Nondoh
JF-Expert Member
- Aug 26, 2016
- 298
- 478
Kama tunavyojua klabu ya soka ya Yanga ina vina saba vya CCM na imekuwa ikijulikana kama timu ya chama na serikali. Unapo iongelea Yanga unaiongelea CCM na unapo iongelea Yanga unaiongelea Serikali.
Kwa miaka zaidi ya 10 (sina uhakika) sasa imekuwa ikifadhiliwa na mfanyabiashara maarufu, kada wa CCM na pia ni diwani huko Mbagala Bw. Yusuf Manji.
Yusuf Manji amekuwa mstari wa mbele katika kuipigania Yanga, Serikali na CCM yake kwa hali na mali. Ameweza kuondoa mgogoro ndani ya Klabu ya Yanga ambao miaka ya nyuma kila kukicha yalikuwa yanazaliwa makundi mbalimbali kama Yanga Kandambili, Yanga Ukuta, Yanga Asili, Yanga Kampuni, Yanga...
Chini ya uongozi wa Yusuf Manji sijasikia migogoro klabuni kama nilivyokuwa nikisikia huko nyuma.
Kiujumla Yusuf Manji kwa muda alio ongoza Yanga kama tunavyosikia kwenye vyombo vya habari na matokeo ya uwanjani Yanga imefanya vizuri sana. Pia ameweza kuwalipia ada za uanachama wapenzi/wanachama wa Yanga na kuwaingiza bure washabiki wa soka kwa baadhi ya mechi za Yanga.
Tarehe 25/2/2017 imekaribia kama tunavyojua kuna ule mpambano wa watani wa jadi Simba na Yanga. Tofauti na miaka ya nyuma mpambano huu utatawaliwa na sakata la madawa ya kulevya. Washabiki wa Simba watawashambulia sana Yanga juu ya hii issue na washabiki wa Yanga nina uhakika kuna watakao onyesha support kwa Manji maybe na wengine kubeba mabango na kuna ambao hawata msupport Manji hawa wanaweza ongozwa na Mzee Akilimali.
Je wewe kama mshabiki wa Yanga upo upande gani? Upo upande wa Manji (team Manji) au upande wa CCM (team Makonda)? Na ukumbuke kuwa upande wa CCM ni kusaport maamuzi ya Serikali na ilani ya chama hivyo unamsaliti Manji aliyejitolea kwa klabu yako na chama, pia kuwa upande wa Manji ni kuisaliti CCM na serikali yake pamoja na jitihada za rais JPM za kupambana na madawa ya kulevya.
Nini maoni yako?

Kama mtanzania wa kawaida nimeshangazwa na huu ukimya wa viongozi wa Yanga na hata matawi ya mashabiki wa Yanga kuhusu suala la mwenyekiti Yusuph Manji, yaani hakuna hata asije kizungu mzima wala kugusia watu wanaendelea na maisha yao kama kawaida pale jangwani kama kwamba huyo mtu anayeteswa huko mahabusu ni panya tu.
Yanga mkumbuke mnaishi na kwenda chooni kwaajili ya Manji.Mmeenda kuifahamu Uturuki huko kwaajili yake na raha zote mnazokula.
Hata hao viongozi makocha watatu wanaotimuliana ushuzi hapo jangwani wote anawalipa Manji lakini na ona hakuna fadhila au hata utu mlioufanya juu ya hili suala lake.
Kumbukeni mahakama ndio inayohukumu kwamba fulani ndo anakosa na sio polisi, hapo alipo Manji ni mtuhumiwa kwahiyo nilitegemea hata pole zenu hata kumtembelea au kukaripia pale sheria zimapokiikwa juu yake.
Alipotajwa Mbowe chadema walicharuka, alipotajwa Gwajima waumini wake pia walicharuka lakini kwa upande wa Manji imekuwa tofauti , yaani ameachwa kama mtoto yatima wote mmempuuza huku mwataka hela zake.
Nakumbuka miezi ya hapo nyuma Manji alitishia kujitoa Yanga , mkamwomba sana na mkamtuhumu Mengi anahusika na hata kuchoma magazeti yake na matusi juu. Lakini Makonda kumdhalilisha Manji mmetulia tuliiiii , hapa mnanifanya niamini mnabifu lenu lililo ndani ya uccm kwa Mengi.
Yaani mnaona mkimkea Makonda ntakuwa mmeidhalilisha ccm ,kwahiyo ni bora Manji ateswe ila ccm mnayoipenda isisemwe.
Yanga onyesheni kwa vitendo mnamsapoti mwenyekiti wenu na muache uoga maana hao mnaowaogopa hawalipi hata mshahara mmoja wa mchezaji wenu.
Ni hayo tu