Radio Mpya Zinapataje Nyimbo Za Zamani TZ

JAYJAY

JF-Expert Member
Oct 31, 2008
7,519
7,559
Habarini wadau wa JF! Hapa nasikiliza kipindi cha nyimbo za zamani kwenye kituo kipya cha radio hapa DSM. Nyimbo wanazopiga ni za zamani sana za TZ na hata Kenya.

Sasa najiuliza huwa wanazipata wapi maana maktaba yao imesheheni na ninavyoelewa nyimbo hizi sio rahisi kupatikana kama za nje yaani Ulaya na Marekani na kwa ubora unaokubalika kwa kucheza redioni. Anayefahamu tafadhali!
 
hata TBC huwa zinapatikana hasa nenda kipindi hiki cha maonyesho ya 7"7 hata mm mwaka jana nilizipata nika change kuweka ktk flash, zilipendwa kama za NUTA,DDC MLIMANI PARK,JUWATA
 
hata TBC huwa zinapatikana hasa nenda kipindi hiki cha maonyesho ya 7"7 hata mm mwaka jana nilizipata nika change kuweka ktk flash, zilipendwa kama za NUTA,DDC MLIMANI PARK,JUWATA, nyimbo nyingi tu kama vile: Edita,Clara,Umenionyesha njia ya kwetu,Kasimu part 1&2,Hiba,Mv mapenzi,Sauda,Kupenda sio ndoto,Maselina NA nyingine nyiiingi na za OSS kama vile :Shida nilikupenda na Kaka Kinyogoli
 
Habarini wadau wa JF! Hapa nasikiliza kipindi cha nyimbo za zamani kwenye kituo kipya cha radio hapa DSM. Nyimbo wanazopiga ni za zamani sana za TZ na hata Kenya.

Sasa najiuliza huwa wanazipata wapi maana maktaba yao imesheheni na ninavyoelewa nyimbo hizi sio rahisi kupatikana kama za nje yaani Ulaya na Marekani na kwa ubora unaokubalika kwa kucheza redioni. Anayefahamu tafadhali!
TBC wana duka, oldies zote unazipata kwenye tape, lp au reel to reel (pia naskia library yao yote walidigitize, hivyo ukiongea vizuri unaweza kupata digital copies-japo mimi napendelea sana analogue over digital, LP ndiyo mpango mzima )
 
Ziko mtaani nyingi sana tena zenye ubora wa hali ya juu. Kama ni mfuatiliaji qa mziki hautatumia nguvu kuzipata. Binafsi nina collection ya nyimbo hizo zaidi ya mia5.
 
Back
Top Bottom