kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 13,423
- 13,935
Wananchi walioko karibu na minara ya simu, wanaotumia simu na walioko kwenye vyumba, majengo na vyombo vya usafiri vyenye wireless internet wameshikwa na taharuki baada ya kusikikia kutoka kwa Dr. Kweka kupitia kipindi cha morning magic kuwa mawimbi na mionzi kutoka minara ya simu, wife, na matumizi ya simu inasababisha madhara makubwa sana kwenye mfumo wao wa uzazi, ubongo, moyo, damu na kinga zao za mwili.
Watu wameonyesha dalili za kuanza kuchukua tahadhari dhidi ya minara ya simu iliyoko kwenye makazi yao pamoja na matumizi ya simu.
Nadhani serikali ina sababu ya kuliweka sawa jambo hili kwa kutoa elimu sahihi kuhusu matumizi ya simu, minara ya simu, vifaa vya wireless internet ndani ya vyumba, majengo na vyombo vya usafiri kwa usalama wa wananchi. Na ikwezekana watoe amri ya kuondoshwa minara hivyo kwenye maeneo ya watu.