Rafiki wa Ex wangu ananitongoza

Mtunza siri zako

JF-Expert Member
Joined
Apr 11, 2025
Posts
586
Reaction score
975
Lamomy alisema niendelee kushea episodes za maisha yangu, basi leo kuna jambo limenitokea na hapa ndiyo pa kusemea.

Iko hivi, mnajua nimeachana na yule mwanaume bondia, sasa huyo Ex wangu alikua na rafiki yake wa karibu sana ambaye wamekua wote tokea wadogo, familia zao ni marafiki yani ni kama ndugu tu na tulikua tumezoeana sana ananiita shemejiakeee.

Huyo kaka alikua mchechi sana na alikuwa anakuja home kwa Ex wangu, wanaangalia mpira pamoja, wakati mwingine nawapikia na yeye ndo ambaye wakati mwingine nilikua namlalamikia matatizo ya rafiki yake.

Aliomba tukutane nimsimulie nini kimetokea mpaka uhusiano wangu umefikia mwisho. Leo mchana nimekutana naye nikamsimulia, amenisikiliza, akanipa pole halafu akaanza kunitongoza. Amesema amekuwa ananipenda wakati wote ambao niko na rafiki yake ila ni heshima tu ilimfanya ajizuie. Amesema yuko tayari kwa lolote na yeye yuko serious anataka kunioa.

Nimechoka maana nilifikiri wanaume hawatongozi wala kutaka kuoa maEx wa rafiki zao ambao ni sawa na ndugu.



Mimi simuamini na bado siko tayari kwa mahusiano ila kama ni wewe, ungefanyaje?
 
Usimpe huyo, nipe mimi ambaye sina uhusiano wowote na EX wako....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…