Raha ya mapenzi kugombana | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Raha ya mapenzi kugombana

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Yona F. Maro, Jan 6, 2009.

 1. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #1
  Jan 6, 2009
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  MOJA ya hulka ya mwanadamu ni kutopenda amani na utulivu uliovuka mipaka. Hulka hii mwanadamu huianza tokea akiwa mtoto ndiyo maana unaweza kuona mtoto anahangaika mgongoni huku akiwa yuko kwenye mebeleko ya mama yake.

  Si kwamba mtoto anahangaika kwa vile ana hofu ya kuanguka kutoka kwenye mgongo wa aliyembebea, la hasha, bali huwa amechoka na amani iliyopitiliza.

  Akiwa mgongoni pale anakuwa yuko salama, ana kinga kamili kutoka kwa amtu aliyembeba, lakini bado hakubali atanyoosha mikono, atatoa miguu na kujirusha kama vile hafurahii kitendo cha kubebwa.

  Mtoto anapokuwa katika mazingira haya sio kwamba hafurahii kubebwa wala si kuwa anatimiza ule msemo usemao "abebwaye hujikaza", hapana, bali hufanya hivyo katika kudhihirisha tu ile hulka ya mwanadamu kuwa huchoshwa hata na amani.

  Ziko hata nchi ambazo huchokonoa hiki na kile na hatimaye kusababisha machafuko wakati kulikuwa na amani ya kutosha na kulikuwa hakuna hoja ya msingi ya kuwepo madai yoyote yale.

  Hata kwenye uwanja wa mapenzi hali haiko tofauti. Ndiyo maana unaweza ukawaona watu wanaachana huku watu wengine wakishangaa kwa vile walikuwa wanawaona wana mapenzi mazito.

  Hali hiyo inatokana na watu hao kuchoshwa na amani, kwa hiyo wanatafuta kila njia ili uwepo mgongano kati yao.

  Bendi maarufu ya muziki wa dansi ya DDC Mlimani Park inayopiga mtindo wa Sikinde iliwahi kutoa wimbo mmoja ambao ulikuwa unazungumza juu ya wanandoa wanapogombana.

  Katika wimbo huo inaelezwa kuwa mwanaume anakuwa mkorofi na anapokosana na mkewe na kurudi kwao anakwenda kutafuta suluhu.

  Sikinde wanaeleza kwamba mwanaume huyo ambaye walimpa jina la "Chuma ulete" akiambiwa aangukie anatoa fedha nyingi kuliko mahari aliyotoa.

  Ni ukweli usiobishika kwamba wako watu wa namna hii ambao wakigombana na wapenzi wao hulazimishwa kuangukia. Wako wanaotoa fedha, nguo, ng'ombe, mbuzi na vinywaji.

  Hawa akina chuma ulete huwezi kuwalaumu hata kidogo kwani ndiyo hulka ya mwanadamu au ndio msingi wa maisha kuwa hakuwezi kuwa na utulivu na amani kupita kiasi.

  Ndiyo maana hata maji kwenye mtungi hubumburika bila hata ya kuguswa na mtu au vyombo kwenye kabati hugongana bila ya kuwepo kwa mkono wa mtu.

  Pamoja na kwamba ni vigumu kuwa na mapenzi yasiyoingiwa na migogoro hata kidogo; vinginevyo labda muwe munadanganyana kama wacheza sinema hivi, ni vizuri kujaribu kuipunguza kwa kadri inavyowezekana.

  Lakini jambo la msingi zaidi inapotokea mgongano kati ya wapenzi ni kuhakikisha kwamba msiwe miamba wote wawili. Kila mmoja asijifanye kifaru na kutaka kuoneshana umwamba na mwenzake, hapo hamutafanikiwa na mapenzi yenu yanaweza kukatika huku munapendana.

  Unapotokea ugomvi baina ya wapenzi si kwamba hawapendani tena au kuna mmoja kapata mwingine au anamchukia mwenzake, la hasha ni hali ileile tu ya kuwepo mikwaruzano ili maisha yawepo.

  Kwa hiyo kinachotakiwa kutokea iwapo mgongano unazuka baina ya wawili wapendanao ni kwa mmoja kuwahi kuomba radhi na mwingine kuikubali hiyo rahi aliyoombwa bila ya kuweka masharti yoyote yale.
   
 2. S

  Stephano Member

  #2
  Jan 7, 2009
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 27
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Du hiyo kali kumbe ndo sababu wadada huwa hamtulii hata mbebewe mbeleko ya chuma?
   
 3. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #3
  Jan 7, 2009
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,918
  Likes Received: 2,068
  Trophy Points: 280
  Leo nimeamka vibaya! Heading ya hii thread ilinitisha kweli! My mind read 'g' as 't':) Only to be disappointed when i read the whole thread!
   
