Rafu za CCM Arusha sasa zahamia kwenye WDC.............. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Rafu za CCM Arusha sasa zahamia kwenye WDC..............

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Rutashubanyuma, Dec 28, 2010.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Dec 28, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,018
  Likes Received: 417,506
  Trophy Points: 280
  Wajumbe WDC wamsusia diwani wa CHADEMA


  Na Said Njuki, Arusha

  WAJUMBE wa Kamati ya Maendeleo ya Kata (WDC) ya Elerai wamemkataa mwenyekiti wa kamati hiyo, Bw. John Bayo kwa sababu ni diwani kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA). Bw. Bayo ambaye pia ni
  msemaji wa CHADEMA na Mwenyekiti wa Serikali wa Mtaa wa Ngurumo, alikumbwa na mkasa huo mwishoni mwa wiki, baada ya wajumbe hao kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM) kudai hawamtabui.

  Walisema wamechukua hatua hiyo kwa sababu chama chake, CHADEMA, hakiwatambui Rais Jakaya Kikwete, Meya wa Jiji la Arusha, Bw. Gaudance Lyimo wala Naibu meya, Bw. Michael Kivuyo (TLP), hivyo na wao hawawezi kumtambua mwenyekiti huyo.

  Diwani wa Kata ndiye Mwenyekiti wa WDC bila kujali anatoka chama gani, na kwa kata ya Elerai, Bw. Bayo anatoka CHADEMA akiwa na wajumbe wa mitaa wawili tu kutoka chama chake, huku wengine 13 wakitoka CCM, hali inayotishia mustakabali wa mipango ya maendeleo katika kata hiyo na
  zingine nane zenye madiwani kutoka CHADEMA kati ya kata 19
  zinazounda jimbo hilo.

  Habari zilizopatikana na kuthibitishwa na Afisa Mtendaji wa kata hiyo, Bw. Charles Sanai zimeeleza kuwa hali ya hewa ilianza kuchafuka mara baada ya mtendaji huyo kutambulisha wajumbe wa kikao hicho, kisha kusoma agenda za kikao akitaraji kumkaribisha mwenyekiti huyo kufungua kikao, ambapo mmoja wa wajumbe hao alinyanyua mkono na kutoa hoja hiyo ya kutomtambua diwani huyo kama mwenyekiti wa kikao.

  “Mwenyekiti wa kikao ni diwani kutoka CHADEMA, chama ambacho hakikuhudhuria kikao cha kumtangaza mshindi wa kura za urais, ambapo Dkt. Jakaya Kikwete alitangazwa kuwa mshindi na Tume ya Taifa ya Uchaguzi, kuapishwa kwake na pia kususia hotuba yake bungeni. Mbaya zaidi kumkataa Mstahiki Meya wa Jiji la Arusha, Bw. Lyimo na naibu wake Bw. Kivuyo kutoka TLP, vipi leo tuongozwe na mwenyekiti kutoka CHADEMA?â€� alihoji mwenyekiti wa mtaa wa Chuma, Bw. Ramadhani Nyagawa.

  Bw. Nyagawa aliongeza kudai kuwa baada ya uchaguzi sasa taifa linatekeleza Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010/15 hayo maazimio ya kikao atayafikisha katika halmashauri inayoongozwa na meya waliyemkataa au yule waliyemchagua wao, CHADEMA, ambaye ni Bw. Estomi Malla na kueleza kwamba hawako tayari kujadili chochote hadi viongozi wa CHADEMA watakapomtambua Rais Kikwete, Meya wa Jiji la Arusha na Naibu wake.

  Mwenyekiti wa mtaa wa SACON, Bw. Losioki Laizer alieleza kuwa wanaheshimu maamuzi ya wananchi ya kupiga kura na kuchagua viongozi wao, lakini Mwenyekiti wa WDC wa Kata hiyo anayetokana na CHADEMA, ndiye msemaji mkuu wa madiwani wa jimbo hilo na ameshatangaza kwenda mahakamani kupinga meya na naibu wake hivyo wasingeweza kumruhusu aongoze kikao hicho muhimu.

  Kukubali diwani huyu kuendesha kikao hiki ni kuwaunga mkono viongozi ambao bado hawajawatambua viongozi halali akiwemo Rais Kikwete, Meya na Naibu wake, hatutabadili msimamo wetu huu. Ni vizuri wakatambua WDC inaendeshwa kisheria na si kiushabiki, tunahitaji kufuata sheria hizo ikiwa ni pamoja na miradi yote iliyoibuliwa awali inaheshimiwa na si vinginevyo,� alionya Bw. Laizer.

