Rais jk arejea kutoka nchini ethiopia…!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Rais jk arejea kutoka nchini ethiopia…!!!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Mar 12, 2011.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Mar 12, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  March 11th, 2011

  [​IMG]
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete mchana wa leo, Ijumaa, Machi 11, 2011, amerejea nyumbani kutoka kwenye ziara ya kikazi mjini Addis Ababa, Ethiopia.
  Rais Kikwete aliondoka Jumatano wiki hii kwenda Ethiopia ili kujiunga na marais wenzake wa Afrika ambao wamepewa jukumu ya kutafuta suluhu katika mgogoro wa kisiasa wa nchi ya Afrika Magharibi ya Ivory Coast.
  Mjini Addis Ababa, Rais Kikwete alijiunga na marais kutoka Afrika Kusini, Chad, Mauritania na Burkina Faso kuendelea na jitihada za kutafuta jinsi ya kurejesha amani na demokrasia katika Ivory Coast.
  Kundi hilo la marais wa Afrika lilipewa jukumu hilo na Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Umoja wa Afrika (AU) katika kikao chake cha Januari, mwaka huu, mjini hapo hapo Addis Ababa.
  Mzozo wa Ivory Coast ulilipuka kufuatia matokeo ya raundi ya pili ya Uchaguzi Mkuu wa Rais nchini humo Novemba 28, mwaka jana, 2010.
  Katika matokeo hayo, Tume ya Uchaguzi ya Ivory Coast ilimtangaza aliyepata kuwa Waziri Mkuu wa nchi hiyo, Alassane Quattara kuwa mshindi.
  Lakini siku nne baadaye, Baraza la Katiba ya nchi hiyo lilibatilisha matokeo hayo kwa kufuata matokeo ya kura 600,000 katika majimbo saba ya kaskazini mwa nchi ambako ndiko ngome ya Mheshimiwa Quattara. Badala yake, Baraza hilo lilimtangaza aliyekuwa anatetea kiti chake, Mheshimiwa Laurent Gbagbo kuwa mshindi.
  Mwisho.
  Imetolewa na:
  Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
  Ikulu,
  DAR ES SALAAM.
  11Machi, 2011
   
 2. Chapa Nalo Jr

  Chapa Nalo Jr JF-Expert Member

  #2
  Mar 12, 2011
  Joined: Dec 8, 2010
  Messages: 6,362
  Likes Received: 3,195
  Trophy Points: 280
  Yaani hiyo ndio kazi ya Kurugenzi!, kusema rais karudi au kaenda!, kweli ilianzishwa kwa ajili ya Rweyemamu, nimeamini.
  Idara ya Habari (Maelezo) ifutwe basi, kuna dublication of taasisi au zaidi ya hapo.
   
 3. Hakikwanza

  Hakikwanza JF-Expert Member

  #3
  Mar 12, 2011
  Joined: Dec 11, 2010
  Messages: 3,898
  Likes Received: 307
  Trophy Points: 180
  Hana msaada wowote hapa nchini hivyo angelibaki hukohuko ingekuwa safi.MAANA ASIPOKIWEPO NI AFADHALI KULIKO AKIWEPO
   
 4. EMT

  EMT JF-Expert Member

  #4
  Mar 12, 2011
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 14,464
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  Ethiopia walienda kujadili pia issue ya Libya na kutoa tamko jana. Mbona taarifa haisemi hili??????
   
 5. Rufiji

  Rufiji JF-Expert Member

  #5
  Mar 12, 2011
  Joined: Jun 18, 2006
  Messages: 1,710
  Likes Received: 161
  Trophy Points: 160
  Kwa hiyo nani anayelipia gharama za kurusha hiyo Gulf Stream?
   
 6. Supervisor

  Supervisor JF-Expert Member

  #6
  Mar 12, 2011
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 553
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 45
  Kuna mkutano wa wafanya biashara wadowadogo Canada mwambieni aende...hiyo kazi ya Ivory cost wamepewa ma rais wasio na tija nchini kwao...
   
 7. Dumelambegu

  Dumelambegu JF-Expert Member

  #7
  Mar 12, 2011
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 1,052
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Watu wazima na akili zenu mnatuletea taarifa ya rais ameenda au amerudi!! Upuuzi gani huu!!
   
