Rais Hassan Rouhani: Mei Mosi ni siku ya kuwaenzi wafanyakazi na kuthamani mchango wao..

Sinoni

JF-Expert Member
May 16, 2011
6,180
10,651
4bk5da4f72dad46to4_800C450.jpg


Rais Rouhani amesema hayo leo kwa mnasaba wa maadhimisho ya siku ya kimataifa ya wafanyakazi ambapo sambamba na kutoa mkono wa kheri na baraka kwa wafanyakazi wote amesema kuwa, wafanyakazi hawa wanaofanya kazi kwa bidii ni fakhari kwa taifa na serikali ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Aidha Rais Rouhani amezungumzia mazungumzo ya nyuklia na kubainisha kuwa, juhudi za kidiplomasia za Iran zimeondoa kizuizi kikubwa mbele ya taifa hili na kwamba, makubaliano ya nyuklia yaliyofikiwa kati ya Iran na kundi la 5+1 maarufu kama JCPOA yamefungua mlango wa harakati kuelekea upande wa kilele cha mafanikio.

Inafaa kukumbusha hapa kuwa, siku kama ya leo miaka 127 iliyopita na kufuatia maamuzi ya Kongresi ya Kimataifa ya Kazi, siku hii ilitangazwa kuwa siku ya 'Wafanyakazi Duniani, maarufu kwa jina la Mei Mosi.

Katika siku hii hufanyika makongamano katika pembe mbalimbali duniani kwa ajili ya kuwaenzi wafanyakazi na kuthamani mchango wao.
 
Back
Top Bottom