Rage mfungwa anaye tanua bungeni

Rage mfungwa anaye tanua bungeni

Selungo

JF-Expert Member
Joined
Sep 23, 2009
Posts
1,271
Reaction score
403
Ni jambo la kusikitisha kuona kwamba, chama ambacho ndicho serikali yake inaongoza nchi kimekuwa msitari wa mbele kukumbatia wahalifu na wavunja sheria za nchi.

Tukumbuke kwamba Aden Rage alihukumiwa kwenda Gerezani miaka mitatu bila adhabu mbadala kwa kosa la kuonyesha silaha ya moto kwenye uchaguzi wa Igunga.

Jambo la ajabu ni kwamba bado Rage mfungwa (sio kifungo cha nje) ambaye yupo uraiani na huku akikitumikia chama chake Bungeni ambapo ndio mahali pa kutunga sheria huku wenye mamlaka ya kumchukulia hatua wakimuangalia.

Je, huu ndio utawala wa sheria na kutii sheria bila shuruti?
 
Sheria ilitamka kifungo au kulipa faini. Alipigwa faini na akalipa, mbona mnaleta hukumu zenu wenyewe humu.
 
sina uhakika sana na Hukumu hiyo lakini hayo ni mambo ya kawaida sana kwenye nchi hii .
 
Ni jambo la kusikitisha kuona kwamba, chama ambacho ndicho serikali yake inaongoza nchi kimekuwa msitari wa mbele kukumbatia wahalifu na wavunja sheria za nchi.

Tukumbuke kwamba Aden Rage alihukumiwa kwenda Gerezani miaka mitatu bila adhabu mbadala kwa kosa la kuonyesha silaha ya moto kwenye uchaguzi wa Igunga.

Jambo la ajabu ni kwamba bado Rage mfungwa (sio kifungo cha nje) ambaye yupo uraiani na huku akikitumikia chama chake Bungeni ambapo ndio mahali pa kutunga sheria huku wenye mamlaka ya kumchukulia hatua wakimuangalia.

Je, huu ndio utawala wa sheria na kutii sheria bila shuruti?

Your are right, hili tumelizungumzia sana hata huku Israel, kigezo eti alisafishwa na mahakama wakati Rage anashinda kesi kwa rufaa teyari alikwisha toka gela kwa msamaha wa rais, kufungwa pekeyake au kufikwisha mahakamani peke yake inatafisiriwa mtu huyo siyo mwaminifu na hafai kuwa kiongozi, pamoja na record chafu za nyuma za huyu Rage bado CCM wamemwona ni deal

Sasa basi hiki ni kitendo cha aibu kabisa, miongoni mwa aibu za taifa letu la Tanzania ni
1. Aden Rage kuchaguliwa kuwa mbunge
2. Kipande cha ardhi cha Loliondo kukodishiwa au kuuziwa mtoto wa mfarme wa Saudi Arabia
3,.Mkataba tata richmund na dowans
4. Kauli ya juzi ya waziri mkuu kuwa police wapige watu
5.Wafanyabiashara kuwa wabunge nakutumia mwanya huo kukwepa kodi hasa ya ongezeko la samani
na aibu ni nyingi mno siwezi kuzitaja zote
Shame kwa wanyamwezi waliomchagua Rage kuwa mbunge wao wakijua wazi kabisa hafai kuwa kiongozi nafikiri watani zangu hao ubongo wao uko kwenye magoti

Ebaeban
Tel.aviv
 
Mangambaz bana, mtuhumiwa anatanua! Where is the rule of law?
 
Sheria ilitamka kifungo au kulipa faini. Alipigwa faini na akalipa, mbona mnaleta hukumu zenu wenyewe humu.

Usipotoshe umma huyu mtu Rage ambaye siyo mwaminifu alifungwa jela, kesi ilikuwa ni ya wizi , kesi ya jinai hazina faini, alifungwa akatoka kwa msamaha wa rais. Nafikiri alishitakiwa kwa wizi wa mpira ambayo inchi ilipewa na FIFA kama mgao wake wenyewe wakaiuza kesi kama hii huwezi kupigwa faini ukiwa convicted.
 
Mkuu wasaidie wanausalama kwa kumkamata rage na umpeleke gerezani.

Kwa vile wana usalama wamegeuka USALAMA-CCM hawaoni tena! Kwa nini tuwasaidie wakati wanapishana nae kila siku bungeni?

Ila kwa wenye itika ya CHADEMA ni TII SHERIA BILA SHURUTI. Siku yaja nao watalipitia tanuru hili.
 
Sheria ilitamka kifungo au kulipa faini. Alipigwa faini na akalipa, mbona mnaleta hukumu zenu wenyewe humu.

Kiongozi!

Jitahidi kuwa na kumbukumbu kidogo. Faini unayo isema ni ile ya Tume ya Uchaguzi. Ambapo kosa lake liliangukia kwenye adhabu ya Shilingi Laki Moja.

Adhabu tunayo zungumzia ni ile ya kesi ya uchaguzi na sio malalamiko kwenye tume ya uchaguzi. Na kosa lile halikuwa na adhabu mbadala. Upo Kiongozi???
 
kuna sehem hata serikalini ukiwa na record hata ya kufunguliwa case unakua hufai kwa kazi flan hata kama ikijathibitika kwamba wewe huna hatia just to be accused is enough kua hufai sasa nilidhan sehem kama bungen hili lingekua ndio jambo la kwanza kabisa!!!! nyerere alimfukuza kazi IGP wa polisi kwa kosa la kugonga mtu.... hakuangalia nani mwenye makosa ilikua ni issue ya collective responsibility!!!
 
Ni jambo la kusikitisha kuona kwamba, chama ambacho ndicho serikali yake inaongoza nchi kimekuwa msitari wa mbele kukumbatia wahalifu na wavunja sheria za nchi.

Tukumbuke kwamba Aden Rage alihukumiwa kwenda Gerezani miaka mitatu bila adhabu mbadala kwa kosa la kuonyesha silaha ya moto kwenye uchaguzi wa Igunga.

Jambo la ajabu ni kwamba bado Rage mfungwa (sio kifungo cha nje) ambaye yupo uraiani na huku akikitumikia chama chake Bungeni ambapo ndio mahali pa kutunga sheria huku wenye mamlaka ya kumchukulia hatua wakimuangalia.

Je, huu ndio utawala wa sheria na kutii sheria bila shuruti?

Usipotoshe umma huyu mtu Rage ambaye siyo mwaminifu alifungwa jela, kesi ilikuwa ni ya wizi , kesi ya jinai hazina faini, alifungwa akatoka kwa msamaha wa rais. Nafikiri alishitakiwa kwa wizi wa mpira ambayo inchi ilipewa na FIFA kama mgao wake wenyewe wakaiuza kesi kama hii huwezi kupigwa faini ukiwa convicted.
Ndiyo unaamka sasa hii nini, hebu kwanza soma vizuri uzi wa mleta hoja.

Ameongelea suala la kuonyesha silaha yake kwenye uchaguzi wa Igunga, wewe unaleta masuala ya mpira wa miguu na FAT, ndiyo maana wenye hekima walisema ukitaka kumfunga mtanzania weka vitu kwenye maandishi, HAMSOMI KWANZA MKAELEWA!!!
 
Kiongozi!

Jitahidi kuwa na kumbukumbu kidogo. Faini unayo isema ni ile ya Tume ya Uchaguzi. Ambapo kosa lake liliangukia kwenye adhabu ya Shilingi Laki Moja.

Adhabu tunayo zungumzia ni ile ya kesi ya uchaguzi na sio malalamiko kwenye tume ya uchaguzi. Na kosa lile halikuwa na adhabu mbadala. Upo Kiongozi???
Kwani mkuu as far as current thread is concerned alifanya kosa gani zaidi ya lile la kuonyesha silaha wakati wa kampeni?
 
