Rais alilidanganya Bunge | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Rais alilidanganya Bunge

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Regia Mtema, Jan 19, 2010.

Thread Status:
Not open for further replies.
 1. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #1
  Jan 19, 2010
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  Wakuu.Heshima mbele.

  Mtakumbuka kuwa Rais amelihutubia Bunge mara kadhaa tangu kuingia kwake madarakani. Katika hotuba zake Bungeni amezungumza mambo mengi na kutoa ahadi na mielekeo kadhaa kuhus Taifa hili.Kati ya ,ambo aliyoahidi na kuahidi kuyatekeleza kabla ya mwaka 2010 ni kuhusu 50/50 representation kati ya Wanawake na Wanaume kwenye vyombo vya maamuzi ikiwemo Bunge.Katika kulitekeleza hilo Chama Cha Mapinduzi(CCM) kilikuwa mstari wa kwanza katika kuhakikisha hili linatekelezeka. Nilikuwa nina imani kubwa na Rais kwamba hili linaenda kutekelezwa.Lakini chakushangaza ahadi hii imeonekana kuwa ni ndoto ya mchana kwani haitaenda kutekelezeka,kama ilivyoelezwa na Makamu Mwenyekiti wa chama hicho Pius Msekwa kama alivyonukuliwa na gazeti la habri leo hapo chini.


  Kufikia 50% ya wabunge wanawake ‘kwayeyuka’9

  Imeandikwa na Anastazia Anyimike;
  Tarehe: 17th January 2010


  MFUMO uliokuwa na lengo la kufikisha asilimia 50 ya wabunge wanawake, ‘umeshindikana’ kutokana na athari za kutekelezwa kwa mfumo huo nchini.

  Akizungumza katika wakati wa kufungua warsha ya siku mbili ya mikakati ya kuongeza idadi ya wagombea wanawake katika Uchaguzi Mkuu 2010, Makamu Mwenyekiti wa CCM, Pius Msekwa alisema ingawa mfumo huo ungefikisha lengo hilo lakini athari zake ni kuwa zaidi ya malengo hayo.

  Kwa mujibu wa Msekwa ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD), CCM wamekubali kuendelea na mfumo wa sasa wa viti maalumu vya wanawake ambao idadi yao katika Bunge na Baraza la Wawakilishi linapatikana kutokana na wingi wa kura za chama katika uchaguzi wa wabunge na wawakilishi.

  Kutokana na hali hiyo, amependekeza vyama vya siasa kuteua wanawake wengi zaidi katika nafasi za kugombea majimboni ili kuongeza idadi ya wabunge bungeni na kwamba mfumo wa viti maalumu ambao utaendelea kuwepo, utasaidia kuongeza idadi yao.

  “CCM ilifanya uchambuzi wa kina wa njia zipatazo tano zinazoweza kutufikisha kwenye lengo lililomo katika azimio la Umoja wa Afrika (AU). Tumeamua kuendelea na mfumo wa sasa ingawa haupendwi sana na kwamba unafaa kwa kuwa ni utaratibu wa muda na sio wa kudumu,”


  Msekwa alitaja njia ambazo zilipendekezwa ili kufikia asilimia 50 kwa 50 bungeni kati ya wanawake na wanaume kuwa ni wa kila chama cha siasa kitakachoshiriki kusimamisha wagombea wawili, wanawake na wanaume, mfumo ambao una athari za kuongeza idadi ya wabunge kutoka 232 wa sasa hadi kufikia 480, idadi ambayo ni kubwa mno ukizingatia uwezo mdogo wa uchumi.

  Alisema kuwa njia hiyo pia inatoa mwanya kwa chama husika kupoteza viti viwili kwa pamoja kutokana na udhaifu wa mgombea mmoja kati yao na pia ungechochea kuwapo mgogoro na mivutano kati ya wabunge na wawakilishi wa majimbo hususani kwa upande wa Zanzibar ambako jimbo moja la uchaguzi lingekuwa na viongozi wanne.

  Msekwa alisema mfumo wa pili ulikuwa kuendelea na majimbo ya uchaguzi yaliyopo sasa na kuanzishwa majimbo mapya ya ziada ambapo kila wilaya ya kiutawala ingekuwa na jimbo la uchaguzi litakalogombewa na wanawake pekee.

  “ Athari za njia hii ni kufanya wilaya ya kiutawala kuwa ni jimbo za ziada la uchaguzi litakalokuwa na mbunge mwanamke, hivyo ingesababisha kupunguzwa kwa idadi ya wilaya za kiutawala kutoka 137 za sasa hadi kufikia 112, jambo ambalo lingeweza kudumaza maendeleo ya nchi hasa wakati huu ambapo kuna maombi ya kuanzishwa wilaya mpya.”


  Alisema njia hiyo pia ingeathiri mamlaka za dola kwa kuingilia uwezo wa Rais wa Jamhuri ya Muungano kuanzisha wilaya mpya pale anapoona inafaa, kwani akifanya hivyo inamaanisha kuongeza majimbo ya uchaguzi wa wabunge na kuwapo hatari ya muingiliano wa kikazi baina ya wabunge wanawake wa wilaya na wabunge wa majimbo ya kawaida hususani kwenye wilaya kubwa zenye majimbo mengi.

  Msekwa alisema mfumo wa tatu uliojadiliwa ni kuanzisha utaratibu wa kura za uwiano (Party list system of proportional), ambao ungetoa nafasi kwa chama kumuombea kura mgombea badala ya kufanya kampeni.