 8. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #8
  Mar 12, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Tatizo ni hizo pesa zinazotumika kumrusha nje ya nchi na hiyo ndege ya serikali, don't you think all the money spend on his trips from last month to this Month would have helped his people? US every trip of their president is counted as waste of taxpayers money and scruitnized...

  Wewe you call it upuuzi sababu pia unapenda kula hizo pesa za wananchi wasioweza hata kununua Sukari Madukani
   
 9. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #9
  Mar 12, 2011
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,202
  Likes Received: 719
  Trophy Points: 280
  maazimio ya kikao hicho ni ninj.........mbona hawasemi kama walifanikiwa............taarifa ya kipuuzi kweli
   
 10. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #10
  Mar 12, 2011
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,985
  Likes Received: 441
  Trophy Points: 180
  Ameshaenda Loliondo kunywa dawa?
   
 11. Susy

  Susy JF-Expert Member

  #11
  Mar 12, 2011
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 1,450
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Mungi tayari amekwisha enda loliondo!!

  hali ngumu ya uchumi lkn atumia alots of money kwa safari baada ya kufikiria atatukwamuaje katika uchumi huu mgumu.
   
 12. U

  Uswe JF-Expert Member

  #12
  Mar 12, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,201
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  na nani analipa marupurupu yake na officials wanaoambatana nae? isije kuwa PAYE yangu, maana huyu jamaa kichomi sana
   
 13. Gagurito

  Gagurito JF-Expert Member

  #13
  Mar 12, 2011
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 5,610
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  kapiga picha na wasanii gan this tym?
   
 14. Juaangavu

  Juaangavu JF-Expert Member

  #14
  Mar 12, 2011
  Joined: Nov 3, 2009
  Messages: 915
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Ningelikuw na No ya mkuku ningelimkaribisha kwa text hii.

  Karibu mh! Ndani ya nch yetu ya Tz. Watz ulowaacha umewakuta salama salimini, lakini mioyo yao inazidi kunyongonyea kila iitwapo leo. Ugumu wa maisha unazidi kuwakaba koo, ukosefu wa maji unashika kasi, huduma za afya zinazidi kudorora kila sekunde inavyopita, umeme umekuwa kama kuchungulia ndani ya chumba cha mkwe; hali ya chakula inazidi kuweweseka na hii ni kwa sababu ya kuendelea kutegemea kilimo cha mvua japokuwa tuna mito & vijito.
  Kwa upande wa kisiasa, hali ni legelege kweli kweli, ulowaacha kila mtu anajitamkia la kwake hakuna anayeonesha njia walokasimiwa madaraka wanaongea kama wapita njia wasohusika na wasokuwa na madaraka kabisa. Wale wa upande wa pili wanawaelimisha raia na kuwatia moyo, machoni pa hawa wasojua ni kwa nini wapo madarakani wanaonekana kama wahaini.
  Mh karibu tz, watz tunaomba fedha zilizotumika ktk ziara yako zirejeshwe na AU kwa kuwa mgonjwa mwenye upungufu wa damu haruhusiwi kupunguzwa damu ili kumuokoa mgonjwa mwingine mwenye tatizo hilo.
  Watz tunashukuru umerejea salama, tunaomba safari za nje ya nchi ambazo wanaokualika hawazigharimii, tunaomba usikubali hiyo mialiko. Tunafahamu wanakuhitaji sana ama unahitaji sana kuhudhuria huko, waambiye wananchi wangu wananihitaji wakati huu kuliko wakati mwingine wowote ule, na kama kweli mnahitaji shuruti mghatimiye na mtoe cha ziada nitakachorejea acho nymbn kwa ajili ya wananchi wangu. Ninahitajika sana nymbn ili nikae na wananchi wangu tujadiliane ni jinsi gani kama taifa tutavuka ktk kipindi hiki cha ukame, uhaba wa umeme, hitaji la katiba mpya, na kushirikiana na wanasisa wenzangu ambao wametoa rasilimali zao na muda wao ktk kutoa elimu ya uraia mambalo ni jukumu la serikali ninayoingoza.
  Mh mkulu karibu sana tz, na ninakutakia tafakari njema ya ujumbe huu. Karibu sna
   
