Rais ajaye awe na sifa zifuatazo

Rais ajaye awe na sifa zifuatazo

simaye

JF-Expert Member
Joined
Nov 5, 2010
Posts
426
Reaction score
214
Tunalo tatizo la uongozi katika nchi yetu ya Tanzania.

Tatizo hili linatokana na viongozi kujipendekeza badala ya kupendekezwa na wananchi.

Leo tunashuhudia ombwe kubwa katika uongozi wa Taifa kwa sababu walioko sasa madarakani waliamua kujipendekeza wenyewe bila ridhaa ya wananchi walio wengi.

Tatizo la nchi yetu ni kuwa wananchi hawana msukumo wa kutaka kupendekeza aina ya mtu wanayetaka awe kiongozi wao.
Sasa kuelekea uchaguzi ujao natoa mapendekezo yafuatayo kuhusu Rais ajaye;

1. Awe ni Mtu ambaye hajaomba mwemyewe kuwa Rais.

2.Atokane na mapendekezo ya Wananchi
3. Awe na Maadili yanayokubalika.

4. Awe na maelezo yasiyo na Mashaka ya nini kinampeleka kutaka kuwa Rais wa Tanzania.

NB Ongeza Sifa nyingine unazoona zinahitajika kuelekea Urais 2015.

Tunahitaji kiongozi asiye na masihara na Taifa hili la sivyo tutaendelea kupata viongozi Walanguzi na Wahujumu uchumi wa Taifa letu.
 
Mkuu ndo umeandika ktk kuoainisha kati ya namba 1 na 4?
 
Ndugu wanajamvi,

Nchi yetu Tanzania mwaka huu 2015 tutakuwa na uchaguzi mkuu wa uongozi wa nchi hii.

Moja ya nafasi nyeti kabisa ni pale tunapotakiwa kumpata kiongozi mkuu/rais wa nchi.

Kwa sasa vyama vyote vya siasa vipo kwenye mchakato wa kuona ni nani ndani ya chama husika atafaa kuteuliwa miongoni mwa wanachama wao kupeperusha bendera ya chama husika ktk kinyang'anyiro hicho cha kumpata rais wa nchi.

Kwa sasa tayari wengine wameenda mbali kwa kuanza kutamka majina ya wanaoonekana kufaa kupewa dhamana ya kuliongoza taifa hili.

Baada ya kutafakari sana, miye naona labda kwa kuwa sasa tunayafahamu masuala/changamoto zinazolikabiri taifa hili ikiwamo ufisadi uliokithiri, hakuna uwajibikaji, rushwa kubwakubwa, wananchi hawafanyi kazi/hawajitumi, hakuna uadilifu kwa viongozi lakini na kwa jamii kwa ujumla wake, wananchi kuchukulia mambo kwa kawaida sana, viongozi waliopewa dhamana na wananchi kuwa waongowaongo, viongozi kutoa ahadi zisizotimilika (hasa wakati wa kampeni) na mengine mengi yanayofanana na hayo.

Kwa hali ilivyo nchini hapa ni muda muafaka sasa kwetu watanzania/wapiga kura kuanza kutafakari ni kiongozi mwenye sifa zipi tunaye muhitaji kuliongoza taifa hili.

Kwa changamoto zinazilikabiri taifa hili, hiki si kipindi cha kumpendekeza ama kuzungumzia mtanzania anayefaa kupewa dhamana ya kuliongoza taifa hili kwa kuangalia mwonekano wake, sura yake, umri wake, anatoka upande gani wa nchi na mambo mengine yanayofanana na hayo.

Hebu tusaidianeni kupata sifa za mtanzania anayefaa kupewa dhamana ya kuliongoza taifa hili hapa chini.

Miye naanza na sifa hizi;
1. Mchapa kazi (hii ije na kumbukumbu za nini aliwahi kulifanyia taifa hili)

2. Mwadilifu
3. Asiwe mpole sana au mkali sana
4.Mwajibikaji (hii iendane na kumbukumbu za utendaji wake, kuwa kama ndani ya utendaji wake aliwahi kuwa kwenye mazingira yaliyokuwa yanamsababishia kuwajibika na hakuwa tayari kuwajibika ama aliwajibika kwa kulazimishwa, huyu hatatufaa)

5. ............
 
