Rada uwanja wa ndege Dar yaanza kazi tena | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Rada uwanja wa ndege Dar yaanza kazi tena

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by thatha, Aug 24, 2012.

 1. t

  thatha JF-Expert Member

  #1
  Aug 24, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  Taarifa ya kurejea kwa huduma ya rada katika uwanja wa JNIA, Dar es Salaam

  23/08/2012

  0 Comments

  TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

  Dar es Salaam 23 Agosti, 2012

  KUREJEA KWA HUDUMA YA RADA KATIKA UWANJA WA KIMATAIFA WA JULIUS NYERERE (JNIA)

  Huduma ya mtambo wa Rada katika Uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) zimerejea baada ya kipuri kinachoingiza umeme katika mtambo huo, Power Supply Unit, kilichokuwa na hitilafu kufanyiwa matengenezo Afrika Kusini.

  Huduma hizo zilirejea, Agosti 23, 2012 majira ya saa 2:45 usiku baada ya kipuri hicho kurejeshwa nchini majira ya saa moja usiku ambapo wahandisi wa Mamlaka walianza kazi ya kukifunga kipuri hicho mara moja.

  Mamlaka ya Usafiri wa Anga-TCAA ililazimika kukipeleka kipuri hicho nchini Afrika Kusini kwa ajili ya kukifanyia matengenezo wakati ikiendelea na mchakato wa kununua kipuri kipya kutoka Kampuni iliyouza rada hiyo ya British Aerospace Systems (BAE) ya Uingereza.

  Imetolwa na

  Fadhili J. Manongi
  Mkurugenzi Mkuu
   
 2. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #2
  Aug 24, 2012
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,333
  Likes Received: 1,795
  Trophy Points: 280
  Bora heshima imerudishwa
   
 3. peri

  peri JF-Expert Member

  #3
  Aug 24, 2012
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 2,588
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  bora wamefanikiwa, ila bado kazi wanayo.
   
 4. Watu8

  Watu8 JF-Expert Member

  #4
  Aug 24, 2012
  Joined: Feb 19, 2010
  Messages: 47,347
  Likes Received: 2,683
  Trophy Points: 280
  Kifaa kilichoharibika ni Power Supply Unit...sasa najiuliza hawa jamaa inakuwaje wanamiliki mtambo mkubwa kama Radar halafu hawana back up ya vifaa vya ziada ikiwemo PSU, huku wakijua kabisa nchi yetu ilivyo na matatizo ya umeme!
   
 5. Chamoto

  Chamoto JF-Expert Member

  #5
  Aug 24, 2012
  Joined: Dec 7, 2007
  Messages: 2,085
  Likes Received: 1,122
  Trophy Points: 280
  Yaani tunashindwa hata kusuka ka-transformer ka power supply, sasa tunasomea uhandisi wa nini?
   
 6. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #6
  Aug 24, 2012
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  wahandisi wenyewe akina stella manyanya....wanasuka transfomer za midomo.
   
 7. eucalyptos

  eucalyptos JF-Expert Member

  #7
  Aug 24, 2012
  Joined: Jan 23, 2010
  Messages: 381
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 35
  Tukisema hatuna "wahandisi waadilifu" tunaweza kusemwa tumewatukana na tukisema "hatuna wahandisi wenye ueledi" sijui tutaambiwaje!!!
   
 8. omujubi

  omujubi JF-Expert Member

  #8
  Aug 24, 2012
  Joined: Dec 6, 2011
  Messages: 4,144
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  ukweli hii ni habari njema japo historia yake inatia uchungu lakini mimi nimeiopenda zaidi hii sahihi (signature)!!!!
  Sijui kama kweli anaweza kuwa signatory hasa kama ni cheque ndio kabisa!
  rada.jpg
   
 9. vipik2

  vipik2 JF-Expert Member

  #9
  Aug 24, 2012
  Joined: Nov 24, 2011
  Messages: 1,175
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  Hii sahihi nafikiri inaendana na IQ yake au la basi ni mwoga sana kuibiwa
   
 10. F

  FJM JF-Expert Member

  #10
  Aug 24, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Ubongo wangu unaniambia niikatae hii taarifa ya bwana Manongi.
   
 11. K

  Kifulambute JF-Expert Member

  #11
  Aug 24, 2012
  Joined: May 8, 2011
  Messages: 2,512
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135

  Mwalimu wake hakumfundisha uandishi mzuri wa sahihi
   
Loading...