Radio Free Africa mpo serious kweli??

Baba Heri

JF-Expert Member
Jul 23, 2013
1,503
2,222
Sijui mna mkataba gani na shirika la Deutsche Welle kurusha matangazo yao ya mchana ila mnachefua sana pale kila siku inapotimia saa saba dk 15 mchana wakati uchambuzi wa habari umenoga automatically nyinyi mnakatisha ghafla na kucheza tangazo lenye sauti kubwa ya kushtusha linalohusu shule fulani.

Tumieni common sense, ni bora msubiri wakati wa kusoma salam ndo mcheze hilo tangazo maana kama hamjajua mtapelekea hiyo shule kuchukiwa kwa staili mnayoshtusha watu na kuwakatishia mtiririko wa habari.

Unasaini mkataba na mteja mwenye shule kuwa tutacheza tangazo lako saa saba dk 15 wakati huku mmeshasaini mkataba mwingine na Deutsche Welle, tabia hiyo ina jina lisilofaa kuliandika hapa!
 
Kumbe na ww limekukera yan RFA sku hiz inapoteza mvuto kabisa kwanza watangazaji sio wabunifu kabisa kwenye vipind vyao.
Atleast mm cku hiz namkubali sana yule jamaa wa mambomambo yeye anjiita Mr C
 
Na wambura mtani vipi humkubali?
Namkubal kwenye kipindi anacho kimaster sema shida ya RFA ni moja ya kila presenter anaweza pangiwa kipindi chochote kias ambacho ladha ya kipind hupotea yan matangazaji huyohuyo anasoma taarifa ya habar, michezo, matukio, nk yan nishida tu
 
Labda ana shortage ya human resource
 
Back
Top Bottom