 15. S

  Salimia JF-Expert Member

  #15
  Mar 12, 2011
  Joined: Feb 14, 2011
  Messages: 665
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Hakikwanza salama mkuu?
  Hivi hapo penye rangi,, unaweza kutufafanulia? Kwamba asipokuwepo huwa kuna afadhalu gani? Huwa tunapata nini watanzania kwa kutokuwepo kwake? Na watanzania wanakosa nini akiwepo? Maana huu ushabiki mwingine ni kama maneno tu yaa kwenye taarab yasiyo na mantiki yoyote.
  Tuelezee labda nasi tutaelewa unachojua wewe.
   
 16. dudus

  dudus JF-Expert Member

  #16
  Mar 12, 2011
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 7,758
  Likes Received: 6,063
  Trophy Points: 280
  Jamani Rais wangu! Hivi hii ilihitaji kweli hadi ifike kwa akina Rweyemamu ndio watoe "TAARIFA KWA UMMA"! Ni jambo la kushangaza kwamba Rais wetu huwa hana utamaduni wa kuitisha "Press Conference" pale airport punde anaporejea safarini kwa ajili ya yeye mwenyewe (nasema YEYE MWENYEWE) kuueleza umma mambo mbali mbali yatokanayo na safari zake mbalimbali. Wenzetu akina Obama, Angela Merkel, Sarkozy, n.k. hufanya hivyo na si vibaya tukaiga yale mazuri. Hii itasaidia sana kuongeza imani ya umma kwa Mkuu wetu wa nchi. Mambo mengine sio siri wala hayana sababu ya kusubiri yachakachuliwe na akina Rweyemamu.
   
 17. taffu69

  taffu69 JF-Expert Member

  #17
  Mar 12, 2011
  Joined: Feb 26, 2007
  Messages: 2,089
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Jumatatu anaanza utalii wa ndani kwa kuzunguka kwenye Wizara!!!
   
 18. Babkey

  Babkey JF-Expert Member

  #18
  Mar 12, 2011
  Joined: Dec 10, 2010
  Messages: 4,256
  Likes Received: 2,079
  Trophy Points: 280
  Naona una mpango wa kumwaibisha zaidi rais wetu. Hujui huwa anasahau hata kilichozungumzwa hadi akapige chabo!
  Mwache ajaribu kuficha baadhi ya madhaifu yake.
   
 19. Kagemro

  Kagemro JF-Expert Member

  #19
  Mar 12, 2011
  Joined: Jan 11, 2010
  Messages: 465
  Likes Received: 50
  Trophy Points: 45

  Karibu Tena.


  1. Tunataka taarifa ya ukweli juu ya mabomu Loliondo ukicheza tu tunaweka hadharani ukweli wote.Kwani tunaujua vizuri.Swala lakuendelea kucheza na akili zetu koma kabisa.
  2. Tunataka traarifa ya fedha zetu zilizotolewa kama Stimulas Package,tena naomba nikueleze wewe Raisi ambaye si halali siku zako zinahesabika,ungekuwa umeapa kwa kutumia Biblia siku ile tungeamuru Mungu akuondoe faster.kwakua ulitumia katiba basi soma vizuri ibara ya nane.
  3. Tunajua kuwa unajua umeiba kura,tafadhali zungumza na Baraza lako la mawaziri waache kuropokaropoka mambo huu ni wakati wa zama zingine mda wenu unaelekea ukingoni naomba mlitambue.inawezekana hatuna njaa,inawezekana hospitali zetu zimejaa madawa na huduma nzuri lakini CCM tumeichoka tunaitaji mabadiliko.
  Kwa haya machache Naomba niseme Karibu.
   
 20. Kagemro

  Kagemro JF-Expert Member

  #20
  Mar 12, 2011
  Joined: Jan 11, 2010
  Messages: 465
  Likes Received: 50
  Trophy Points: 45


  usipate shida number zake si alishasema ni hizi

  0754777777 / 0754777775
   
Loading...