Rais anaupiga mwingi, ila kwanini tusifanye Reforms?

Rais anaupiga mwingi, ila kwanini tusifanye Reforms?

888I

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
445
Reaction score
554
NITATUMIA ALIYOYASEMA GWAJIMA PIA..

Kwa takwimu zao wenyewe, Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinasema kimefanikiwa kuwasajili wanachama zaidi ya milioni 10 kote nchini. Hii si idadi ndogo. Hii ni jeshi la maana kweli kweli wameshashinda Uchaguzi kabla ya kupiga kampeni hapa.

Tukigeuka upande wa maendeleo ndiyo balaa madaraja yamejengwa, barabara zimefunguliwa, mikopo ya elimu ya juu imetolewa kwa wingi, madarasa yameongezeka, vituo vya afya vimepanuka, na mapato ya taifa yameimarika.

Ni wazi Rais Samia Suluhu Hassan anafanya kazi. Hakika, mama anaupiga mwingi.

Lakini basi, tukiwa tumefika hapa – kwanini sasa tusifanye reform ya uchaguzi?
Kwa nini tusirekebishe sheria na mfumo wa Tume ya Uchaguzi ili kuonesha dunia na wananchi kuwa:
✅ Tuna ushindi wa haki,
✅ Tuna uwanja wa ushindani ulio sawa,
✅ Tuna imani hata kwa wanaotofautiana nasi.

Tumejenga vituo vya afya, shule, na reli. Kwani tunaogopa Nini ?

Wapo wanaosema Chadema HAWANA hoja wananchi hawawaelewi.
Basi kama ni hivyo, kwa nini tuogope reforms?
Si bora tufungue milango, kila mtu ashindane kwa uwanja sawa, halafu tuwashinde kishujaa kama tulivyozoea?

CCM ina nguvu.
CCM ina mtandao.
CCM ina historia.

Lakini historia ya kweli haijengwi kwa woga wa mabadiliko — inajengwa kwa uthubutu wa kukubali kwamba hata wenye nguvu, wanahitaji kanuni za haki.
 
Ningependa kuona Tanzania inakuwa na democrasia ya nchi kama Ghana. Ningependa kuona Tanzania inaendeleza vipaji na uwajibikaji wa watoto wao kwa kuwapa stadi na elimu nzuri ili Taifa lipate maendeleo ya kweli.

Tunachoogopa nini? Maana kuna mambo hakuna atakayeweza kuyalinda kwa muda mrefu. Mabadiliko yanalazimisha mabadiliko mengine yatokee.

Kwanini tusianze kwa kuyaruhusu kwa utaratibu, badala ya kusubiri yaje kama mafuriko?
 
Hatukuelewi sisi mama mitano tena ndiyo tunachojua
 
Hata kama kumi..haina shida. Mabadiliko yatakuja tu, hata kama hatuyapendi. Kwanini tusiwe sehemu ya mchakato mzima, mzuri wa mabadiliko hayo?

Kuna vitu kwenye haya maisha, hakuna mtu anaweza kuvizuia
Kabisa kipindi Cha masika mafuriko yanakuja tu hata kama hutaki
 
Dunia ni watu,watu wanabadilika kulingana na mazingira,Hii Hali ya Kupenda kulazimisha watu waende kama vipofu si sawa,maana watu wameelimika, mambo ya mabadiliko hayana kuyazuia, mwisho wa siku hatuna wa kumlaumu kila mtu atashangaa!,Ndio Viongozi na wapambe wanakotupeleka,nao watasemavtulilazimishwa kwa kupewa hela,watoa hela nao watasema tulilazimishwa ili mambo yaende, Viongozi watasema tuliaminishwa kwamba, wananchi ndivyo watakavyo! Katiba hii ya Warioba pia ipitiwe upya maana kuna mambo yanakuwa yameaanza kupitwa na wakati.Ifikie mahali tuachane na Uchawa tuwe wakweli ili kuinusuru nchi yetu.Haya yaliyotokea Rwanda,Burundi,Kongo yalianza kama utani matokeo yake wote tunayaona!
 
Kila mmoja aliyepale juu analinda maslahi ndiyo tatizo kubwa
 
Back
Top Bottom