Rais Donald Trump aimwagia fedha Tanzania za kupambana na Ukimwi

ras mkweli

JF-Expert Member
Mar 12, 2012
280
104
Serikali ya Marekani kupitia mpango wa dharura wa Rais wa nchi hiyo wa kukabiliana na Ukimwi (Pepfar), umeidhinisha Dola 526 milioni katika kipindi cha mwaka mmoja ujao kwa ajili ya kukabiliana na VVU na Ukimwi nchini.

Msaada huu utaongeza idadi ya Watanzania wanaopatiwa matibabu ya kufubaza VVU kufikia milioni 1.2.

Pia utaimarisha mapambano dhidi ya VVU kupitia huduma za upimaji, matibabu, kufubaza na kuzuia maambukizi ili hatimaye kufikia lengo la kutokomeza Ukimwi ifikapo mwaka 2030.

Taarifa ya ubalozi wa Marekani nchini imesema fedha hizo zitafadhili miradi inayotekelezwa chini mpango wa utekelezaji wa Pepfar utakaoanza kutekelezwa Oktoba hadi Septemba 2018, na ni ongezeko la asilimia 12.3 ya bajeti ya mwaka jana.

Bajeti iliyotengwa inajumuisha pia utoaji wa huduma na matibabu kwa watoto yatima na walio katika mazingira hatarishi pamoja na kukabiliana na ukatili wa kijinsia.

Pepfar pia itasaidia mpango wa tohara ya hiari kwa wanaume, walengwa wakiwa 890,000.

Mpango huu unaendeleza ubia wa muda mrefu kati ya Marekani na Tanzania katika sekta ya afya ikiwa ni pamoja na muongo mmoja wa ushirikiano uliowezesha kudhibiti kwa mafanikio maambukizi ya VVU.

Kaimu Balozi wa Marekani nchini, Virginia Blaser alisema, “Kwa pamoja tunafanya kazi ili hatimaye kuwa na kizazi kisicho na Ukimwi Tanzania – ambacho hakuna hata mtu mmoja anayeachwa nyuma.”

Chanzo: Mwananchi
 
Kwa macho ya kawaida naona huku vijijini Ukimwi umeshika kasi sana, kibaya zaidi waathirika wapya ni bibi vizee!
Nilipouliza nikaambiwa labda kwasababu ndilo kundi linaouguza watoto na wajukuu zao wagonjwa na hivyo wanapata maambukizi wakati wakihudumia.
Tunawashukuru sana Watu wa Marekani!
 
Ni kweli hata shangazi yangu alifariki kwa ugonjwa huo kwa kumuuguza kijana wake!! Hatukuamini tulivyompeleka hospitali wakasema huyu bibi ana ngoma!!!
 
Kwa masuala ya Kibiti vipi, hawawezi kutia guu? Just thinking maana nayo naona ni hatari kuliko ukimwi.
 
Kwa macho ya kawaida naona huku vijijini Ukimwi umeshika kasi sana, kibaya zaidi waathirika wapya ni bibi vizee!
Nilipouliza nikaambiwa labda kwasababu ndilo kundi linaouguza watoto na wajukuu zao wagonjwa na hivyo wanapata maambukizi wakati wakihudumia.
Tunawashukuru sana Watu wa Marekani!
Kweli kabisa mkuu.
 
Asante USA kwa kujali maisha yetu, ombi zielekezwe ziliko kusudiwa pls.
 
Trump anamkubali sana Magufuli.
Kwa hiyo na Obama alikuwa anamkubali sana Kikwete?

Sema ni sera ya nchi ya Marekani kusaidia nchi masikini kama hii ya Magufuli. Hata raisi angekuwa Membe bado tu msaada huu ungekuja.
 
habari njema.

ukimwi unanishangazaga sana yani china walivyo wengi waathirika ni 320,000 tuu maajabu...

Tanzania waathirika 1,500,000 huu ugonjwa unaubaguzi kwa kweli
Huku watu wanagegedekana sana jombaaa,huku ni too much kwa migegedeko ndio sababu hasa
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom