comrade igwe
JF-Expert Member
- Jan 12, 2015
- 7,295
- 3,952

Kituo cha radio cha Angola kimetangaza kuwa, Rais Jose Eduardo dos Santos, ambaye ametawala taifa hilo kwa karibu miongo minne atajiuzulu kabla ya Uchaguzi, mwaka ujao.
Waziri wa Ulinzi, Joao Lourenco, anatarajiwa kuwa mkuu wa chama kinachotawala cha MPLA.
Bwana Dos Santos, ambaye ana umri wa miaka 74, wakati mmoja alikuwa kiongozi mdogo zaidi katika Bara la Afrika aliposhinda uchaguzi wa kuwa Rais akiwa na umri wa miaka 34 tu.
Amewahi kusema kuwa hatashiriki uchaguzi lakini baadaye akabadilisha maoni yake na kugombea tena.
Amekuwa akituhumiwa na makundi ya kupambana na ufisadi kwamba anaendesha serikali kama biashara binafsi.
Chanzo: Radio Angola