SI KWELI Rais George Washington alikuwa na meno ya mbao

SI KWELI Rais George Washington alikuwa na meno ya mbao

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Wakuu

kuna hizi story hapa kijiweni wanasema kuwa Rais Washington alikuwa na meno ya plastiki.
1781522334268.png
 
Tunachokijua
George Washington alikuwa Rais wa kwanza wa Marekani kati ya mwaka 1789 hadi 1797. Washington anatambulika pia kama baba wa tgaifa hilo.

Madai

Kwa muda sasa kumekuwa na dhana ama nadharia kuwa Rais Washington ana meno ya mbao na siyo meno halisi.

Washington kuwa na tatizo la meno.

Washington alikuwa akisumbuliwa mara kwa mara na maumivu ya meno na kuvimba kwa fizi. Akiwa na umri wa miaka 24, alitoa jino lake la kwanza kwa gharama ya shilingi 5.

Hadi wakati anaapishwa kuwa Rais wa taifa hilo Washington alikuwa na jino halisi moja na yaliyosalia yote yalikuwa bandia.

Je, alikuwa na meno ya mbao?

Licha ya kuwa Rais Washington alikuwa na tatizo la meno na kutumia meno bandia lakini hayakuwa yametengenezwa kwa mbao.

Meno yake yalikuwa yametengezwa kwa mchanganyiko wa meno ya binadamu, meno ya ng’ombe, pembe za tembo na kiboko. Pia yalikuwa na sehemu zilizotengenezwa kwa dhahabu, risasi na chemchemi za metali.

Kwa nini watu wengi walidhani meno hayo ni ya mbao?

Ingawa hakuna anayejua kwa uhakika chanzo cha imani kwamba George Washington alikuwa na meno ya mbao, inaaminika kwamba watu wengi walichanganya mabadiliko ya rangi ya meno yake ya bandia yaliyotengenezwa kwa pembe za wanyama (ivory) na mbao. Hali hiyo huenda ilichangia kuibuka kwa dhana potofu ambayo imeendelea kuaminiwa hadi leo, mamia ya miaka baadaye.
Back
Top Bottom