Hii ni RAI kwa chama cha CDM kwa sababu inaniuma kuona LULU inasagwa na kuwa vumbi.
Mimi sio nguli wa siasa lakini ninajua madudu ya kisiasa ninapoyaona.
Viongozi wote wa siasa lazima wawe wavumilivu (THICK SKIN_ED).
Tuko sisi
mburura (nimelipenda hili neno ingawaje sijui maana yake vizuri - bali najua sio la kujivunia) ambao tutawatusi, kuwakejeli, kuwadhalilisha, na kuwadharau kiasi kwamba hata mbwa wako huwezi kumfanyia hivyo. Nyie mnapaswa kutuvumilia (roll with the punches) na kutujibu kwa mantiki (respond objectively).
Kwa nini?
Kwa sababu tunaotupia madongo viongozi pengine ni asilimia moja (1%) ya wananchi. Sasa utawatosa waTanzania wote (99%) kwa ajili ya sisi mburula wachache. Tumesema mengi: Mbowe this - Slaa that- Zitto -who?, Kitila - what? and so on...
RAI
Hii ni rai yangu.
CHADEMA-sasa hivi
hamdemi (hamjikongoji) tena - (you are a force to be reconciled with.
ACT IT!!)
Itisheni Mkutano wa Usuluhishi (Party Reconciliation Meeting)
Katika kipindi kifupi sana (kutegemea na katiba yenu) itisheni mkutano mkuu na kuuita
MKUTANO wa kusuluhisha chama na wanachama wake.
Hapa wanachama wote (wa sasa na waliofukuzwa) wakaribishwe. Huu
sio mkutano wa kutajana nani mkosefu au msaliti
(naomba msilitumie hili neno msaliti tena - it has a religious connotation - or maybe it is just me) bali ni mkutano wa upatanishwaji. Katika mkutano huu, yafuatayo yafanyike:
- Wanachama hai wahamasishwe
- Waliofukuzwa ambao bado wanakipenda chama warudishwe kwenye ngazi stahiki (maybe just plain member) bila ya masharti.
- Wanachama walio na mgogoro na chama ambao watataka wabaki (kundini) waruhusiwe - unconditionally.
- Futeni kesi zote zilizopo mahakamani hivi sasa.
- Chama kitoke na kauli moja kuwa mpo pamoja kupigania UMMA.
Kumbukeni: Hakuna CDM, CCM, TLP, NCCR-Mageuzi, etc.
Kuna:Tanzania tu.