RAIA MWEMA: Slaa afufua upya ufisadi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

RAIA MWEMA: Slaa afufua upya ufisadi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Jul 2, 2011.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Jul 2, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Mwandishi Wetu
  29 Jun 2011
  Toleo na 192

  [​IMG]

  • Asema hadanganyiki na kesi za dagaa
  • Wazungu watoa ripoti kwa donors inayotaja ufisadi
  • Wawataja Lowassa na Rostam
  • Rostam aitwa mtengeneza viongozi – kings maker

  WAKATI wafadhili wakikabidhiwa ripoti inayoonyesha bado Tanzania kuna ufisadi, Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa, ameibuka na kusema hatorudi nyuma katika mapambano dhidi ya rushwa kutokana na serikali kuwaogopa wala rushwa na mafisadi wakubwa.

  Akizungumza katika mahojiano maalumu na Raia Mwema, jana, Jumanne, Dk. Slaa amesema wakati wote ambao yeye na wenzake katika Upinzani wakipigania hatua kuchukuliwa dhidi ya mafisadi na wala rushwa wakubwa, serikali imekuwa na kigugumizi katika kuchukua hatua; huku ikitumia mbinu za kuwafunga midomo.
  Akitoa mfano wa kesi mbalimbali zikiwamo za wizi katika akaunti ya madeni ya nje (EPA) ndani ya Benki Kuu ya Tanzania (EPA) kupitia kampuni ya Kagoda Agricultural Limited na kashfa ya rushwa katika ununuzi wa rada ya kijeshi, Dk. Slaa amesema serikali inawalinda wahusika wakuu.

  “Kampuni kama Kagoda wahusika wanajulikana lakini hakuna hatua zinazochukuliwa dhidi ya wahusika. Hii si dalili nzuri maana inaashiria kwamba wakubwa wanahusika ama wanawaogopa wahusika. Hatudanganyiki na hatunyamazishwi, tutaendelea kusema na kutaka hatua zichukuliwe,” anasema na kuendelea;
  “Kashfa ya rada ni aibu kusikia serikali inadai fedha za rada wakati ilikuwa na kigugumizi wakati Uingereza wakichunguza wahusika wa rada na walishindwa kutoa ushirikiano kwa wachunguzi, lakini sasa eti wanasikia kuna fedha ndio wanazitaka. Kwa nini walikataa kushughulikia wahusika kwa sheria zetu za Tanzania na kuachia Waingereza kila kitu?” alihoji Dk. Slaa.

  Alitoa mfano wa kashfa ya Meremeta inayohusiana na kampuni iliyohusishwa na Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ); huku kukiwa na wanasiasa nyuma ya kampuni husika akisema fedha zilizopotea katika kashfa hiyo zingeweza kutumika kusomesha walimu 19,000.

  Dk. Slaa amesema sasa ana muda zaidi wa kupambana kwa kufanya utafiti wa kina na kwamba atahakikisha wananchi wote wanaelimika na kufahamu haki zao. Amesema amekua akifanya ziara vijijini kukutana na wananchi mara kwa mara na kuzungumza nao juu ya mustakabali wao.

  Wazungu wawasilisha ripoti kwa donors
  Wakati huo huo ripoti iliyoandaliwa na waandishi wawili wa Kizungu, Brian Cooksey na Tim Kelsall, yenye jina “The political economy of the investment climate in Tanzania”, imekabidhiwa kwa wafadhili wakuu wa Tanzania.
  Baadhi ya mambo muhimu kuhusu uchumi wa Tanzania yameanishwa katika ripoti hiyo, ambayo Raia Mwema lina nakala yake, ikiwa ni pamoja na mifano hai ya rushwa kubwa kubwa inayogusa wanasiasa.

  Waandishi hao waliandaa ripoti hiyo kwa niaba ya taasisi ya kimataifa ya Africa Power and Politics Programme (APPP) ya Uingereza. Uandaaji wa ripoti hiyo umefadhiliwa na Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Uingereza (DFID) na Shirika la Misaada la Ireland (Irish Aid); licha ya kuwa taasisi hizo zimejipembua kwenye utangulizi wa ripoti hiyo kwamba si lazima mawazo ya waandishi hao yafanane na ya kwao.

  Katika ripoti hiyo, waandishi hao wameonyesha wazi kwamba bado Tanzania inaathiriwa na mabadiliko ya kisiasa na ufisadi unaowahusisha wanasiasa pamoja na kuwa imekuwa ikipokea wawekezaji wengi kutoka nje katika kipindi cha miaka kumi na tano iliyopita.

  Lowassa , Rostam watajwa kwenye ripoti
  Ripoti hiyo imewataja kwa majina wanasiasa ndani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ambao chama hicho kimewataja kuwa chanzo cha kushuka kwa umaarufu wake mbele ya umma kikielezea kuhusishwa kwao na kashfa mbalimbali, baadhi zikiwa zinatajwa hadharani kwa mara ya kwanza.