  • Thanks
Reactions: Gor
5.Asiependa kupanda ndege hata pasipo stahili
6.Asiependa udokta,uprofesa wa kusanifiwa
 
Awe ni yule aliyechaguliwa na watz bila kushurutishwa.
 
mkweli, muwazi. muadilifu mwajibikaji kwa maana ya mchapakazi,mvumilivu na mstahimilivu, asiwe mwizi mroho wa madfaraka na asiyeye jilimbikizia mali
 
bila kusahau asiye na roho ya kisasi kwa vyovyote vile na awe mtenda haki
 
kama taifa sidhan kama tunahitaji rais kijana eti awe ndio dawa mujarabu ya matatizo yetu. eti mpole, mwenye hekima na huruma. Tanzania leo hii inahitaji Rais mchapakazi, jasiri na mwenye uwezo wa kuchukua maamuzi magumu kwa maslahi ya taifa tena pasipokusubiri kuambiwa na wasaidizi wake "FANYA" bali yeye mwenyewe. tunamhitaji mtu mwenye rekodi hiyo na hakika mtu huyo hatakuwa na kazi ngumu ya kuwaambia watanzania atafanya kwani ndio hurka yake. tunakutakia kila lililojema wewe kiongozi mwenye hurka na sifa hizo.
 
Sifa za rais ajaye:
A) Asiwe CCM.
B)Asiwe CCM
C)Asiwe CCM
D)Asiwe CCM
UKAWA mpango wa Mungu.
 
Ndugu watanzania acheni kupotoshwa maana huu mwaka kuna watu watakufa kwa pressure pale majina yao yatakapo kwatwa, kama alivyo kwisha wahi kusema Mh Kikwete Kuhusu swala la rais ajaye alisema watanzania wasubirie kumpata rais mwenye sifa zote tajwa ktk chama. hizi kelele hakuna mtu yeyote atajibu maana baraza la taifa la usalam wameapa kufanya kazi hii ktk usiri mkubwa sana sana hivyo watanzania someni alama za nyakati magazeti na vyombo vya habari acheni njaa kusema mambo yanayo leta hofu kwa taifa maana Rais ajaye ni siri nzit na atakaye teguwa kitendawili hiko ni Rais wa sasa siku ikifika
 
Kikwete huyu dhaifu ndio atuchagulie dhaifu mwenzie?likwende zake msoga..
 
Ndugu watanzania acheni kupotoshwa maana huu mwaka kuna watu watakufa kwa pressure pale majina yao yatakapo kwatwa, kama alivyo kwisha wahi kusema Mh Kikwete Kuhusu swala la rais ajaye alisema watanzania wasubirie kumpata rais mwenye sifa zote tajwa ktk chama. hizi kelele hakuna mtu yeyote atajibu maana baraza la taifa la usalam wameapa kufanya kazi hii ktk usiri mkubwa sana sana hivyo watanzania someni alama za nyakati magazeti na vyombo vya habari acheni njaa kusema mambo yanayo leta hofu kwa taifa maana Rais ajaye ni siri nzit na atakaye teguwa kitendawili hiko ni Rais wa sasa siku ikifika
"Ndugu zangu nafarijika sana kwa kauli zenu lakini hili suala la urais ni kubwa, tumuachie huyu aliye juu (Mungu), yeye akiamua liwe linakuwa," By Lowassa..... Mtanzania tarehe 9.02.2015
 
Hii show bwana!!!. Kila mtu anakata viuno kwa style yake. Kila mtu anamfagalia mwanaume wake. Sorry..mwanaume anayeona anafaa maana wanawake hatuwasikii..
 
"Ndugu zangu nafarijika sana kwa kauli zenu lakini hili suala la urais ni kubwa, tumuachie huyu aliye juu (Mungu), yeye akiamua liwe linakuwa," By Lowassa ....... Mtanzania tarehe 9.02.2015.....
 
"Ndugu zangu nafarijika sana kwa kauli zenu lakini hili suala la urais ni kubwa, tumuache huyu aliye juu (Mungu), yeye akiamua liwe linakuwa," By Lowassa........ Mtanzania tarehe 9.2.2015
 
"Ndugu zangu nafarijika sana kwa kauli zenu lakini hili suala la urais ni kubwa, tumuache huyu aliye juu (Mungu), yeye akiamua liwe linakuwa," By Lowassa........ Mtanzania tarehe 9.2.2015
Kauli ya unyenyekevu kwa Mungu....... Lowassa for 2015
 
Back
Top Bottom