Exclusive. Hatimaye Yusuph Manji amerejea rasmi Yanga na amemsajili Ibrahim Ajib

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
36,979
2,000
Huwezi amini ila ndiyo hivyo habari nilizozipata hivi punde kutoka katika chanzo changu cha kuaminika kabisa zinasema kwa yule Tajiri na Mwenyekiti wa Yanga Yusuph Mehboob Manji amerejea rasmi Klabu ya Yanga na kwamba urejeo wake muda wowote utawekwa wazi na Katibu Mkuu wa Yanga Boniface Mkwasa.

Katika kuonyesha kuwa Manji amerudi na hatanii hivi ninavyoandika huu uzi tayari 99% Mchezaji wa Simba SC Ibrahim Ajib amesaini Yanga na kwamba kati ya Kesho hadi Jumapili Nahodha wa Simba SC Jonas Gerald Mkude nae atasaini Yanga FC.

Inasemekana sababu kubwa iliyomuudhi na kumkasirisha Tajiri Manji ni Kitendo cha Simba SC kumalizana na Mchezaji mahiri na tegemo wa Yanga Mnyarwanda Haruna Fadhil Hakizimana Niyonzima kwa dau linalokaribia Tsh Milion 110 za Kitanzania na kumalizana pia na Mshambuliaji wa Yanga FC Donald Ndombo Ngoma.

Kazi imeanza na Shikamoo Yusuph Manji na Mohamed Dewji ' Mo '.

Nawasilisha.
 

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
36,979
2,000
Mpira wa bongo...unamsajiri mchezaji kwa m 110...!atairudishaje?mwisho wa siku mnanunua mechi za mbao
Inasemekana Manji kakasirishwa na Umafia ambao Simba SC imewafanyia Yanga FC hasa kwa Mchezaji ambaye pia ndiyo roho ya Yanga FC Niyonzima tena huku wakipewa msaada wa kufanikisha hili na Matajiri wawili kabisa wa Yanga FC ambao imegundulika kuwa wana Uadui mkubwa na Manji ( ambao kwa sasa sitoweza kuwataja Majina yao ila kama ukiwa Mtu wa Mpira najua utakuwa umeshawajua na bahati nzuri wote wawili Ofisi zao ziko jirani na Kampuni ya Superdoll na Benki ya Diamond Trust barabara Kuu ya Kariakoo / Msimbazi ) na wamefanya hivyo ili kuidhoofisha Yanga FC na kumtia aibu Manji ili Timu ifanye vibaya na Mhindi wa Watu aumbuke na apate aibu kwa Wanachama.

Kumekucha Simba na Yanga. Sasa Fedha za Manji na Dewji zinaongea Kudadadeki!
 

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
36,979
2,000
GENTAMYCINE... ulituletea exclusive hapa ya Simba washapewa points 3 zao za rufaa kwa FIFA.. Mpaka leo hiyo ndoto haijatokea... Nina mashaka sana na habari zako mkuu
Kwani Wachungaji na Maparoko walivyotuletea Exclusive ya Ujio rasmi wa Yesu Kristo wa Nazareth aliye hai ilitimia au Kristo sasa tunatiririka na kuserereka nae live / mubashara kama walivyotuaminisha?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom