Rais Donald Trump ni Rais wa awamu moja tu

Rais Donald Trump ni Rais wa awamu moja tu

ila inabidi uangalie wakati Obama anaingia madarakani deni la taifa lilikuwa kiasi gani na wakati anatoka madarakani ameacha deni kiasi gani.
obama ameliacha deni lisilolipika
Kwani hujui aliingia wakati uchumi ukoje? Deni line ndiolo lililotumika kufufua uchumu huo. Halafu ukitaka kujua ni raisi gani aliyeleta deni kubwa sana Marekani angalia chati hii. Kila aliyekata kodi alikuwa akiongeza deni, na sasa subiri uje uone deni la Trump, mzee mwenye uzoefu wa madeni na bankruptcies

1565643878242.png



Halafu angalia jinsi Trump anavyoogeza deni licha kukuta uchumi una hali nzuri
1565644796701.png


 
Trump anakubalika sana na wamerekani wazalendo na hao Ndio huamua matokea. Nchi za magharibi zinarudi kwenye u nationalist na hawa kina trump ni mwanzo tu watachaguliwa sana. Achana na wapiga porojo kina obama wanaongea sana vitendo sifuri
Je, unaijua Marekani? Wamarekani wazalendo ni akina nani? Acha kudandia mambo usiyoyajua kijinga jinga kama hivi unavyofanya. Bila shaka ungeweza kuwatetea na hata kuwaita wazalendo wale makaburu wa Afrika Kusini. Je, hii ni akili kweli?
 
Je unaijua Marekani? Wamarekani wazalendo ni akina nani? Acha kudandia mambo usiyoyajua kijinga jinga kama hivi unavyofanya. Bila shaka ungeweza kuwatetea na hata kuwaita wazalendo wale makaburu wa Afrika Kusini. Je, hii ni akili kweli?
Mbona unakasirika mkuu? Au kwako wewe wale wanaharakati wanaupiga magoti wakiimba wimbo wa Taifa ndio wazalendo?
 
Mbona unakasirika mkuu?.Au kwako wewe wale wanaharakati wanaupiga magoti wakiimba wimbo wa Taifa ndio wazalendo?
Samahani ndugu, nadhani nimepotea njia, nilifikri niko kwenye jukwaa la watu makini. Am out!
 
1.Ubaguzi ni nini?
2.Nipe sera 3,Donald Trump alizozianzisha za kibaguzi.
Chuki za wazi dhidi ya walatino na watu wenye asili ya watu weusi.
Chuku dhidi ya watu wanaotoka nchi za kiislaam
Chuki dhidi ya nchi masikini. Sheet holes countries
 
Chuki za wazi dhidi ya walatino na watu wenye asili ya watu weusi.
Chuku dhidi ya watu wanaotoka nchi za kiislaam
Chuki dhidi ya nchi masikini. Sheet holes countries
Toa mfasno mmoja hapo kwa walatino.
Toa mfano mmoja hapo kwa waislamu.
Aliposema shithole countries alisema ni nchi za Africa au zipi?
 
Nimefuatilia sana matamshi ya Trump kwa makini mno,sijaona huo ubaguzi hasa mnaousema ni upi..Au labda kuna definition mpya ya neno ubaguzi niambiwe.
....kwa sababu labda hujui maana ubaguzi ni nini kwa hiyo hata ukiuona hutautambua.
 
Mkuu hapo kwenye kudorora kwa uchumi ni kama ulijisahau ukachomoa betri coz uchumi wa marekani unakua kwa kasi na umeongeza spidi baada ya "FED" kukata interest rate
 
Sijaona upande ws Democrats atakayemshinda Trump, ishu kubwa inayombeba ni Kuuweka uchumi ukaendelea kuwa imara, na kampeni yake ya kutengenezea bidhaa ndani ya nchi na watu kuzinunua, ishu ambayo angeingia chaka ni Vita dhidi ya Iran au Venezuela ingefanya USA ayumbe kiuchumi.
 
....kwa sababu labda hujui maana ubaguzi ni nini kwa hiyo hata ukiuona hutautambua.
Ndio maana nikasema labda siku hizi wanaharakati mna definition mpya ya neno ubaguzi..Hebu niambie wewe ubaguzi maana yake nini na unipe reference kwa Maneno ya Trump na video.Usiniwekee edited clip za CNN.
 
Ndio maana nikasema labda siku hizi wanaharakati mna definition mpya ya neno ubaguzi..Hebu niambie wewe ubaguzi maana yake nini na unipe reference kwa Maneno ya Trump na video.Usiniwekee edited clip za CNN.
Basi chukua kombe la ushindi iwapo unaamnini CNN ina edit clips hata zile tunazokuwa tunaona live kwenye mikutano ya hadhara anayofanya. Sasa je vipi hizo Twitter feeds zake?
 
Trump anakubalika sana na wamerekani wazalendo na hao Ndio huamua matokea

Nchi za magharibi zinarudi kwenye u nationalist na hawa kina trump ni mwanzo tu watachaguliwa sana

Achana na wapiga porojo kina obama wanaongea sana vitendo sifuri
Nakubaliana na wewe
 
Mkuu na hilo la Ubaguzi ndiuo litampa tena kura., na hakika akirudi atakichafua mbaya hata vita atapigana maana taakuwa hana cha kupoteza tena, kwa sasa anaogopa kuanzisha vita maana atakosa kura.
Umesema ukweli kila mzungu ni mbaguzi ila hawana wa kuwasemea, kwakuwa walimpata Trump mambo yako powa
 
Mkuu hapo kwenye kudorora kwa uchumi ni kama ulijisahau ukachomoa betri coz uchumi wa marekani unakua kwa kasi na umeongeza spidi baada ya "FED" kukata interest rate
 
Sita kati ya saba uliyosema ni kweli lakini, lile la pili siyo sahihi kwani Uchumi wa Marekani haujadoroa labda huko mbeleni. Trump ana bahati kuwa alikuta Obama kaimarisha Uchumi unaanza kung'aa yeye akingia wakati una'gaa na hivyo amejipa sifa zote za kujenga Uchumi. Obama aliitoa nchi kwenye unemployment rate ya 10% mpaka 4.7% kukiwa na improvement ya 5.3%, na Trump ameongeza imrpovement ya 1.0% tu kufikia 3.7% ambayo ilikuwa likely kufikiwa na utawala wowote baada ya Obama kutokana na momentum aliyoacha Obama, lakini Trump na watu wa republican wanatumia maikrofoni kubwa sana kupigia debe namba hizo kama vile ni muujiza wa Trump wakati sivyo.

Hitimisho lako pia siyo sahihi kwa sababu mbili. Kwanza, muundo wa Uchaguzi wa marekani unategemea sana jinsi atakavyowavuta watu weupe wa PA, WI, MI, OH, VA na NC ambao walikuwa hawapigikura siku za nyuma. Anaweza kupata kura kiduchu kama ilivyokuwa mwaka 2016 lakini iwapo atavuta wabaguzi wengine wengi katika majimbo hayo na kushinda hata kwa kura kumikumi tu, basi ataingia tena Ikulu. Hapo hujaweka rungu la Putin.

Sababu ya pili ni kwa Democrats kutokuwa na mgombea mzuri. Katika kundi lote la democrats sasa hivi hawana mgombea mzuri kabisa. VP Biden ana nguvu lakini siyo mtu makini katika maneno yake, na wakati mwingine haonyeshi kujiamini na amekuwa anafanya makosa ya kipuuzipuuzi sana. Seneta Elizabeth Warren ni mzuri sana kwa sera lakini anatoa ahadi nyingi sana za kufikirika kama vile hayuko serious, Seneta Kamala Harris hana sera yoyote ya kuaminika, yuko huku na kule na ni mwepesi wa kukimbilia ubaguzi na pia kutoa ahadi za kufikirika, Seneta Sanders pia hana sera zozote bali anaahidi mambo ya kufikirika tu kama Elizabeth. Seneta Corry Booker, yeye ni mpiga kelele na mlalamikaji tu hana sera yoyote, Meya Pete, ana akili za kuchambua mambo kwa makini lakini pia hajatoa sera zozote za maana. Halafu ile ya yeye kuwa shoga linaweza kuwa tatizo kubwa sana kwa wahafidhina. Seneta Klobacher na wengine wote waliobaki kwenye kinyanganyiro kile wamowamo tu. Binafsi nilikuwa nadhani yule Gavana wa Colorado, na yule Congressman wa zamani wa Maryland ndio walikuwa candidate reasonable sana lakini wameishiwa pumzi mapema mno.
 
Back
Top Bottom