RadioOne/ITV na IPP yake hawamtaji Yusuph Manji kabisa

pilau

JF-Expert Member
Aug 16, 2012
1,594
447
Katika hali isiyokuwa ya kawaida vyombo vyombo vya habari havimtaji kabisa mwenyekiti wa Yanga Yusuph Manji, wamekuwa wakikwepa sana na kupepesa macho inapofika ulazima wa kumtaja Yusuph Manji katika taarifa mbalimbali zinazohusu Manji kama mwenyekiti wa klabu hiyo, wanapepesa macho badala yake wamekuwa wakiwatumia viongozi wengine wa yanga kama Makamu mwenyekiti Sanga na msemaji wao Sendeu, Je ugomvi huu ni ule wa Manji vs Mengi au Yanga vs IPP media?
 
Hapana kama sikosei kuna wakati Yusuph Manji aliomba mahakama iamrishe baadhi ya vyombo vya habari ambavyo ni vya IPP pamoja na gazeti la Mwananchi kutoandika habari zozote zinazomuhusu ziwe nzuri au mbaya. Bila shaka hiyo ndiyo sababu.
 
Ni bifu la kipindi kile wakati manji alienda mahakamani na kudai alipwe shilingi moja na mengi kwa kumdhalilisha. So msidhani kuna siku maji ataandikwa au kuonekana kwenye vyombo vya habari vya mengi labda wakijakupatanishwa na JK
 
Katika hali isiyokuwa ya kawaida vyombo vyombo vya habari havimtaji kabisa mwenyekiti wa Yanga Yusuph Manji, wamekuwa wakikwepa sana na kupepesa macho inapofika ulazima wa kumtaja Yusuph Manji katika taarifa mbalimbali zinazohusu Manji kama mwenyekiti wa klabu hiyo, wanapepesa macho badala yake wamekuwa wakiwatumia viongozi wengine wa yanga kama Makamu mwenyekiti Sanga na msemaji wao Sendeu, Je ugomvi huu ni ule wa Manji vs Mengi au Yanga vs IPP media?

Naona unahamu sana ya jona la manji kutajwa redioni? Kwani wewe huwa wanakutaja? Vipi viongozi wa vilabu vingine kama JKT Oljoro au Mgambo mbona hatujui majina yao? Kifupi kuna watanzania wengi tu hawatajwi kwa hiyo sio issue sana
 
Back
Top Bottom