  Hoja hizo ziliungwa mkono na Mwenyekiti wa Mtaa wa Mama Musa, Bw. Yasini Selemani ambaye pia ni Mwenyekiti wa Vijana wa CCM Tawi la Elerai Magharibi alimtaka mtendaji kukubaliana na hoja hizo akidai kuwa diwani huyo hata baada ya kuukwa udiwani alitishia kuwafuta baadhi ya wenyeviti kutoka CCM katika kata yake akiwemo yeye (Yasini), jambo ambalo haliwezi kwani alichaguliwa na wananchi na si kiongozi moja.

  Baada ya muvutano huo uliodumu takribani dakika 20, mtendaji huyo aliwataka wajumbe ambao hawawezi kuendelea na kikao hicho kutoka nje, ndipo wajumbe wote 13 wa CCM walipotoka na kuwaacha wawili wa CHADEMA ambao ni Mwenyekiti wa Mtaa wa Majengo, Bi. Sara Mrema na diwani huyo, hali iliyomlazimu mtendaji huyo kusitisha kikao. Mtendaji huyo alisema kuwa angetoa taarifa sehemu husika kwa mujibu wa sheria zilizopo na kwamba anachosubiri na maelekezo kutoka ngazi za juu.

  Kwa upande wake, Meya wa Jiji la Arusha, Bw. Lyimo alipohojiwa alikiri kupata taarifa hizo na kueleza kuwa ni haki ya wajumbe hao kumsaidia mwenyekiti huyo licha ya kuwa anatoka chama pinzani kwani ni diwani halali na mwenyekiti wa WDC.

  Mkurugenzi Mtendaji wa Jiji la Arusha, Bw. Estomih Chang'ah alikiri kupata taarifa na kueleza kuwa bado hajapata taarifa rasmi, hivyo anasubiri taarifa hiyo ndipo atakapoangalia kanuni za Serikali za Mitaa zinaelekeza nini juu ya tukio hilo.

  [​IMG]


  3 Maoni:

  [​IMG]
  Anonymous said... Kaaazi kwelikweli, vyama au wananchi? kama ni vyama kwanza hatuna haja ya kupiga kura. nadhani haya matukio yataendelea kupunguza idadi ya wapiga kura,uchaguzi ujao. kura haina heshima hata kidogo. Tumieni busara ndogo za kawaida kumaliza tofauti na sio kuzikuza. ugomvi wa baba na mama waachiwe wenyewe. wenzetu wako bize na maendeleo , sisi tuko bize na siasa za ujima!!! inatisha. ndio maana watu wanatoza ushuru hadi saa 6 usiku wakizani maendeleo yanaletwa na kutoza shilingi 1000!!!! fufueni viwanda (General tyre Kilitex nk)jengeni barabara. Acheni ujima.
  December 27, 2010 8:44 PM [​IMG] [​IMG]
  Anonymous said... HAWA VIONGOZI WA CCM NI WAPUMBAVU SANA. NA HAWA WANANCHI WALIOPIGA KURA , CCM IWAHESHIMU. NI UJING KUSUSIA KIKAO CHA MAENDELEO YENU WENYEWE. PUMBAVU SANA HAWA WAJUMBE WA WDC. NYIE MNAONA KULIKUWA NA UCHAGUZI WA MEYA NA NAIBU???MNASALI WAPI NYIE? HAMWOGOPI HATA MWENYEZI MUNGU???
  December 28, 2010 2:08 AM [​IMG] [​IMG]
  Anonymous said... Safi kabisa CCM. dawa ya moto ni moto akochomae mchome. Sasa Chadema mnalalmika nini; au mkuki nikwa nguruwe tu, kwa binadamu mchungu?
  Mwamdeka

  December 28, 2010 2:39 AM
   
 2. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #2
  Dec 28, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,018
  Likes Received: 417,506
  Trophy Points: 280
  Kama wajumbe wa CCM kwenye WDC hii hawataki kufanyakazi na Mheshimiwa Diwani aliyechaguliwa na wananchi si ni wao wajiuzulu? Hakuna sheria inayowapa ubavu wa kudharau taratibu za uendeshaji wa vikao vya WDC.......................
   
 3. m

  mageuzi1992 JF-Expert Member

  #3
  Dec 28, 2010
  Joined: Apr 9, 2010
  Messages: 2,512
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Hawa wajumbe wa WDC wamelaaniwa wote na laana itaanza kuwatafuna hivi karibuni ngoja malaika wa Bwana atawatembezea viboko!
   
 4. Ngalikihinja

  Ngalikihinja JF-Expert Member

  #4
  Dec 28, 2010
  Joined: Sep 1, 2009
  Messages: 16,404
  Likes Received: 3,734
  Trophy Points: 280
  CDM haitambui matokeo yaliyotoa urais kwa JK kwa sababu yamechakachuliwa...................... Na huyo Meya hatambuliki kwa vile amechaguliwa nakikao ambacho si halali........wajumbe wa kikao hicho hawakufika theruthi mbili.......na vile vile kuna mpiga kura mmoja ni wa kutoka Tanga hakutakiwa kupiga kura Arusha ............sasa wao wanasababu gani ya kutomtambua huyo.......???
   
