Rais asema fedha si tatizo kuhamia Dodoma

Rais asema fedha si tatizo kuhamia Dodoma

Miji mikuu mingi ipo pembezoni mwa bahari...!!

Aseme ajenda ya dodoma imebebwa na nini??
Wewe ebu acha kutudharau kuona AKILI yako na yetu ni sawa...........we unajua bahari inapita mataifa yapi na yapi????Kwa akili yako ndogo UNAJUA BAHARI IMEPITA kila taifa DUNIANI
 
huyu jamaa kweli ni balaa basi kama fedha hipo wapeni wanafunzi wa vyuo pesa za kujikimu.


swissme
Pesa za kuwapa wanafunzi zipo na zilikuwepo na ndio maana wakati wengine wanakosa hizo pesa za wanafunzi wakati huo huo kuna wanafunzi hewa walikuwa wanalipwa. hivyo pesa walizokuwa wanalipwa wanafunzi hewa ndizo watakazopewa wanafunzi wanaopaswa kupewa tatizo lilikuwa ni usimamizi mkubwa kwani watanzania wengi ni watafuna pesa
 
Pesa za kuwapa wanafunzi zipo na zilikuwepo na ndio maana wakati wengine wanakosa hizo pesa za wanafunzi wakati huo huo kuna wanafunzi hewa walikuwa wanalipwa. hivyo pesa walizokuwa wanalipwa wanafunzi hewa ndizo watakazopewa wanafunzi wanaopaswa kupewa tatizo lilikuwa ni usimamizi mkubwa kwani watanzania wengi ni watafuna pesa
when.

swissme
 
kumbe mtu wa misifaz camp!anaamini kila asemacho lazima kitokeee!!,
 
RAIS John Magufuli amesema fedha kwa ajili ya kuhamia makao makuu Dodoma siyo tatizo na kwamba suala la kuhamia huko halina mjadala na wanaosema haliwezekani wanatakiwa kutambua kuwa jambo hilo mbele yake litawezekana.

Alisema jambo hilo mbele yake haliwezi kukwama, kwani michakato ya kuhamishia serikali Dodoma imezungumzwa kwa miaka mingi, hivyo yeye anafanya utekelezaji huo kwa kufikisha michakato hiyo katika tamati.

Akizungumza baada ya kuwasili katika Ofisi Ndogo za Makao Makuu ya CCM zilizopo Mtaa wa Lumumba, Dar es Salaam kwa mara ya kwanza tangu achaguliwe kuwa Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Magufuli alisema haiingii akilini tangu mwaka 1973 jambo hilo linazungumzwa, lakini halitekelezeki.

“Wanasema eti kuhamia Dodoma haiwezekani, hee! Mbele ya Magufuli itawezekana tu. Michakato imetosha… nitahakikisha tunahamia Dodoma,” alisema na kuongeza: “Wapo wanaosema hela (fedha) tutatoa wapi, mbona kipindi cha Bunge huwa tunakaa na hata wakati wa Bunge la Bajeti tunakwenda huko mpaka watendaji… tunakwenda kule na ukisikia waziri amekuja Dar unamwambia kazi hamna.”

Alisema anatambua kuwa kuna wizara zinazotazamana na bahari, hivyo atatangaza zabuni ya kujenga hoteli katika maeneo hayo ili aone nani atakayeendelea kukaa huko.

Aliongeza fedha zitakazopatikana kwa kujenga hoteli hizo atazipeleka Dodoma kwa ajili ya kujenga majengo mengine.

Kuhusu uvumi kuwa majengo ya Ikulu yatauzwa, alisema si kweli kwa kuwa majengo hayo hayawezi kuuzwa, kwani ni ya heshima ila yatabaki kama makumbusho.

Alisema katika kipindi cha utawala wake atahakikisha serikali inahamia Dodoma, kwani hakuna kinachoshindikana ila ilikuwa imeshindikana kwenye akili za watu.

