Boniphace Kichonge
JF-Expert Member
- Jul 31, 2017
- 1,605
- 1,957
Kiongozi wa upinzani nchini Kenya, Raila Odinga amesisitiza kuwa ataapishwa, kutwaa madaraka na kuunda baraza lake la mawaziri hata kama ikimlazimu kufanya hivyo akiwa mafichoni.
Kasema akiwa mafichoni sasa kama rais akiwa mafichoni ataapishwa nanani? Au atajiapisha maana sidhani kama jaji mkuu ataenda huko kinyemela na kumwapisha.Atakuwa anahudumu kama rais wa Kenya..!?
Au huku kuapishwa kumekaaje maana Kenya itakuwa na marais wawili.
James Orengo ndio mchora ramaniMusyoka, Wetangula na Orengo hawaungi mkono huu mpango wanasisitiza mazungumzo.. Tayari NASA ina mpasuko na kwa kawaida ya kisaikolojia na kisiasa huu mpango haupo
Orengo anajifanya yuko smart sana ila kwa sasa kule Jubilee Samoe R ndio anaongoza jahazi na huyu anajulikana kwa misimamo na siasa za kimafiaJames Orengo ndio mchora ramani
lkn nyuma ya huo mpango ni kumshinikiza Kenyata
aridhie mazungumzo
Ofcourse Orengo yupo smart.Orengo anajifanya yuko smart sana ila kwa sasa kule Jubilee Samoe R ndio anaongoza jahazi na huyu anajulikana kwa misimamo na siasa za kimafia
Siku ukifahamu kuna wajeda wanamsapoti hapo itakuwaje?Anachotafta atakipata...
Walisema watachukulia ni kosa la uhaini na adhabu yake ni Kunyongwa
Huyu jamaa kumbe naye ni mpumbavu kabisa, rais yuko ikulu, mihimili yote ya nchi inamtambua,arafu yeye anataka ajiepushe ili amtawale nani na kwa ofisi ipi ya umma,?Kiongozi wa upinzani nchini Kenya, Raila Odinga amesisitiza kuwa ataapishwa, kutwaa madaraka na kuunda baraza lake la mawaziri hata kama ikimlazimu kufanya hivyo akiwa mafichoni.
Katika mahojiano maalum na Idhaa ya Kiswahili ya Sauti ya Amerika, Bw. Odinga amefuta uwezekano wa kufanya mazungumzo na rais aliyepo mamlakani Uhuru Kenyatta ili kuweza kupatikana kwa suluhu ya kisiasa kati ya wawili hao.
Bw. Odinga amesema kuapishwa kwake kutafanyika Januari 30 kama ilivyopangwa awali na kila mkenya amealikwa kuhudhuria hafla hiyo na kueleza kuwa huenda ikamlazimu afanye hivyo akiwa mafichoni.
Rais Kenyatta kwa upande wake amekuwa akiuhimiza upinzani wa NASA kuachana na siasa kwani kipindi cha siasa tayari kimekamilika kwa mujibu wa kalenda ya matukio nchini Kenya.
Matamshi ya Bw. Odinga kuwa ataapishwa na kuwa rais wa wananchi yamekuwa yakiibua hisia mbali mbali miongoni mwa wakenya wengi wakijiuliza kule anapoelekea kutekeleza majukumu ya urais wakati ikulu ya Kenya ina mwenyeji ambaye ni Uhuru Kenyatta, Odinga hakubaliani na hilo.
Wachambuzi wa siasa za Kenya wamekuwa wakitofautiana kwa kauli kuwa huenda Odinga na vinara wenzake wanatumia kisingizio cha kuapishwa kama chambo cha kutaka mazungumzo na Bw. Kenyatta na vile vile kujumuishwa katika serikali, lakini Bw. Odinga anasema hilo si kweli hata kidogo.
Chanzo: VOA
Kama Trump, ameapishwa kuna mwehu mwingine atashindwa apishwa!Hivi Mwendawazimu wa Kisiasa nae huwa anaapishwa?