Rais John Magufuli akataa maombi ya kuugawa mkoa wa Tabora

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,395
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 30 Julai, 2016 ameendelea na ziara yake katika Mkoa wa Tabora akitokea Mkoa wa Singida. Dkt John Magufuli.

Mkoani Tabora, Rais Magufuli amezungu
mza na wananchi waliosimamisha msafara wake katika vijiji vya Nanga na Ziba na amefanya mikutano ya hadhara katika miji ya Igunga na Nzega ambako amewahakikishia wananchi kuwa serikali yake itahakikisha inatekeleza ahadi zilizopo katika Ilani ya Uchaguzi Mkuu ya Mwaka 2015.

Katika mkutano wa hadhara uliofanyika Igunga, Rais Magufuli amepokea malalamiko ya wananchi kuhusu kutoanza kutumika kwa kituo cha mabasi na soko na amewaagiza viongozi wa Mkoa wa Tabora kuhakikisha kituo cha mabasi cha Igunga na soko la Igunga vinaanza kutumika kuanzia Jumatatu ijayo ya tarehe 01 Agosti, 2016.

Rais amekaa maombi ya Mkoa wa Tabora kutaka kuanzishwa Mkoa mwingine kutokana na ukubwa wa baadhi ya Wilaya Rais Magufuli amesema haoni umuhimu wa kuanzisha Mikoa mipya hapa nchini kwa sasa, na badala yake fedha zitaelekezwa katika huduma kwa wananchi kama vile maji, barabara, miundombinu na huduma za afya.

Kabla ya kuingia Mkoani Tabora, Rais Magufuli amezungumza na wananchi wa Mji wa Misigiri katika Wilaya ya Iramba ambapo amemuagiza Meneja wa Wakala wa Barabara katika Mkoa wa Singida kuhakikisha mkandarasi anayejenga daraja la Sibiti anarejea kazini mara moja kukamilisha ujenzi wa daraja hilo.

Rais Magufuli amesema serikali yake imejipanga kumlipa fedha mkandarasi huyo na hivyo hakuna sababu ya kuendelea kusimamisha ujenzi huo.
 
Kiukweli nilikuwepo nzega alizungumza vizuri mno namnukuu "sina fedha za kuanzisha mkoa mpya nina fedha za kuboresha huduma za jamii kama barabara, maji,hospital nk"
 
Hapana, ukweli tutasema daima kwenye hili nami namuunga mkono, yupo sawa kabisa japokuwa kwenye suala la kuzuia sauti ya vyama vingine kuviminya ametuangusha sana na atarajie ugaidi kuchipuka.
 
Rais kanena vema, ingekuwa ni enzi zilee za Msoga... Ombi la Kigwangara la Nzega kuwa mkoa, Puge na Bukene kuwa wilaya lingekubalika..... na hivyo kuongeza mzigo tu kwa Serikali.
 
Rais kuongea vyema sana
Mikoa yanini wakati iliopo bado Huduma Mbaya!!
Tabora ipo hoi Leo aongeze mkoa haitapendeza bwana

Hii inaonyesha sio kila ombi Rais wetu atalikubari no
 
Lakini Tabora kubwa jamani! Anyway ana point lakini afikirie hapo baadaye!
 
Rais John Magufuli amewagomea baadhi ya wabunge waliopendekeza Tabora kugawanywa kwa kuanzisha mkoa mpya wa Nzega.

Wabunge hao ni Naibu Waziri wa Afya, Dk Hamisi Kigwangalla ambaye pia ni mbunge wa Nzega Vijijini, Hussein Bashe (Nzega Mjini) na Seif Gulamali wa Manonga.

Akizungumza na wakazi wa mji wa Nzega ambako wabunge hao walitoa ombi hilo, Magufuli alisema hana mpango wa kugawa mkoa wala wilaya kwa kuwa kufanya hivyo ni kuongeza gharama za uendeshaji wa shughuli za Serikali.

Badala yake alisema fedha ambazo zingetumika kuanzisha mikoa na wilaya mpya zitaelekezwa kutekeleza miradi ya maendeleo.

Ni kweli kuongeza mkoa/wilaya kunaongeza gharama lakini pia kunasaidia serikali kuwa karibu na wananchi. Kama population imeongezeka ina mana resources zinatakiwa ziongezeke na zisimamiwe vizuri. Raisi asingekataa mbele ya wananchi badala yake angetafakari kwanza ombi la wabunge. Mshauri wa Raisi ni either anamuogopa au kazi imemshinda haiwezekani mtu anatoa matamko tu bila kushauriwa.
 
Wao wametoa ombi mbele ya wananchi halafu unataka Rais awaite chumbani kuwapa majibu? Hivi hizi akili mnazipata wapi?

Umefahamu vipi kama Rais alikuwa hana majibu ya swali hata kabla ya kuulizwa hilo swali?

Hufahamu kama suala la kugawa mikoa na wilaya limepigiwa kelele sana na kwa muda mrefu ndani ya bunge kwa sababu kufanya hivyo kunaongeza gharama kwa serikali.
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom