exceptional lady
JF-Expert Member
- Oct 16, 2015
- 332
- 248
Habari zenu humu ndani,
Mimi mwenzenu ninatoka na mume wa mtu ndo mbaba wangu na ananiweka mjini mwaka sasa, kuna kipindi cha nyuma tulienda zetu huko sehemu ya mbali kidogo kubadilisha hali ya hewa.
Sasa akanitambulisha kwa rafiki zake ambao walikuwa wakifanya kazi pamoja, ila baadae wakatenganishwa. Kijana mmoja akaonyesha kama kanizimia mana alivyokuja akanisalimia akanishika mkono kama shemeji yake.
Sasa tukakutana ghafla siku nyingine tukapeana namba. Sasa kijana akanipenda tangu ile siku kiukweli nilipomuona pia nilijikuta navutiwa nae. Basi tumewasiliana na nampenda na tumepanga mikakati mingi na soon tunataka tukatambulishane ili mwakani Mungu akipenda tuoane.
MTIHANI UNAKUJA HAPA. Mchepuko ananipenda mpaka basi na hii ni kutokana tunaheshimiana na naiheshimu familia yake. Je naanzaje kumwambia huyu mtu? Na mi najua hatoweza kunioa kwa mara ya pili, na mi kijana tumeelewana vyema.
Ebu wenye upeo wanipe mawazo na ushauri jinsi ya kumwambia huyu baba pia nahitaji maneno ya busara maana asije akafa kwa presha.
Wale mliozoea kutukana sihitaji comments zenu za matusi, muwe wastaarabu kwani hakuna asiejua kwamba kuna kuchepuka au kutembea na mke au mume wa mtu huwezi kushauri pita tu kwa ustaarabu.
Karibuni kwa msaada