Rais Huyu kashaurika , wa kwetu Je?

Msharika

JF-Expert Member
May 15, 2009
947
69
Obama Atakiwa Aache Kuvuta Sigara

Rais Barack Obama wa MarekaniMonday, March 01, 2010 6:54 AM
Rais Barack Obama wa Marekani ametakiwa aache kuvuta sigara na daktari wake.Rais Obama ametakiwa na daktari wake aache kabisa kuvuta sigara kwaajili ya afya yake mwenyewe.

Obama aliambiwa hivyo baada ya vipimo vya kwanza vya afya yake tangia alipochaguliwa kuwa rais wa Marekani kuonyesha kuwa ana afya njema sana na yupo fiti kulitumikia taifa lake.

Daktari binafsi wa Obama, Jeffery Kuhlman alisema kuwa vipimo vya afya ya Obama vimeonyesha kuwa Obama atakuwa mwenye afya njema kipindi chote cha urais wake.

Dr. Kuhlman alimshauri Obama aendelee na jitihada zake za kujizuia kuvuta sigara ili aiche kabisa tabia ya kuvuta sigara.

Rais Obama mwenye umri wa miaka 48, amekuwa akijitahidi kujizuia kuvuta sigara mbele za watu na amesema kuwa siku hizi huwa havuti sigara mbele ya familia yake.

Enzi zake kabla ya urais, Obama alikuwa mvutaji mkubwa sana wa sigara na kuna wakati Michelle Obama alinukuliwa na jarida moja la Marekani akielezea kukerwa na uvutaji sigara wa Obama.

Rais Obama alimuahidi mkewe kuwa akishinda urais ataacha kabisa kuvuta sigara lakini alikiri kuwa amekuwa akivuta sigara siku moja moja tangia alipoingia ndani ya ikulu ya Marekani.

Mwaka jana rais Obama alisema kuwa amefanikiwa kujizuia kuvuta sigara kwa asilimia 95.
 
Wa kwetu ni sikio la kufa!
mshauri wake ni Shehe Yahya Husein aka Shehe Video, kwahiyo ondoa shaka, kiona mbali anampa ushauri mwanana.
Rais Obama mwenye umri wa miaka 48, amekuwa akijitahidi kujizuia kuvuta sigara mbele za watu na amesema kuwa siku hizi huwa havuti sigara mbele ya familia yake
.
huyu anashauriwa na wataalamu Yakinifu, kwa viwango na vigezo vya aina yake.....ndo maana wanaendelea kwa kasi ya aina yake.
 
Kwani wa kwetu mnataka ashauriwe kitu gani? Ana tatizo lolote?

Tanzania bwana lol!!
 
Jamani, nadhani humu JF kuna mada nyingi zimeshatioka kwa jinsi Mkulu anavyoshauriwa vituvingi na hakubali, mfano mdogo ni safari zake za mara kwa mara ka ajili ya afya yake, Je uoni ili ni tatizo, mwenzake kashauriwa kakubali na kapunguza hata mbele ya familia avuti tena.
Sasa hata kwenye kufanya maamuzi mfano, Richmond ushahidi uko tayari ila hataki kutekeleza, RADA waingereza wamepoteza muda kutafuta ushaidi lakini kusema watu washughulikiwe hayuko tayari.
Ilo sio tatizo?
 
Naona mnamuonea muungwana, kwasababu mimi nadhani anashaurika sana ila inategemea na ushauri huo unatoka wapi; je unadhani kwa haki lilahi kamati yake ya ufundi ikimshauri kuwa asipowapeleka mafisadi lupango atakosa URAIS ataacha kuwasweka LUPANGO wakina EL,RA,AC,Karamagi na Rashid.? You should contract KAMATI yake ya ufundi to do that cosultancy!!
 
- Rais wetu amepimwa mpaka akili kwa maneno yake mwenyewe na yuko fit, sasa huyo Obama ana matatizo ya kuvuta sigara ambayo kwenye paketi imeandikwa warning za kutisha kuhusu uvutaji, kama anavuta anyways then ndio maana ataishia kuwa one term president kama dalili zinavyoonyesha,

- Mtu huwezi kuwa na akili timamu ukavuta sigara, ninasema no way! Tafadhali msimlinganishe Rais wetu, na wavuta tumbaku, sawa Rais wetu ana mapungufu yake kiuongozi lakini ya kuvuta sigara hapana hana!

Respect.


FMEs!
 
Hapa nimetoka kapa kwa kweli,sijaona uwiano wowote wa Obama kushauriwa kuacha sigara(kakubali?) na Rais wetu.sijakuelewa unamaanisha nini kwa kweli maana hujasema Rais wetu kashauriwa nini,hakuna mlingano wowote hapa...Au ndo mambo ya kuongeza Sredi nini?
 
Unafikiri siku zote hizo Obama alikuwa hajui athari za kuvuta sigara?

- Haibadili ukweli kwamba hawezi kufikiri sawa sawa, I mean sigara inakataliwa kila mahali duniani infact huko US hata kwenye majengo ya Federal hairuhusiwi, ina maana huyu Rais huwa inabidi akajifiche huko nje ya White House ili avute hizo tumbaku sasa huyu kweli atafaa vipi kuwa Rais wa Super power, ndio maana polls hazidanganyi!

Respect.


FMEs!
 

Wavuta sigara wanasiasa marekani wapo wengi tu, ila huwa hawavuti hadharani. Hebu angalia hii ya Shwarznegger, ingawa ni ya zamani kidogo















 
Huyu wetu apunguze mizigo
lakini tangu aanze weka ndani wanaomzibia akuna anaethubutu
kumshauri labda kingunge
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…