Rage azomewa jimboni kwake | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Rage azomewa jimboni kwake

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by sulphadoxine, Dec 22, 2011.

 1. sulphadoxine

  sulphadoxine JF-Expert Member

  #1
  Dec 22, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,264
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  MBUNGE wa Tabora Mjini, Ismail Rage na Diwani wa Kata ya ChemChem, Furaha Ikunji, jana walijikuta kwenye wakati mgumu baada ya kuzomewa na wananchi kwenye mkutano wa hadhara. Hatua hiyo ilikuja baada ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Fatma Mwasa, kuwataka kusalimiana na wafanyabiashara wa soko kuu la mkoa huu.
  Aliyeanza kusalimia wananchi ni Ikunji, ambaye baada ya kutoa salamu rasmi ya ‘Umoja’, wananchi hao walikaa kimya hata aliporudia mara tatu hawakujibu.
  Baada ya kuona wananchi hao hawamjibu, alianza kueleza yake ya moyoni na kusema, hata mkinichukia mimi ni walewale, akimaanisha wafanyabiashara hao hawampendi wanamuona ni msaliti.
  ”Ndugu zangu wafanyabiashara wenzangu hata mimi nina vibanda hapa sokoni, mimi siku zote ninawatetea, sasa nashangazwa na nyinyi kudai kuwa mimi ni walewale mkimaanisha ninashirikiana na wakuu wa masoko na watendaji kuwakandamiza, si kweli,” alisema.
  Alisema yeye ni mtu mzuri kwao kwani alirudi katika nafasi hiyo kwa kuwa ana ubunifu wa miradi na kwamba amekuwa akiwatetea kiasi cha kuchukiwa na watendaji wa Manispaa ya Tabora.
  Kwa upande wake, Rage, baada ya kusalimia “Soko Kuu Tabora Oyee!” wananchi walikaa kimya na hata aliporudia tena mara ya pili, wafanyabiashara hao walikaa kimya.
  Lakini bila kujali ukimya huo, Rage aliendelea kumwaga sera akisema Wanatabora wanapaswa kuondokana na kero ya maji na barabara, akisema maji yatapatikana kwa wingi na barabara za lami zitajengwa, ndipo naye kwa mara nyingine alipozomewa.
  "Ndugu zangu niseme tu kuwa mnakaribia kuingia kwenye raha kwani maji na barabara za kiwango cha lami zitajengwa, kwani niligombea ubunge baada ya kuona maendeleo yanakaribia,” alisema Rage huku akiendelea kuzomewa.
  Wafanyabiashara hao baada ya kuona haeleweki, waliomba kipaza sauti ili watoe kero zao huku wakimwomba mbunge huyo akae kimya kwa kuwa wameteseka vya kutosha pasipo kuwasidia.
  Hatua hiyo, baada ya kuona hali tete hiyo, Mwasa alichukua kipaza sauti huku akimtaka Rage aandae mkutano na wananchi na kuwashirikisha watendaji wa manispaa hiyo.
   
 2. Mkuu wa chuo

  Mkuu wa chuo JF-Expert Member

  #2
  Dec 22, 2011
  Joined: Feb 3, 2011
  Messages: 7,253
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  hao wananchi na wenyewe ni wajinga! Sasa mbona walimchagua! Rage wa magamba kamua hivyo hivyo mpaka wapate akili wasije rudia tena kufanya ujinga wakati mwingine...
   
 3. wizaga

  wizaga Member

  #3
  Dec 22, 2011
  Joined: Nov 27, 2011
  Messages: 70
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mtavuna mlichopanda wana tabora,wenzenu wameishabadirika bado tu......mh
   
 4. k

  kidele Member

  #4
  Dec 22, 2011
  Joined: Aug 16, 2011
  Messages: 37
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  enyi wanyamwezi na wakati mwingine msiwe mnalalamika kana kwamba huyo Rage mlilazimishwa kumchagua?
   
 5. MUSONI

  MUSONI JF-Expert Member

  #5
  Dec 22, 2011
  Joined: Dec 20, 2011
  Messages: 554
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  Mmeanzan kuona kosa la kutotumia haki yenu vema na kuchagua msanii kuwa Mbunge wenu sasa mnaanza kununiana., wakati wa kupiga kura ni kipindi muhimu sana....!! poleni wana N'tobora.
   
 6. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #6
  Dec 22, 2011
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,153
  Likes Received: 2,402
  Trophy Points: 280
  Wana Tabora angalieni asije akawa fourty five(45) si unajua anamiliki mguu wa kuku(9mm)
   
 7. Straddler

  Straddler JF-Expert Member

  #7
  Dec 22, 2011
  Joined: Sep 9, 2009
  Messages: 719
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Hawajalazimishwa...
  .... Ni yale yale ya kuuziwa mbuzi ndani ya gunia.
   
 8. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #8
  Dec 22, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,278
  Likes Received: 19,430
  Trophy Points: 280
  rage waonyeshe mguu wa kuku wote hawa watapiga kimya
   
 9. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #9
  Dec 22, 2011
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  Kwani hawa wanyamwezi hawakujua kuwa walikuwa wanamchagua Al-Shabaab kuwa ndio mbunge wao!!Kama hivyo ndivyo ndio maana mizigo mizito wanapewa wanyamwezi kubeba.
   
 10. yutong

  yutong JF-Expert Member

  #10
  Dec 22, 2011
  Joined: Apr 15, 2011
  Messages: 1,604
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Na bado 4 years to go
   
 11. fredmlay

  fredmlay JF-Expert Member

  #11
  Dec 22, 2011
  Joined: Apr 30, 2008
  Messages: 1,855
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Safi sana wananchi (mahakama kuu)
   
 12. nyabhingi

  nyabhingi JF-Expert Member

  #12
  Dec 22, 2011
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 10,896
  Likes Received: 5,357
  Trophy Points: 280
  wanatabora ni wanafki,wachache ndo makini..
   
 13. t

  tizo1 JF-Expert Member

  #13
  Dec 22, 2011
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 857
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 45
  Jaman Rage alitumainiwa sana.sasa anatusumbua vichwa kuliko maelezo.....tuliamin tumepata kumbe tumepatikana.Kazi yake ni kucheza bao na kunywa kahawa
   
 14. s

  sarawati Senior Member

  #14
  Dec 22, 2011
  Joined: Dec 19, 2011
  Messages: 121
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  mimi naona ndo wamejifunza hivyoooooooooo!!!
   
 15. Daudi Mchambuzi

  Daudi Mchambuzi JF-Expert Member

  #15
  Dec 22, 2011
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 31,782
  Likes Received: 36,776
  Trophy Points: 280
  Hapo sokoni kulikua hakuna nyanya zilizooza??
   
 16. Mbugi

  Mbugi JF-Expert Member

  #16
  Dec 22, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 1,488
  Likes Received: 100
  Trophy Points: 160
  kwani sisi tuliosubutu kuchagua wa cdm _mbeya tumepata nini? zaidi ya maigizo, na misemo ya untivirus na vinega na mbaya zaidi kufundisha wanetu matusi? kwa ujumla wanasiasa wa kibongo wote nomaaaaa na hovyoooo kabisa msidanganye watu kuwa sijui magamba, cdm cuf wema wao ni pale wananjaa.
   
Loading...