RAI ya SALMA2015 kwetu wana ARUMERU | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

RAI ya SALMA2015 kwetu wana ARUMERU

Discussion in 'Chaguzi Ndogo' started by Eng. Y. Bihagaze, Mar 31, 2012.

 1. Eng. Y. Bihagaze

  Eng. Y. Bihagaze Verified User

  #1
  Mar 31, 2012
  Joined: Sep 8, 2011
  Messages: 1,481
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  Wenzangu MAJI YA CHAI- wazee wa kumiliki viumbe na vyombo vya angani, wajomba zangu KIKATITI wana wa visima na mwaka , wakubwa wa KINGORI wale watu jasiri sana waliopambania ardhi yao ,LEGURUKI wazee wa Kukarabati nyakati, NGARENANYUKI wamiliki wa maji wa karne hii,NGWARANGA wasiookotwa na maneno mboga... , NKORUA kikosi cha kupambana na haramia wa mashambani, MBUGUNI wazee wa Vito nyepesi ila gharama (Zairwaa), SINGISI wenye vijiji vya haki,AKERI watu wasiobahatisha na hali za Milima,KIKWE watu watulivu wa kuaminiwa washikao dini ,SONGORO yenye wazee warefu wenye kuona mbali na karibu, na maeneo mengine ya..USA.. Mji uliopendwa na Benjamin Franklin kabla ya sehemu ya mji huo haijatokomea ardhini 1863..

  Kwa Muda wa wiki Tatu, sehemu kubwa ya mji wetu huu, ARUMERU MASHARIKI umegubikwa ugeni wa makundi ya watu wa aina na rangi tofauti. na Haijawahi kutokea Hivi kwenye Historia ya Mji huu. Hii yote ni kwa sababu ya turufu tuliyoishika mkononi na wageni hawa wanataka tuicheze jumapili ya tarehe moja. si kucheza turufu hii kunakoleta maana ila wapi pa kuicheza. wageni hawa wametuomba, wametubembeleza, wametulazimisha na wengine kutushurutisha tuicheze kwa faida ya kundi lao..

  Ni wazi yako mabaya na mazuri ya ugeni mzito huu.. miongoni mwao ni matusi.. Tumetukanywa, tumechambwa, tumedhalilishwa .. ingawa wao wanasema walikuwa wanatukanana wao kwa wao lakini Tusi kamtukane aliyekutusi sasa tusi unatukana mbele ya asiyekutukana si kutukanywa huko?, akina mama.. mimba zimefanywa katuni kwanye majukwaa na wageni hawa. Tumesikia, tumevumilia na sasa tunahesabu madakika.. wanasema ni kampeni za Kisiasa.. si hivyo hata kidogo, ingelikuwa ni kisiasa ndani ya jimbo letu si wangetuachia wenyewe tufanye tujuacho, kwani watu wetu hawana midomo? kwanini waje kutusemea wao.. ok basi bora wangetusemea lakini si kututusi, nasi ni raia halali wa Jamhuri tunaohitaji kuheshiwa sisi na familia zetu na si kutukanywa!!

  Mbali na Mabaya Tunakiri kuna neema kiasi imetokea, mara tatu au nne vijana wetu wa bodaboda wamejaziwa mafuta kwenye tukutuku zao na kupewa cash ya siku Tsh20,000. kinabibi, babu, na wazee wengi wamepewa viruzuku .. ukipata Tsh20,000 unakunywa pombe za kienyeji karibia mwezi mzima ukitunza bajeti yako..pia kuna watu wamepata nguo mpya za kutokea zenye rangu ya migomba na t-shirt rangi ya ndizi zilizoiva, ambazo ni za kutokea siku za sherehe au kwendea kwenye nyumba za ibaada.

  Mimi nadhani hatukusimuliwa kadhia iliyotupata, Tumeona, tumeshuhudia na tuna kila sababu sasa wana Arumeru ya kufanya,
  kufanya jambo, jambo moja, jambo moja Tu, Sababu ya kufanya jambo Hilo ..TUNAYO, Nguvu ya kufanya ....TUNAYO na Nia ya kufanya Vilevile ..TUNAYO.. TUTAFANYA..Tunataka Dunia Ijue, Viongozi wa Nchi hii wajue, na Raia wazalendo wa Kweli wa nchi hii wajue kwamba Ingawa sisi ni maskini wa kipato, lakini hatuko tayari KUDANGANYWA TENA.. IMETOSHA!!..   
 2. Halisi

  Halisi JF-Expert Member

  #2
  Mar 31, 2012
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 2,810
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  SALMA2015 ni kiboko. Hongera sana kwa kipaji chako cha kuwasilisha ujumbe. Ni kipaji adhimu sana.
   
 3. K

  Keil JF-Expert Member

  #3
  Mar 31, 2012
  Joined: Jul 2, 2007
  Messages: 2,214
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  SALMA2015,

  Nimevutiwa na analysis yako na namna unavyolijua jimbo la Arumeru Mashariki (geographically). Nime-LIKE post yako na ninaongezea kui-LIKE hapa.

  Pia jina SALMA2015 ni ujumbe kwamba kuelekea uchaguzi wa 2015 SALMA anaweza kuwa mgombea, sasa hapo lengo ni Udiiwani au Ubunge? Mimi niko tayari kuwa msaidizi wa Kampeni zako popote utakapogombea, maana unaonekana una uelewa wa kutosha katika kukata issues kwenye majukwaa.

  Akina Mama/Dada hata bila kuwezeshwa wanaweza ... usikimbilie Viti Maalum, kama jimbo kabisa au kwa kuanzia unaweza kuanza na Udiwanii kwenye Kata mojawapo!
   
 4. d

  dada jane JF-Expert Member

  #4
  Mar 31, 2012
  Joined: Dec 8, 2011
  Messages: 566
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Halow kama ni kike kweli umetuwakilisha.
   
 5. I

  ISOPOWER Member

  #5
  Mar 31, 2012
  Joined: Sep 17, 2010
  Messages: 40
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  Jamani huu ujumbe ni muhimu sana. Hapo arumeru mashariki hakuna mtu au watu ambao wanaweza wakaurudufu na kuusambaza kwa wingi kabla ya machweo leo jumamosi 31/12/2012?
   
 6. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #6
  Mar 31, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Wacha kudanganya watu. Huyo umtakae kaahidi nini zaidi ya matusi, hana hata sura ya uongozi, kwa kuwa tu mtoto wa mchungaji kondoo zilizopotea?
   
 7. Losambo

  Losambo JF-Expert Member

  #7
  Mar 31, 2012
  Joined: Nov 8, 2011
  Messages: 2,623
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Una bahati nijatumia simu ningedondosha signature yangu kama ya wale nalog off lakini hii ni ya Lusinde akitema sera.

  Salma2015 ipo vizuri good analysis asiyekuelewa basi tena.
   
 8. MTAZAMO

  MTAZAMO JF-Expert Member

  #8
  Mar 31, 2012
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 12,503
  Likes Received: 5,613
  Trophy Points: 280
  You are Superdupa Genious!
   
 9. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #9
  Mar 31, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,508
  Likes Received: 2,249
  Trophy Points: 280
  Nice one, ila umewasimanga wazee wangu! Wameru wanatupia pamba ile mbaya, so zile nguo za rangi ya mgomba na ndizi mbivu hawavai kwenye nyumba za ibada.
   
 10. u

  ungonella wa ukweli JF-Expert Member

  #10
  Mar 31, 2012
  Joined: Mar 27, 2012
  Messages: 4,227
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hapo ni chama makini tu yaani CHADEMA.PIPOZZZ........!
   
 11. jouneGwalu

  jouneGwalu JF-Expert Member

  #11
  Mar 31, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,680
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 145
  Nimeipenda hii post!

  Usivunjike moyo na hao wageni, bado una nafasi ya kuwaonyesha kuwa huo ni msitu wako na hauwaogopi kama "Jaguar Paw" !!
  Ndoto njema ni ile inayoanzia nyumbani....
   
 12. Facilitator

  Facilitator JF-Expert Member

  #12
  Mar 31, 2012
  Joined: Oct 30, 2010
  Messages: 2,288
  Likes Received: 802
  Trophy Points: 280
  Sijakupata hapo kwenye date. Unamaanisha leo jmosi 31/03/2012 au? manake kwanza 31/12/2012 itakuwa jumatatu.
   
 13. Eng. Y. Bihagaze

  Eng. Y. Bihagaze Verified User

  #13
  Mar 31, 2012
  Joined: Sep 8, 2011
  Messages: 1,481
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  Kesho.. Tumebakiwa Na Dakika.. Tumeahidi kutoa mshtuko.. Kwamba hata Kama kutakuwa Na uchakachuaji .. Haitawezekana.. Tunayo fimbo mkononi.. Tutawachapa..watachapika.. Arumeru si mji wa mabwege wanaoburuzwa Kwa nguvu za shilingi.. Tuliahidi kuzivaa nguo zao.. Tumezivaa.. Tuliahidi kutokataa pesa Yao of which ni Yetu waliyotunyang'anya, Na tumezipokea, kanga zimevaliwa, malori tumeyapanda sana Na radhim matusi tumeyabeba hapanashaka.. Lakini kichapo tutakitoa.. Kesho Nyangumi atapatiwa dozi yake stahili Na Ujinga nchini UTAKOMA.. Kijana wetu, ingaIwa Meru ni sehemu ya nyumbani kwako, Na ingawa Makazi yako ya Kudumu ni Mbezi DSM, sisi hatuna Ubaya Na wewe.. Tutaendelea kukukaribisha Hapa kwetu Kama mtalii.. Tumeishi Na Nyamgumi miaka 50 sasa, amepiga kelele kwamba yeye ni zaidi ya fahari wote wa Baharini.. Kumbe amekuwa akitudanganya maskini sisi, ametunyang'anya hata kile tulichopewa Na Mola kama tunu ya zawadi yetu.. Katuhadaa, katudhalilisha Na kudiriki kututukana wazi wazi.. Tunasema lazima AADHIBIWE.. Kama hutaki tumuadhibu Basi tutakuadhibu na wewe pia..
   
 14. d

  dada jane JF-Expert Member

  #14
  Mar 31, 2012
  Joined: Dec 8, 2011
  Messages: 566
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mama SALMA.2015 kipaji ulichonacho ni kutoka kwa Mungu hongera sana. Nakupenda bure.
   
 15. M

  Mwanyava JF-Expert Member

  #15
  Mar 31, 2012
  Joined: Jul 25, 2011
  Messages: 206
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Inapendeza!!!
  Kama Arumeru yote inamwamko huu basi NYANGUMI atakuwa dagaa kesho!!
  Angalizo wanaweza wakawazidi kete kwa kuchakachukua na keshokutwa NYANGUMI akendelea kuwa Mkubwa zaidi.
   
 16. I

  ISOPOWER Member

  #16
  Apr 1, 2012
  Joined: Sep 17, 2010
  Messages: 40
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  Samahani saana. 31/03/2012
   
 17. Halisi

  Halisi JF-Expert Member

  #17
  Apr 2, 2012
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 2,810
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Hongera sana SALMA2015 sitokusahau. Umeonyesha ukomavu. Nasubiri maneno yako baada ya matokeo. Keep it up.
   
 18. Memo

  Memo JF-Expert Member

  #18
  Apr 2, 2012
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 2,147
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Robisome: BANNED!!!!
   
 19. Eng. Y. Bihagaze

  Eng. Y. Bihagaze Verified User

  #19
  Apr 2, 2012
  Joined: Sep 8, 2011
  Messages: 1,481
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  TUMECHAPA.., HATUJACHAPAAA!!??!!
  Watu eee TUMECHAPAAAAAAaaa! Na kichapo moja Kwa Moja.. Kwani polisi wao ni watu Wa wapi? Ni watanzania vilevile.. Kuwaburuzia wamwage dam hiyo haipo aisee.. Ha ha haaaaa... Aisee ntacheka Mie.. Mnatengeneza kikosi kazi fresh cha kuchakachua Kura halafu kikosi hicho hicho kinavujisha siri CDM.. Mnajaribu kupenyeza Kura mlizojipigia kisha Hao Hao watu Wenu wanavujisha Siri Kwa CDM. Yaani ni ulemavu wa kifikra Wa karne kudhani wote jeshi la wananchi, Polisi, Magereza, watumishi wa serikali kwamba wote ni CCM damdam.. Ni Ukengeufu uliokomaa Na nuksan..
   
 20. MTAZAMO

  MTAZAMO JF-Expert Member

  #20
  Apr 2, 2012
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 12,503
  Likes Received: 5,613
  Trophy Points: 280
  Wamekusikia Salma 2015! Can you explain the meaning of your name please?
   
Loading...