  Alisema njia hiyo ilikuwa na athari za kupunguza hamasa kwa wapiga kura kujitokeza kwa wingi siku ya uchaguzi, kwani hawapati fursa ya kumfahamu mgombea watakotaka kumchagua.

  “ Huu ni mfumo mpya ambao unahitaji muda wa kutosha kuwaelimisha wananchi juu ya faida zake hivyo usingeweza kufanyika kwa ufanisi kabla ya uchaguzi wa 2010.”

  Msekwa alitaja njia ya nne kuwa ni kuendelea na mfumo wa sasa wa viti vya maendeleo vya wanawake kulingana na idadi ya kura ingawa athari zake ni kuendeleza ‘upendeleo’ kwa wanawake kwa kutengewa viti na hauwezi kupatikana kwa asilimia 50 ya wabunge/ wawakilishi wanawake ambayo imekusudiwa.

  Alisema mfumo wa mwisho ulikuwa ni kufuta majimbo yote 232 yaliyopo na kuunda majimbo mapya machache na kila jimbo kuwa na wabunge wawili wanawake na wanaume.

  “ Pia njia hii ina athari za kurudisha nyuma katika maendeleo ya kidemokraisa nchini kwa kufuta majimbo, pia utatoa mwanya kwa chama kupoteza viti vyote viwili na unachochea mazingira ya kuwapo migogoro na mivutano miongoni mwa wabunge hususani kwa Zanzibar.”

  Msekwa alivitaka vyama vya siasa nchini kuteua idadi kubwa ya wagombea wanawake kugombea majimbo ya uchaguzi mkuu ujao ili kutimiza lengo la kuongeza wabunge wengi wanawake.

  Alisema kuwa kuna umuhimu wa kushirikisha wanawake katika vyombo vya maamuzi kutokana na idadi ya wanawake katika jamii, mchango mkubwa wa wanawake katika maendeleo ya jamii na kiuchumi na pia kuimarisha demokrasia. Semina hiyo inaendelea leo ambapo mada mbali mbali zitatolewa na kujadiliwa.


  SOURCE: HABARI LEO JUMAPILI 17 JAN 2010

  Kwa maelezo hayo basi. Rais alidanganya Bunge na Watanzania kwa ujumla. Hivi hii nchi inalekea wapi kama hata Rais amekuwa akitoa ahdi za uongo?
   
 2. B

  Boramaisha JF-Expert Member

  #2
  Jan 19, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 820
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  President Kikwete made very promising speeches when he took over reigns. Some of us were filled with hope.... But as it turned out they were just mere empty words from State House speech papers prepared by his speech writer. If he is at all serious he has time to rectify his mistakes in his second term to be able to retire in honor. Otherwise he will end up like his predecessor Benjamin Mkapa who failed his subjects and failed Mwalimu Nyerere by his dishonesty/disloyalty and is now rarely seen in public!
   
 3. Edson Zephania

  Edson Zephania Verified User

  #3
  Aug 3, 2011
  Joined: Apr 8, 2011
  Messages: 507
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Kazi kweli kweli. Inaonekana uongo ni mtaji wa kisiasa?
   
 4. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #4
  Aug 3, 2011
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 445
  Trophy Points: 180
  CCM kudanganya ni jadi yao.
   
 5. AshaDii

  AshaDii Platinum Member

  #5
  Aug 3, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 16,247
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180
  Huu uzi wa January 2010... Rejina kama upo... Je so far unaonaje ilikua bora au bado unataka angetimiza hio ahadi??
   
 6. Nduka

  Nduka JF-Expert Member

  #6
  Aug 3, 2011
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 8,483
  Likes Received: 765
  Trophy Points: 280
  Hii ndio Tanzania na mbunge naye analalamika rais kalidanganya bunge, lakini akimuuliza waziri mkuu swali anauliza upupu.
   
 7. m

  mzee wa njaa JF-Expert Member

  #7
  Aug 3, 2011
  Joined: Jun 16, 2011
  Messages: 1,368
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mbona tushazoea kudanganywa sio la kwanza hilo.
   
 8. The Analyst

  The Analyst JF-Expert Member

  #8
  Aug 3, 2011
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 464
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 45
  Mh. Regia, JK hupenda kufurahisha watu kwa ahadi pasipo kujua utekelezaji wake utakuwa vipi. Kila mwenye kufuatilia siasa za nchi hii anajua hilo! Hofu yangu sasa ni juu ya hekima za baadhi yenu watetezi wetu wapendwa "CDM". Da' Regia, unadhani idadi ya uwakilishi ikiwa 50 kwa 50 wananchi tutanufaika na lolote endapo baadhi yenu mtaendelea kukosa hekima na kupashana Bungeni hata kwa mambo madogo madogo kama taarifa juu ya nani anakuwa rais 2015 nk.

  Wabunge wa CCM wanapofanya vituko Bungeni wanatetea matumbo yao kwa kuwa tayari tunajua udhaifu wao ni ulaji. Unaonaje nyie mkiamua kuwa makini na aina ya miongozo na taarifa za maana kama zile za uongo wa waziri mkuu na mawaziri na kuachana na miongozo na taarifa zenye lengo la kukejeliana na kurushiana vijembe? Hayo mkiwaachia wa CCM binafsi nitafurahi sana. Napenda kuwaona mnaendelea kukomaa na umakini uleule mlioanza nao.

  Nakutakieni kila la kheri na Mungu awaepushe na mitego ya mafisadi.
   
Thread Status:
Not open for further replies.
Loading...