Aliongeza kuwa, hata kwa mambo ya kiusalama hakuna mji unaojengwa pembezoni mwa bahari, ni lazima uwe katikati na wakihamia Dodoma miji ya Iringa, Babati, Singida na maeneo mengine ya jirani itapanuka.

Wakati akitoa hotuba ya shukrani kwa kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti wa CCM Taifa, Dk Magufuli alitangaza kuwa Serikali ya Awamu ya Tano itahamia Dodoma ndani ya miaka yake minne na ushee iliyobaki sasa kabla ya kumaliza muhula wake.

Alirudia suala hilo kwenye sherehe za Mashujaa mjini humo Dodoma, Julai 25; na kuungwa mkono na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa aliyetangaza kuwa yeye atahamia mjini humo mwezi ujao, uamuzi ambao una maana kuwa serikali yote sasa itapaswa kuwa makao makuu hayo ya nchi. Dk Magufuli alizungumzia pia masuala mengine ya serikali yake hadi sasa akisema imefanikisha elimu bure na hilo limejionesha kwa idadi ya watoto walioandikishwa darasa la kwanza kuongezeka maradufu.

Alisema alipoingia madarakani alianza utekelezaji wa ahadi zake kwa wananchi kwa kutoa elimu bure, kwani ilifika mahali watoto wa masikini walikuwa wakidaiwa ada na wengine walishindwa kusoma kwa kukosa ada lakini sasa wengi wanasoma kwa kuwa elimu ni bure.

“Nilipanga hela lazima nizitafute, mimi sina hela mfukoni mwangu ila hela tutazipata kwa mafisadi ndio maana mimi na serikali yangu tunawatumbua ili tupate hela za kusomesha watoto wetu. Nataka kujenga nidhamu ndani ya serikali,” alisema.

Alisema alipoingia alikuta makusanyo ya mapato ni Sh bilioni 850, lakini baada ya kubana mapato yaliongezeka hadi Sh trilioni 1.5, akisema makusanyo hayo yalikuwa yakiliwa na wachache wachache walioko ngazi ya juu.

Aliongeza kuwa spidi yake ya kufanya kazi ni kubwa hivyo hataki kuona mtu anamkwamisha kwa kuwa amepanga kufanya mambo mazuri. Alisema ndio maana wameamua kujenga reli ya kisasa ili kubeba mizigo ya kutosha, kununua ndege tatu na mbili zitaingia mwezi ujao na kwamba serikali imetenga Sh bilioni 100 kwa ajili ya kuboresha viwanja vya ndege vya Iringa, Songea na Musoma.

Alizitaja huduma nyingine ambazo serikali imeamua kuboresha ni umeme ambapo mradi wa Kinyerezi II una megawati 240 na Kinyerezi I utaongezewa megawati 185 na pia Kinyerezi III na IV inakuja ili kuongeza usambazaji wa umeme nchini uwe mkubwa.

Alisema bajeti ya maji mwaka huu imeongezwa na pia kwa Dar es Salaam kuna mradi wa maji unakuja, na pia wamepata mkopo wa dola za Marekani milioni 500 (sh trilioni 1.05) kutoka Serikali ya India.

Kwenye sekta ya afya, alisema wametenga Sh trilioni 1.99 na kwamba wametenga Sh bilioni 200 kwa ajili ya kununulia dawa hospitalini tofauti na mwaka uliopita ambapo ilitengwa Sh bilioni 25.

Habari Leo
Haya sasa, jembe limenena na linatenda. Watalalila njooni.
 
