Rafiki kununa bila sababu

Rafiki kununa bila sababu

sasa bibie kama huyo kakununia, kwa nini usitengeneze urafiki na mimi?
 
Nilichojifunza ukiolewa ukamkuta mume ana rafiki yake ambae ameoa usijitie kimbelembele cha kuwa na urafiki na mke wa shemeji yake mara nyingi urafiki huo huwa hauwork out ni unafiki.
Nina case 3.
1.Recently kuna wadada wawili malkia wanguvu marafiki zangu waume zao marafiki basi huyu anapiga simu kwa wengine kumponda mwenzake na mwingine naye anahangaika kumponda mke wa shemeji yake.
Siku yao moja nitawaamulia nitawarekodi nitawafungulia group nitatuma voice notes zao wakisemana kisha naleft wapambane wajinga sana hao kuoneana wivu wa kijinga.

2.Case ya pili hubby alitakaga niwe na urafiki na mchepuko wa rafiki yake.
Yaani eti huyo rafiki yake ameoa mkewe yuko masomoni sasa ana kamchepuko kanajitegemea, wanaume walikuwa wana project yao tukajikuta na sie tunashiriki.
Mhhhh si unajua ile ego tena mke wa ndoa nitaundaje urafiki na mchepuko nikawa bandidu balaa kadada kanajidai kanajitahidi kujenga urafiki mimi nakaza uso.
Eti kuna siku tunaenda kula sikukuu ukweni hubby anapropose tuende nae. Nikamuambia wee vipi mke wa jamaa akirudi tena awe rafiki yangu? Nikalianzisha au hako kadada kamekutafutia mchepuko ndo maana unakapenda? Nililianzisha balaa.
Kuna siku wameenda kwenye mishe na le hubby mie nilikuwa naumwa hakyaMungu wamerudi nikawanunia na sikumtengea chakula hubby yule dada alipataga tabu na mimi sana. Kiufupi haikuwork out.

3.Mke wa rafiki wa mume wangu huyu wa ndoa kabisa nilimpenda balaa nikawa nikinunua kitu namnunulia malavidavi kama yote. Na yeye anashow love. Siku niliyosikia akiongea na simu kuwa najishaua na kujidai.
He he he he he nikachange na kila kitu kikaishia hapo kila mtu akala kona.

My dia wewe komaa na mume wako huyo ana sababu zake asikupasue kichwa.
Ukute mume wake anamchepuko huko basi anahisi labda mume wako anaujua au wewe unajua au kichaa cha ndoa kimempanda.

Hivi humu Jf kuna wake za watu!!nawaharumia sana wanaume waliovaa mabomu ya nyuklia


Sent using IPhone X
 
ipo hivi; nyie wadada mnapoombana ushauri hamnaga siri maybe kuna m2 ulizungumza nae habar zake nae kazisikia kitaa/mtu kampelekea sasa hapo atakua anakuona kama rafiki mnafik hebu jipeleleze kwanza.
 
Wadau natumai mu wazima.

Naombeni ushauri. Nimetokea kuwa na urafiki na.mke wa rafiki wa mume wangu kwa muda sasa. Tumekuwa tukiwasiliana tukionana tukitoka out. Bahati mbaya ana changamoto kwenye ndoa yake so muda mwingi natumia kumliwaza na kumshauri.
Cha kushangaza amekata mawasiliano tangu juzi alhamis alinitumia ujumbe kunialika kwa pasaka nikamjibu nitaconfirm na mr kisha nimerudia. Tangu hiyo siku hapokei simu zangu na wala hajibu ujumbe. Nimemuuliza kama nimemkwaza kitu napo hajibu. Je nimpotezee au nimtafute ili nijue tatizo ni nini?
Potezea huyo.
 
We nan alikwambia mapenz ya mtu yanashaurika? Haya Sasa wameshaelewana na mume wake tayar umeonekana mmbea

GunFire
 
ipo hivi; nyie wadada mnapoombana ushauri hamnaga siri maybe kuna m2 ulizungumza nae habar zake nae kazisikia kitaa/mtu kampelekea sasa hapo atakua anakuona kama rafiki mnafik hebu jipeleleze kwanza.
Mimi sina mashoga wa kupiga story zisizowahusu. Maisha yangu ni kazini nyumbani na shosti yangu ni hubby ila nae simuhadithii mambo ya huyu mdada.
 
  • Thanks
Reactions: amu
We nan alikwambia mapenz ya mtu yanashaurika? Haya Sasa wameshaelewana na mume wake tayar umeonekana mmbea

GunFire
Jambo usilolijua .....sijamshauri vibaya sanasana ni kumpa moyo tu .hamna umbea wowote na wewe umefeli
 
Pengine yuko karantini kuwa mvumilivi,akitoka atakujibu
 
Akii mi ningekausha kimya siku akijiskia kunambia atasema, mambo ya kubembelezana nop unless kuna kitu unajua umeharibu either umemuongelea Uongo labda. Ila kama sivyo subiri atakutafuta mwenyewe.
hvyo ndo inavyotakiwa kuna mmoja alinifanyia hvyo ila nilipojichunguza hamna baya nililomfanyia nilimpotezea na mimi kimya toka mwaka jana october sahv ndo anajifanya kunipigia simu ata sina habari nae
 
unaweza waza vibaya kumbe kapokonywa simu😥😥😥

think loudly.
 
hvyo ndo inavyotakiwa kuna mmoja alinifanyia hvyo ila nilipojichunguza hamna baya nililomfanyia nilimpotezea na mimi kimya toka mwaka jana october sahv ndo anajifanya kunipigia simu ata sina habari nae
Safi hadi amejishtukia mwenyewe, mimi pia siwezagi kubembeleza mtu afu ikiwa hujamkosea kitu aargh.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom