Radi yajeruhi Wanafunzi 14 Wilayani Muleba

Radi yajeruhi Wanafunzi 14 Wilayani Muleba

Kurzweil

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2011
Posts
6,622
Reaction score
8,427

radi 1.jpg
Wanafunzi 14 wa shule ya sekondari Rulongo wilayani Muleba Mkoa wa Kagera wamelazwa katika hospitali ya Lubya wilayani humo baada ya kujeruhiwa na radi.

Akizungumza jana Jumatano Januari 16, 2019 mganga mkuu wa hospitali hiyo, George Kasibante amesema tukio hilo limetokea leo na kwamba kati ya wanafunzi hao, watatu wana hali mbaya baada ya kuungua sehemu kubwa mwilini.

Amesema mwanafunzi mmoja amepoteza fahamu na madaktari wanajitahidi kuhakikisha anarejea katika hali yake ya kawaida, kwamba wengine walipata zaidi mshtuko.

Amesema radi hiyo ilipiga vyumba vya madarasa ya kidato cha pili na tatu, kwamba shule hiyo ipo mlimani eneo ambalo radi hupiga zaidi na kuwashauri wanafunzi kutojikinga na mvua katika maeneo yenye miti mirefu.
 
Ingekung'uta ferry karibu na soko la samaki.
 
Pole sana kwa majeruhi..
Heh sasa radi imepiga madarasa halafu anasema wasikae kwenye miti?
 
Back
Top Bottom