  Wanamtaja Waziri Mkuu, aliyejiuzulu, Edward Lowassa, wakianzia na wakati akiwa Waziri wa Ardhi na baadaye Waziri wa Maji na Maendeleo ya Mifugo, wakimuelezea kuwa alitumia madaraka kwa maslahi binafsi. Wameorodhesha mifano.

  Ripoti hiyo yenye kurasa 96 imemtaja pia Mbunge wa Igunga (CCM), Rostam Aziz, wakimuelezea kuwa mmoja wa wanasiasa walioonyesha umahiri mkubwa katika kutengeneza viongozi na kupewa jina la ‘king-maker’ akihusishwa kikamilifu katika kampeni za urais wa Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete hata kabla ya kuingia rasmi katika Kamati Kuu ya chama hicho akiwa Mweka Hazina nafasi aliyodumu nayo hadi mwaka 2007.

  Katika ripoti hiyo, Rostam anatajwa kuhusishwa kwake na sakata la Richmond lililomgharibu marafiki zake, Lowassa, Nazir Karamagi na Dk. Ibrahim Msabaha, ambao kwa pamoja walijiuzulu nafasi zao za uwaziri mkuu (Lowassa) na Wizara za Nishati (Karamagi) na Madini na Afrika Mashariki (Dk.Msabaha).

  Ripoti hiyo, ambayo imetolewa Juni 2011, imetolewa katika kipindi ambacho nchi wahisani zimeonyesha kutoridhishwa na hatua zinazochukuliwa dhidi ya watuhumiwa wakuu wa ufisadi pamoja na kuwapo kesi kadhaa za rushwa zilizofikishwa mahakamani na nyingine kuwa katika hatua za upelelezi.

  Tayari Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) imekuwa katika wakati mgumu kukabiliana na changamoto hizo, huku kukiwa na kampeni za kisiasa za kuzima hatua kadhaa zinazofanywa na taasisi hiyo ambayo kwa sasa imepanua matawi yake nchi nzima.

  Vyanzo vya habari mjini Dodoma vimeeleza kwamba watuhumiwa wakuu wa ufisadi wamemwaga mamilioni ya fedha kuendesha kampeni za kuzuia uchunguzi dhidi yao ikiwa ni pamoja na kuwatisha watendaji wa TAKUKURU akiwamo Mkurugenzi wake Mkuu, Dk. Edward Hosea, wakitaka ang’olewe katika nafasi yake.

  “Baada ya kuona kwamba kuna majalada yameanza kukamilika, baadhi ya watuhumiwa wanaendesha kampeni za kutaka Hosea ang’olewe ili kesi hizo zisimame na wao wapate kujipanga upya. Inabidi wabunge wetu wawe macho na watuhumiwa hao ambao wamekwishafikia Dodoma kuendesha kampeni hizo wakishirikiana na wenzao walioko huko,” anaeleza mtendaji mmoja serikalini.
   
 2. Tiba

  Tiba JF-Expert Member

  #2
  Jul 2, 2011
  Joined: Jul 15, 2008
  Messages: 4,511
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 145
  Magamba watakuja sasa hivi na kusema hao walioandika hiyo ripoti ni CHADEMA!!! LOL

  Tiba
   
 3. h

  hans79 JF-Expert Member

  #3
  Jul 2, 2011
  Joined: May 4, 2011
  Messages: 3,802
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 145
  taarifa ya hao wazungu iwekwe JF ili ijadiliwe kwa faida ya wengi,pia la maana sana kuwa na nyaraka husika ili kupata habari kamili.
   
 4. Oxlade-Chamberlain

  Oxlade-Chamberlain JF-Expert Member

  #4
  Jul 2, 2011
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 7,928
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 160
  Kuiweka taarifa ya page 96 simchezo wewe gonga tu hapo link hio usome mwenyewe alafu uendelee kuijadili hapa.
  "The political economy of the investment climate in Tanzania"
   
 5. POSHO MAVYEO

  POSHO MAVYEO JF-Expert Member

  #5
  Jul 2, 2011
  Joined: Jun 28, 2011
  Messages: 377
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Wazungu walikua wanawapa pesa ya maendeleo wanakula wamekaa kimya sasa wanawageuka
  mimi ndipo hapo nawaheshimu wazungu hawana muda na kitu kisicho na mvuto watakutumia kisha kukimbilia upande wa pili kama utapata nguvu.

  wa sasa wameshasoma dira kwamba watanzania wameamuka kuendelea kula na ccm ni sawa na kuzama nao

  kwa heri magamba

  TAIFA KWANZA
   
 6. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #6
  Jul 2, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Wazungu sasa hivi kinachowatisha ni kuingia kwa Wachina na Wahindi kufuatilia Mali Ghafi zetu

  Na Viongozi wetu wanaonyesha Utamu wa Wachina na Wahindi hawajali pesa wanazotupa zinaenda wapi; Matumboni au Mferejini as long as

  They own the mine they don't care where the money go...
   
Loading...