 5. TUKUTUKU

  TUKUTUKU JF-Expert Member

  #5
  Dec 28, 2010
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 11,852
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Mh!huu ni ujinga wa karne!!!
   
 6. Ngalikihinja

  Ngalikihinja JF-Expert Member

  #6
  Dec 28, 2010
  Joined: Sep 1, 2009
  Messages: 16,404
  Likes Received: 3,734
  Trophy Points: 280

  Aliyeandika komment hii lazima atakuwa mwenzie na Mahamoud au MS ................ maana inashauri JINO kwa JINO
   
 7. m

  mageuzi1992 JF-Expert Member

  #7
  Dec 28, 2010
  Joined: Apr 9, 2010
  Messages: 2,512
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Asante kuchangia wadau
   
 8. S

  Subira Senior Member

  #8
  Dec 28, 2010
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 162
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  sasa kuna haja ya kutoa tusi hapo kweli " hawa viongozi wa ccm pumbavu sana'kwani ukitoa maoniyako bila kutusi utakuwa ni mjanja zaidi? toa maoni bila kutusi tusi,
   
 9. m

  mageuzi1992 JF-Expert Member

  #9
  Dec 28, 2010
  Joined: Apr 9, 2010
  Messages: 2,512
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Wamechanganyikiwa kabisa hawa....
   
 10. Mabel

  Mabel JF-Expert Member

  #10
  Dec 28, 2010
  Joined: Sep 1, 2010
  Messages: 1,018
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  CCM naona wanakoelekea sio chama cha siasa tena, itabidi tuwatafutie jina lingine.
   
 11. O

  Oldarasu Member

  #11
  Dec 28, 2010
  Joined: Dec 22, 2010
  Messages: 45
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Katika hili, kwanza niseme tutoe hoja ama ushauri wetu bila matusi. Matusi ni dalili kamili ya kushindwa kutoa hoja. Waungwana hushindana kwa hoja wapumbavu kwa matusi. Sasa mimi ninapenda kuwakumbusha madiwani wote kuwa hawajachaguliwa na wananchi kwa ajili ya maslahi yao binafsi. Wakumbuke kwamba muda wanaoupoteza katika malumbano ya kisiasa ni kurudisha maendeleo nyuma na matokeo yake ni wananchi ndio wataumia. Pili, wanaogoma kuketi katika kikao watambue kwamba hawawagomei watu wa CHADEMA bali wananchi na adhabu yao itakuja 2015. Wasifikiri ni mbali sana. Tatu, madiwani wa CCM hamna haja ya kuleta migomo itakayochelewesha maendeleo yetu sisi wananchi wa Arusha. Mbona wanakuwa shortsighted kiasi hiki. CCM imeshika mpini ndio yenye serikali, wao wako 13 wa CHADEMA wako 2 ni nini wanachoogopa? Angalieni maana mnachopanda leo mtavuna baadaye! Tutawaadhibu 2015 kwa kutucheleweshea maendeleo. Sasa wekeni tofauti zenu kando mfanye kazi ama hamtuheshimu sisi wapiga kura?
   
 12. Wambugani

  Wambugani JF-Expert Member

  #12
  Dec 28, 2010
  Joined: Dec 8, 2007
  Messages: 1,755
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 145
  Hawa wanaCCM wa Elerai ni wapinga maendeleo na hawasomi alama za nyakati.
   
 13. n

  nguluvisonzo JF-Expert Member

  #13
  Dec 28, 2010
  Joined: Dec 27, 2010
  Messages: 511
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  kuna rafu huwa zinamanufaa lakini hii siyo.Bado elimu inatakiwa hata viongozi wetu.
   
 14. F

  Froida JF-Expert Member

  #14
  Dec 28, 2010
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,900
  Likes Received: 1,328
  Trophy Points: 280
  Mh Diwani aitishe mkutano wa wananchi katika kata yake awaeleze yaliyotokea
   
 15. BIN BOR

  BIN BOR JF-Expert Member

  #15
  Dec 29, 2010
  Joined: Nov 23, 2010
  Messages: 752
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  yaonekana kikao kilikuwa hakina posho, la sivyo wasingekimbia wehu wale.
   
 16. n

  ngwendu JF-Expert Member

  #16
  Dec 29, 2010
  Joined: Jun 7, 2010
  Messages: 1,967
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  kwenye red. Wadau hii imekaaje? mbona hamuijadili? au kwa sababu inagusa chadema na masilahi yake?
   
Loading...