Rais John Magufuli akataa maombi ya kuugawa mkoa wa Tabora

hahahah mtanyooka tu. Tuliwaambia mlikuwa mnashabikia shetani sasa ona mnavyo jileta kiaina.
Katika uchaguzi watu wanashindana kwa sera, katika kusapoti au kupinga yanayoendelea yanatumikaje maneno ya kutukana? Umewahi kumuona shetani wewe?
Inaonekana huna malezi!
 
tuwe wastaimilivu ktk lugha tunazo tumia.
kwani sidhani kama rais anaweza kumrizisha kila mtu.

ni vizuri hata kama ni m.baya uka muacha na baya yake.
 
Ni kweli kuanzisha Wilaya na Mikoa mipya nikuongeza gharama za kuendesha serikali. Hivyo ni vyema kuacha siasa hizi kabisaa maana kuendesha Wilaya na Mikoa ni aghali wakati uzalishaji wetu ni mdogo..
 
Wanasema Tabora ina eneo kubwa kuliko mikoa mingine. Kwa hili la kugawa mikoa au wilaya kila kukicha halipendezi na ifike mahala hili jambo likikemewe kwa nguvu zote. Wanasiasa wanapenda kuvalia njuga ugawaji wa mikoa au wilaya kwa mbwembwe nyingi sana ili kufanikisha malengo na utashi wao.
Kuna mikoa au wilaya ukifika makao makuu ya mkoa au wilaya ni kama kitongoji, mkoa au wilaya haijajitosheleza kwa kuwa na miundombinu na huduma za kijamii za kutosha.
Ukijiuliza kulikuwa na sababu za kuugawa hupati jibu, ila ni utakutana na furaha ya kuwepo watu waliobahatika kupewa vyeo vya kimamlaka kutokana na ugawaji wa eneo, lakini kwa upande wa wananchi ni mafukara kupindukia na wala hawafaidiki na chochote.
 
Back
Top Bottom