The Father of All
JF-Expert Member
- Feb 26, 2012
- 10,998
- 13,532
View: https://www.youtube.com/watch?v=gU1TYtFaOXM
Japo amesifiwa sana kuwa msikivu, sijui kama ni kweli. Amesifiwa ana kifua, kweli anacho kifua kama cha wengine lakini si kifua cha chuma kama chawa na mashabiki zake wanavyotaka tuamini. Je yeye ni kama jogoo au tetea na anatetea nani na nini tena kwa matusi reja reja?
Leo anaita watu mataahira na wanyama kwanini naye asiwe kama wao maana wanafanana naye isitoshe anaongoza hivyo? Kimsingi, watawala wetu wanatokana na sisi na wanafanana nasi. Kama baadhi yetu ni wanyama, hata hao wanaowaongoza kadhalika. Mama ana matusi kwa uoni wangu.
Sijui wewe unamuonaje na unasemaje? Je kama hao anawatukana kwa kuwaita majina ya kiarabu na kuwalinganisha na wanyama wakiamua kujibu mapigo hata kumlinganisha na chawa wake atasema wanatukana au wanatenda haki? Je uongozi bora kweli unaishiwa hoja na sera hadi kugeuza matusi hoja na sera zake? Tunagombeani wakati kama ni kutaka katiba ni yetu sote jamaninin?
Ana matusi sina mfano, al jununu fununu sijui ndo kajifunzia huko Dubei kwa watu wake. Je rais mama anapoanza kulalamika wakati hata awamu yenyewe hajaimaliza kweli anatufaa huyu al junun funun au mgonjwa wa akili?
Je, nani hao wagonjwa wa akili kati yao na chawa? Je, ni makosa kuanza kumuita al jununu fununu? Wewe unasemaje? Je, kazi ya rais mama ni kuwasemea Wapinzani na wabaya wake? Je wanapomsemea mbona anawatumia ndata?
Baba yenu nyote ningependa kupata utajiri wa mawazo yenu toka kwenye kuhusiana na mama matusi aka mama mipasho aka al junun funun? Hebu nawe tupe fununu bila kuwa al junun