 4. Shishi

  Shishi JF-Expert Member

  #4
  Jan 7, 2009
  Joined: Feb 11, 2008
  Messages: 1,244
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Duh!! naona kweli umeamka vibaya kweli, rudi ukalale basi.....labda baada ya muda kidogo u will rise with a sober mind
   
 5. Kana-Ka-Nsungu

  Kana-Ka-Nsungu JF-Expert Member

  #5
  Jan 7, 2009
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 2,260
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 135
  Hivi ni kweli wanawake wa mkoani Mara wanapenda kupigwa na waume zao na wasipopigwa wanahisi kuwa hawapendwi? Nimewahi kufika Musoma na wakati napiga misele kwenye bars za high street yao ya mukendo, kwa masaa machache tu nilishuhudia incidents kama tatu za wanawake kupewa kichapo na wanaume, nikaanza kuhisi labda kuna ukweli kwenye hili.
   
 6. J

  John W. Mlacha Verified User

  #6
  Apr 20, 2013
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 3,515
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Usipompiga anakuacha
   
 7. Mtumpole

  Mtumpole JF-Expert Member

  #7
  Jan 17, 2018 at 9:43 PM
  Joined: Aug 30, 2010
  Messages: 1,444
  Likes Received: 98
  Trophy Points: 145
  Mganga hajigangi!
   
 8. Mwifwa

  Mwifwa JF-Expert Member

  #8
  Jan 17, 2018 at 9:47 PM
  Joined: Apr 3, 2017
  Messages: 15,114
  Likes Received: 35,899
  Trophy Points: 280
  Kaburi
   
 9. Tusker Bariiiidi

  Tusker Bariiiidi JF-Expert Member

  #9
  Jan 17, 2018 at 10:08 PM
  Joined: Jul 3, 2007
  Messages: 4,757
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  Oooh Dear
   
 10. LAMBOFGOD

  LAMBOFGOD JF-Expert Member

  #10
  Jan 17, 2018 at 10:39 PM
  Joined: Aug 12, 2016
  Messages: 1,039
  Likes Received: 642
  Trophy Points: 280
  bonge la somo mkuu
   
 11. omary urassa

  omary urassa Member

  #11
  Jan 17, 2018 at 10:55 PM
  Joined: Jun 30, 2015
  Messages: 24
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 5
  Yeah ujakosea uko sawa
   
 12. mbalizi1

  mbalizi1 JF-Expert Member

  #12
  Jan 17, 2018 at 11:01 PM
  Joined: Dec 16, 2015
  Messages: 4,804
  Likes Received: 3,482
  Trophy Points: 280
  Wengi wa wanawake wa mkoani Mara wana makovu sana mwilini
   
 13. ISLETS

  ISLETS JF-Expert Member

  #13
  Jan 18, 2018 at 2:57 AM
  Joined: Dec 29, 2012
  Messages: 5,304
  Likes Received: 1,189
  Trophy Points: 280
  mkuu Yona Maro(RIP) hapa alikuwa akiandika hii hread huku akivuta taswita ya anayoyapitia, lakini bahati mbaya ndio hivyo, uhalisia wa maisha ukamshinda, hivyo hata huu uzi umekuwa invalid.
   
 14. y

  young super Senior Member

  #14
  Jan 18, 2018 at 3:03 AM
  Joined: Jan 21, 2013
  Messages: 139
  Likes Received: 129
  Trophy Points: 60
  apumzike salama
   
 15. Rebeca 83

  Rebeca 83 JF-Expert Member

  #15
  Jan 18, 2018 at 3:10 AM
  Joined: Jun 4, 2016
  Messages: 3,275
  Likes Received: 3,634
  Trophy Points: 280
  duh nimeamini humu wana JF wanaandika yanayowasibu kwenye real life,pole msaada haukifika kwako kwa muda muafaka RIP rafiki
   
 16. Jolie Jolie

  Jolie Jolie JF-Expert Member

  #16
  Jan 18, 2018 at 3:26 AM
  Joined: Dec 28, 2017
  Messages: 476
  Likes Received: 635
  Trophy Points: 180
  Roho yake ipumzike kwa amani
   
 17. J

  JWKRMM JF-Expert Member

  #17
  Jan 18, 2018 at 8:29 AM
  Joined: Sep 17, 2017
  Messages: 943
  Likes Received: 515
  Trophy Points: 180
  Lakini pia vurugu ikizidi ni mbaya pia kama amani ikizidi we need a middle path
   
 18. Mtemi mpambalioto

  Mtemi mpambalioto JF-Expert Member

  #18
  Jan 18, 2018 at 9:31 AM
  Joined: Aug 23, 2015
  Messages: 475
  Likes Received: 476
  Trophy Points: 80
  huyo unayemwambia tayar ameshatangulia mbele za haki! kazkwa wikiend!
   
 19. Mtemi mpambalioto

  Mtemi mpambalioto JF-Expert Member

  #19
  Jan 18, 2018 at 9:32 AM
  Joined: Aug 23, 2015
  Messages: 475
  Likes Received: 476
  Trophy Points: 80
  mods wale walio R.I.P nashauri nyuz zao zingekuwa zinalokiwa
   
 20. Horseshoe Arch

  Horseshoe Arch JF-Expert Member

  #20
  Jan 18, 2018 at 9:40 AM
  Joined: Aug 10, 2009
  Messages: 11,231
  Likes Received: 4,951
  Trophy Points: 280
  Kuna somo la kujifunza kuhusu yale tuyaonyayo na yale tuyaishiyo...R.I.P Yona!
   
Loading...