GE2025 Rahma Mwita wa ACT achukua fomu ya kuwania Ubunge - Kinondoni atoa ahadi ya kuboresha huduma za afya kwa Mama na mtoto

GE2025 Rahma Mwita wa ACT achukua fomu ya kuwania Ubunge - Kinondoni atoa ahadi ya kuboresha huduma za afya kwa Mama na mtoto

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

BigTall

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2022
Posts
654
Reaction score
1,598
Mgombea wa Ubunge kupitia Chama cha ACT Wazalendo katika Jimbo la Kinondoni, Rahma Mwita ameahidi kuwekeza nguvu zake katika kuboresha huduma za kijamii na miundombinu endapo wananchi watampa ridhaa ya kuwaongoza.

Hayo ameyabainisha Agosti 24, 2025 mara baada ya kuchukua fomu katika Ofisi za Halmashauri ya Wilaya ya Kinondoni, mgombea huyo alieleza kuwa ajenda yake kuu ni kusimamia miundombinu ya barabara, kuhakikisha elimu ya bure inakuwa na hadhi kubwa zaidi pamoja na kuboresha huduma za afya kwa Mama na mtoto ili ziwe bora na bure kwa wote.

Aidha, Bi, Rahma alisisitiza kuwa changamoto za mazingira zitatiliwa mkazo, akiahidi kusimamia usafi na uhifadhi wa mazingira ili Kinondoni ibaki kuwa sehemu salama na rafiki kwa maisha ya wakazi wake.

Mchakato wa wagombea kuchukua fomu unaendelea katika wilaya mbalimbali za Jiji la Dar es Salaam, ambapo vyama vya siasa vipo katika hatua za awali za maandalizi kuelekea uchaguzi mkuu.
 
Back
Top Bottom