungeenda kumchukua mwingeleza atuongoze, go JPM go wataelewa tu.

Vipi kuhusu ubakaji wa demokrasia Zanzibar? mimi nimeliona hili ni kubwa zaidi kuliko yote na yeye akiwa ndo amiri jeshi mkuu. Zanzibar ni kiza kitupu hadi sasa.
 
Kama kweli magufuli ni mzalendo katiba ya warioba ndio itakusaidia bila ya hivyo utapotea tu huna uwezo wakuwazibiti ccm
 
Inamaana hata suala la Sukari alirithi kwa Utawala wa JK?

Suala la kudhoofisha bunge kama chombo cha kuisimamia serikali alirithi kwa JK?

Kama hana Unafiki ni kwanini anafumbia macho suala la Bunge maana mtu asiye na chembe ya Unafiki anapenda mambo yawe wazi

Unasema eti bunge kuonyeshwa live humaliza muda wa wananchi ,mbona yeye alikua akihutubia akiwa Live TBC?

Kama huu sio unafiki basi labda sijui maana ya Unafiki

Kama yeye yupo real arejeshe Rasimu ya Wananchi tulijenge taifa upya tutatue matatizo kimfumo once and for all.

Kulalamikalalamika kwake huko hakumfanyi kuwa Rais Bora
Magu ni mkweli sana na hiyo inampa wakati mgumu reason being chama chake cha sisiemu ni direct opposite na mawazo yake.That is why Mr.President analalamika tu hawezi kufanya kitu for now coz people within the sisiemu hawana nia nzuri na sisi Watanzania....Believe me
 
Back
Top Bottom