Kuamini kuwa Pesa za kuhamia Dodoma zipo ni kulubali hadaa.
Hakuna pesa ya serikali iliyo ya siri, majuzi tumeona Dr Mpango analia Bungeni kuomba wamuhurumie pale wabunge walipokuwa wanashinikiza fedha hazitoshi lwenye Afya , Elimu, maji na miundo mbinu. Waziri alisema uwezo ni mdogo hivyo mipango mingi itatekelezwa hivyohivyo kidogo kidogo mpaka itakapo kwisha. Sasa hili ambalo halikuwa katika budget fedha anazosema zipo anazitoa wapi? Jee kakopa tena? Au atachukua zile za afya na elimu?
Tabia ya kumshangilia bila kumhoji nchi itaishia kulia tuu. Ni vema katiba ipitiwe upya kile kipengele cha kushtakiwa mtu akiondoka madarakani kitazamwe ili mtu mbishi atakaye haribu tumfunge
 
Nina ndugu yangu anasoma UD hadi leo hajapata pesa za kujikimu field [emoji22][emoji22][emoji22].
Halafu huku anasema pesa zipo.
Tulia dogo safari hii hakuna kukurupuka kumwaga pesa...hatuwezi kurudia makosa...nyie wanafunzi hewa mmetutesa sana
 
Hapo sasa tutakuwa kama ng'ombe, siyo kila analolisema yeye ni sahihi, naye ni mwanadamu ana mapungufu yake, anapokosea akubali kukosolewa arekebishe tupate kitu kizuri zaidi tusipende kuwa " Yes Man" muda wote, hatutaendelea
Mpinge au mkosoe kwa hoja na data sio talalila tu.
 
Hapo sasa tutakuwa kama ng'ombe, siyo kila analolisema yeye ni sahihi, naye ni mwanadamu ana mapungufu yake, anapokosea akubali kukosolewa arekebishe tupate kitu kizuri zaidi tusipende kuwa " Yes Man" muda wote,hatutaendelea
Unajua kukaa mnapigizana kelele kunagharama zake zikiwemo za kupoteza muda bure sasa ya nini hayo yatokee ni lazima mmoja akubali kushindwa ili kumpisha mwenzie afanye anachoweza kukifanya sasa tukisema watu watu waingie kwenye ligi ya kupingana bila kukubali kushindwa ,je ni nini itakuwa tofauti kati yao na yeye?Naona tukubaliane naye tu tumpe muda wa kufanya analoona litafaa.
 
Kilichopo hapa ni kutafuta sifa tu.
Kwamba wote wameshindwa yeye kaweza.
Na wale wanaosema hawezi (akina sisi ) anataka kutuonesha anaweza....na sio vinginevyo.
Period
Wacha weeee...huyu jamaa ana dhamira ya dhati kutatua matatizo ya wanyonge...u can tell, maneno anayosema yanatoka moyoni...now deal with it, boy
 
Waende huko dodoma, watupunguzie msongamano hapa Dar.
Hela zipo au wakakopa hiyo haituhusu.
 
huyu jamaa kweli ni balaa basi kama fedha hipo wapeni wanafunzi wa vyuo pesa za kujikimu.


swissme
Huko umeenda mbali, mkumbushe bei ya Sukari kwa kilo moja ni sh.ngapi kwa sasa, wakati viwanda vipo hapa hapa na malighafi inapatikana hapa hapa?
 
Watu wanachomkosea huyu mheshimiwa ni kumpinga.Huyu anaonekana ligi anaziweza na hashindwi sasa mkitaka kutimiza miradi yenu dawa ni moja tu nayo ni hii;KILA ANALOLIONGEA NA KULIPANGA DAWA NI KUKUBALIANA NAYE TU NA KUMUUNGA MKONO.
Hakuna dawa nyingine
If you cant fight him join him,,, simple ! na kwa sababu anafanya mazuri na kwa dhati kabisa kutoka sakafu ya moyo wake basi tumuunge mkono. tuache ushezi ushenzi wa sijui UKUTA. tunadanganywa na mapebari wa nje ili waendelee kututawala na sisi tunakubali tu. tutaendelea lini. kweli nimeamini maadui wa maendeleo popote pale huwa wanatoka ndani mulemule. they are just from within that community.
 
Back
Top Bottom