Kumbuka kwamba kulikuwa na mashauri mawili kwa nyakati tofauti kuhusu uchaguzi wa Igunga. Kwanza ni malalamiko kwenye Tume ya Uchaguzi ambapo CHADEMA walilalamikia kuvunjwa kwa kanuni/sheria za uchaguzi likiwepo tukio la huyu jamaa kuonyesha silaha wakati anafanya kampeni jukwaani. Kosa hili aliadhibiwa kulipa shilingi Laki moja kwenye Tume ya Uchaguzi.

Shauri la pili ni pingambizi la ubunge wa Mh. Kafumu. Ambapo pamoja na madai mengine ni pamoja na hili la kuonyesha silaha. Hili ni shauri la mahakamani. Ndilo tunalo lisema, upo Mkuu??
 
Idd Simba kaingiza pesa ya umma kwenye akaunti binafsi, DPP bado anasema hakuna ushahidi!!!!
 
Rage anatafutwa na polisi ili akatumikie kifungo,
ukimuona mahali popote tafadhali toa taarifa kituo cha polisi kilicho karibu nawe!
 
Kiongozi!

Jitahidi kuwa na kumbukumbu kidogo. Faini unayo isema ni ile ya Tume ya Uchaguzi. Ambapo kosa lake liliangukia kwenye adhabu ya Shilingi Laki Moja.

Adhabu tunayo zungumzia ni ile ya kesi ya uchaguzi na sio malalamiko kwenye tume ya uchaguzi. Na kosa lile halikuwa na adhabu mbadala. Upo Kiongozi???

Mkuu hapo kwenye red. Ni kesi ipi?
 
nishindwa kuelewa kwa nini police na wana usalama wanatumika kuuwa upinzani,hawataweza jamani CHADEMA hiki chama ni mpango wa Mungu hakuna wa kukiondoa fikirieni vizuri
 
Kumbuka kwamba kulikuwa na mashauri mawili kwa nyakati tofauti kuhusu uchaguzi wa Igunga. Kwanza ni malalamiko kwenye Tume ya Uchaguzi ambapo CHADEMA walilalamikia kuvunjwa kwa kanuni/sheria za uchaguzi likiwepo tukio la huyu jamaa kuonyesha silaha wakati anafanya kampeni jukwaani. Kosa hili aliadhibiwa kulipa shilingi Laki moja kwenye Tume ya Uchaguzi.

Shauri la pili ni pingambizi la ubunge wa Mh. Kafumu. Ambapo pamoja na madai mengine ni pamoja na hili la kuonyesha silaha. Hili ni shauri la mahakamani. Ndilo tunalo lisema, upo Mkuu??
Ok. Nimekupata Mkuu. Kwahiyo Mahakama Kuu ilitengua ubunge wa Kafumu, lakini haikuishia hapo, pia ilimhukumu Rage ambaye aliunganishwa na mlalamikiwa Kafumu kwenye kaunti fulani, miaka 3 jela (kimya bila faini). Isn't it Sir?
 
Kiongozi!

Jitahidi kuwa na kumbukumbu kidogo. Faini unayo isema ni ile ya Tume ya Uchaguzi. Ambapo kosa lake liliangukia kwenye adhabu ya Shilingi Laki Moja.

Adhabu tunayo zungumzia ni ile ya kesi ya uchaguzi na sio malalamiko kwenye tume ya uchaguzi. Na kosa lile halikuwa na adhabu mbadala. Upo Kiongozi???
Hivi wale wasemaji wa CCM hapa jamvini wako wapi waje kumsafisha mtu wao? Au wako busy Arusha? Njooni huku bwana, mwenzetu anaadhiliwa huku mchana kweupe peee! CC: Chama; Ritz; Tandaleone
 
Back
Top Bottom