Rais Colombia aapa kubeba silaha tena

Rais Colombia aapa kubeba silaha tena

Juuchini

JF-Expert Member
Joined
Dec 10, 2018
Posts
1,923
Reaction score
2,739
Rais wa Colombia Gustavo Petro ameapa kuitetea nchi yake dhidi ya kile alichokiita vitisho kutoka kwa Rais wa Marekani Donald Trump.

Kupitia mtandao wa kijamii, Petro, ambae aliwahi kuwa mpiganaji wa msitumi, ameionya Marekani dhidi ya hatua yoyote ya ukiukaji kwa Colombia, inayofanana na ile iliyofanywa Venezuela mwishoni mwa juma.

Hii inafuatia kauli ya mwishoni mwa juma ya Trump kwamba anaweza kuchukua hatua kama ya Venezuala.

1767788456338.png
 
Hahaha halafu kuna wanajeshi 28 wameuawa wakati wa ukamataji wa bwana Maduro ila kuna majinga fulani yanasema amekamatwa kizembe.. kizembe wakati walinzi wake wote anaowaamini wameuawa sasa uzembe upo wapi hapo? Mfano WU A U walinzi wake wote wafyekwe kisha watokomee nae kuna atakae sema amedakwa kizembe?
 
Mbona hii mada umeileta huku jukwaa la kilimo na ufugaji??

Au rais wa Colombia ni mboga mboga?
 
Huyu anaweza akala shaba hapo hapo kwake na biashara ikaisha kwa kuwekwa mrithi kibaraka.
 
Rais wa Colombia Gustavo Petro ameapa kuitetea nchi yake dhidi ya kile alichokiita vitisho kutoka kwa Rais wa Marekani Donald Trump.

Kupitia mtandao wa kijamii, Petro, ambae aliwahi kuwa mpiganaji wa msitumi, ameionya Marekani dhidi ya hatua yoyote ya ukiukaji kwa Colombia, inayofanana na ile iliyofanywa Venezuela mwishoni mwa juma.

Hii inafuatia kauli ya mwishoni mwa juma ya Trump kwamba anaweza kuchukua hatua kama ya Venezuala.

Na yule wa Panama , Manuel Noriega alisemaga hivyo hivyo wakamnyakua, Duh! Uraisi wa hizio Nchi lazima ulinde mslahi ya USA.
 
Back
Top Bottom