Elections 2010 RAI: kutoka nguvu ya hoja hadi siasa za maji taka

minda

JF-Expert Member
Oct 2, 2009
1,068
65
wakuu, gazeti hili nilipata kulijua zaidi ya miaka 10 iliyopita; likiwa na uadilifu na weledi wa hali ya juu kiasi cha kufanya mmiliki wake kutangazwa kuwa si raia wa nchi hii kisheria.

lakini katika miaka ya hivi karibuni, gazeti hili kwa mtazamo wangu, limekosa dira na limeegemea zaidi kwenye habari za kuchafuana, tuhuma bila uthibitisho na kuandika habari za uchochezi kwa misingi ya udini na ukabila.

mfano mzuri ni gazeti hili kuandika kwenye ishu zake lukuki kuhusu ukabila ndani ya chama fulani cha siasa bila ya uthibitisho; japo chama hicho kilishafafanua kwa ufasaha.

mfano mwingine ni habari za uzushi kuhusu dhehebu fulani hapa tanzania kumuandaa mgombea wa chama fulani ili eti aweze kubalance kura za waislamu na wakristo, bila ya kutoa uthibitisho.

inasikitisha kwamba gazeti hilo lililokuwa likijiuza kwa hoja zake sasa linategemea uchochezi wa kikabila na udini kama mtaji wake; na hivyo kubadili hadhi yake kutoka nguvu ya hoja hadi siasa za maji taka.

hivi mmiliki bado ni yule wa zamani na sasa amelegea kabisa baada ya kutangazwa kuwa persona non grata?

je, kuna kitu kingine cha ziada kilichofanya gazeti hilo libadili na kuandika habari zisizozingatia maadili ya uandishi?
 
Mkuu, mmliki wa kwanza alishajitoa humo. siku hizi linamilikiwa na mafisadi fulani hivi. Hadhi yake ya nguvu ya hoja imebadilika na kuwa zaidi ya siasa za maji taka, nadhani maji taka ni masafi sana kuliko hoja zinazotolewa humo.
 
mkuu, mmliki wa kwanza alishajitoa humo. Siku hizi linamilikiwa na mafisadi fulani hivi. Hadhi yake ya nguvu ya hoja imebadilika na kuwa zaidi ya siasa za maji taka, nadhani maji taka ni masafi sana kuliko hoja zinazotolewa humo.

we dare to talk openly
 
umesahau na lile la kumwandama Spika Sitta, kama issue ya majuzi hapa wanamwandama na ofisi ya ubunge Urambo mashariki!
 
Rai sio gazeti ni waraka wa kikundi fulani cha watu wanaotaka kujisafisha.
 
Aliyekuwa anamiliki gazeti la "Rai" alijitoa sasa anamiliki gazeti la "Raia Mwema". Rai sasa inamilikiwa na Kigogo fisadi mmoja ambaye alikuwa mbuge wa jimbo karibu na mlima Sekenke.
 
rai lilishauzwa mkuu limenunuliwa na mbunge wa kinondoni presumably with mafisadi backing! wale wote wa rai na wamiliki wao wamehamia RAIA MWEMA, ukitaka zile makala za kina ulimwengu, padre karugendo na the great, joseph mihangwa mkuu nunua raia mwema kila j5! nlishaacha nunua rai mda tu, sasa kila j5 nasoma raia mwema tu
 
maripota wenyewe kina Malaria Sugu unafikiri kuna gazeti hapo ni umbea tupu, afadhali mia tano yangu ninunue toilet paper kuliko RAI na Mtanzania na Mwananchi.
 
Hata humu ndani kuna wanaoandikia RAI. Wewe jaribu tu kupitia mada mbalimbali utakuta nyingine ni maji taka vile vile.
 
Mimi nashaanga mwandishi mahiri kama Joseph Mihangwa bado ana makala katika gazeti la Rai!! Kusema kweli magazeti yote ya New Habari Corporation (ukitoa The African kidogo) ni gutter press. It is full of personal vandetta.
 
Rai iliacha siku nyingi kuwa gazeti, hivi sasa rai ni kipeperushi cha mafisadi kichapishwacho na Rostam Aziz.
 
Nashangaa kwa nini mpaka leo.MAELEZO bado haijalifungia gazeti hili kwa uchochezi wa kidini ambao ni hatari sana kwa usalama wa taifa. Wahariri makini na wenye uweledi hawawezi kuruhusu habari kama ile iliyomhusisha Dk Slaa na Kanisa ichapishwe. Ila kuna taarifa kwamba wahariri wa Habari Corporation hupokea maelekezo ya habari za kuandika na vichwa vya habari kutoka kwa mmiliki Rostam Aziz na swahiba wake Lowassa kwa malengo maalum.
 
Mkuchika hawezi kulifungia kwa sababu anapata amri kutoika kwa akina RA -- na anaogopa kupoteza Ubunge.
 
Back
Top Bottom