Raila Odinga Kujiunga Jubilee William Ruto Kujiunga NASA

Commodores

JF-Expert Member
Feb 5, 2018
289
335
Kuelekea uchaguzi mkuu wa Kenya 2022 kuna dalili wazi kama kawaida kwa siasa ya Kenya kutakuwa na mabadiliko ya viongozi wawili Raila Odinga na William Ruto kubadilishana vyama. Jana nyumbani kwake Karen jijini Nairobi William Ruto alifanya mazungumzo na viongozi wa NASA kutoka Magharibi ya Kenya wakiongozwa na Moses Wetangula, katika mazungumzo hayo viongozi hao wamemuhakikishia William Ruto kumuunga mkono kwenye uchaguzi mkuu wa 2022 kama mgombea wa urais wa Kenya.
Baada ya Raila Odinga kufanya mazungumzo na Rais Uhuru Kenyatta hii imeleta taswira mpya za kisiasa nchini Kenya kwani chama ODM kinaonekana imejiondoa kutoka kwenye Muungano wa vyama NASA haswa baada ya kumwondoa Senata Moses Wetangula kuwa kinara wa upinzani katika bunge la senete nafasi yake ilichukuliwa na James Orengo wa ODM.
William Ruto anaonekana kupingwa vikali na wanasiasa wengi kutoka Central Kenya katika mpango wake wa kumrithi Rais Uhuru Kenyatta baada ya kumaliza mhula wake 2022.
 
Kuna wale wild cows wa bongo, sijui watamuunga mkono nani if this becomes true. Watabaki ukiwa
 
Back
Top Bottom