Raia wa uholazi kotini Arusha

jembejembe

JF-Expert Member
Jun 9, 2016
546
1,000
Kutoka Arusha

Mwanamke raia wa Uholanzi,Marion Hasseloh 47) mkazi wa Usa
River,wilaya ya Arumeru anayemiliki kituo cha watoto
yatima,amepandishwa kizimbani katika mahakama ya wilaya iliyopo,
Arumeru akikabiliwa na kosa la kufanya uharibifu wa mali zenye thamani
ya mamilioni ya fedha kinyume cha sheria.

Akisoma mashtaka mbele ya hakimu ,Devota Msofe wa mahakama hiyo
,mwendesha mashtaka wa serikali ,Rose Sule aliieleza mahakama hiyo
kuwa mnamo mwaka elfu mbili na kumi na tatu na 2016 mshitakiwa akiwa
mpangaji wa Silvester Masawe alifanya uharibifu wa mali, ikiwemo
kuvunja lango la kuingilia ,kubomoa ukuta na kuondoka na baadhi ya
mali za mwenye nyumba wake kinyume cha utaratibu.

Pia mshitakiwa a anadaiwa kukiuka mkataba ya upangaji na kufanya
uharibifu mwingine mkubwa bila makubaliano na mwenye nyumba licha ya
mwenye nyumba kuhoji lakini raia huyo anadaiwa kuwa mkorofi na
kutosikiliza chochote hadi mkataba wake ulipomalizika mapema mwaka
huu.

Mshitakiwa huyo ambaye alipanga katika nyumba hiyo kwa lengo la
kuendesha kituo cha watoto yatima alikana mashataka hayo na yupo nje
kwa dhamana ,hadi kesi hiyo ya jinai namba 481 ya mwaka 2016, itakapo
tajwa tena desemba 22 mwaka huu.

Akizungumza nje ya mahakama mlalamikaji katika shauri hilo,Silvester
Masawa alisema kuwa aliingia mkataba wa upangaji na mshtakiwa wa
kipindi cha miaka mitatu kwa makubaliano ya malipo ya shilingi million
1.4 kwa mwezi na kwamba mshtakiwa hakutakiwa kufanya mabadiliko
yoyote katika nyumba hiyo bila makubaliano suala ambayo mshtakiwa
hakulitekeleza.

Pia alisema mshtakiwa huyo alikuwa akiendesha shughuli za kukusanya
watoto wa kike na kuwapatia mafunzo kwa ajili ya kufanya kazi za
ndani ambapo baadaye huwatafutia kazi kwa wazungu wenzake waishio hapa
nchini,jambo ambalo mlalamikaji alisema halikuwa ndani ya makubaliano
Mwisho
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom