Rada imekufa - BAE ipo wapi??

Interested Observer

JF-Expert Member
Mar 27, 2006
2,665
3,047
Rada ilinunuliwa kwa pesa za marekani 40 million. Ms. Short alimwambia Mkapa kuwa ile rada ilikuwa gharama mno, na kuwa Tanzania ilikuwa haihitaji rada ambayo pamoja na mengine ina uwezo wa miltaly Defence systems. Short alisema Tanzania inahitaji Rada rahisi ambayo itafanya kazi ya kumonita ndege za ki-raia kwa kuwa haina jeshi ambalo linahitaji rada kama ile. Mkapa na wapambe wake walikataa na kutaka ile "sophisticated". Tunambiwa ile rada imeharibika, na uharibifu huu umetokea mara nyingi, inawezekana kuwa imekufa.

Maswali yanakuja, Rada bei ni 40 million Dollar; muuzaji kachukua hizo pesa lakini hawezi kukupa spea au huduma. Wewe mtumiaji huna mafundi, hata BAE unashindwa kuwatafuta, unatafuta fundi Kenya au South Africa. Kwa nini spea na mafundi wasitoke BAE?? Sababu iliyotolewa na wahusika ni kuwa BAE hawahusiki. We paid USD 40 million (USD 28 million net for BAE); but we can't get them service it?

Sasa hivi ndege zinaelekezwa kwa kutumia watu yaani "manual". Si hatari hii?

Kuna uwezekano mkubwa sana ile rada ambayo ipo Airport siyo ile ya BAE, au?? Ile ya BAE ipo wapi? It can be a very stupid question, but I doubt it is an espionage case!!.
 
Au tulinunua rada mtumba? Nusu ya bei ya rada hiyo waligawana mawaziri akiwemo Chenge na Mkapa mwenyewe.
 
Hii ilikuwa sababu tosha ya kumkamata Benjamin Mkapa na kuwamjibisha bila kujali kuwa alikuwa rais. Mbona Silvio Belusconi pale Utaliana amepigwa mvua bila kujali kuwa alikuwa kiongozi wa taifa hili? Hii rada na huu mdege wa rais vinajulikana ilivyokuwa dili ya kupata pesa ya uchaguzi kwa kuongezea kwenye EPA. Natamani huo mdege wao uanguke na kuwadungua walioununua wakijua haufai sawa na rada lao.
 
Kila siku ni kufuga ujinga tu, walau tungepata dictotor kwa miaka miwili afanye ile kazi alofanya Idd Amin pale

Uganda. Jamaa walisha kula aslimia kubwa ya kwanza kwenye manunuzi wakatuaminisha sophisticated Rada kumbe toy,

nasasa wanakula za kusingizia matengenezo na wataziiba sana kwa kisingizio cha spares and maintenance, hawa watu

walikuwa wakufunga maisha au kunyonga mpaka kufa maana wanakwiba mpaka sasa wanahamia kwenye NSSF zetu, hawana adabu wala aibu.
 
Kiongozi wa serikali ya Italia, Waziri Mkuu wa zamani Silvio Berlusconi (miaka 76) amehukumiwa kifungo cha miaka minne gerezani baada ya kukutwa na hatia ya kukwepa kulipa kodi.

Huyu babu alikuwa anatumia kila njia kukwepa mashtaka, lakini hatimaye amenaswa.

Mafisadi wa kibongo wasome maandishi ukutani, nao watanaswa tu...
 
Kwa maana hii, Air Defense system ya TZ iko 'extremely WEAK', sisi hakuna kitu ambacho tunaweza kufanya vizuri... Muda ndio kila kitu, muda ndio utatuonyesha u.puuzi wa serikali yetu... Sasa kwa maana hii, ndege yoyote ya kivita inaweza kuingia kwenye anga letu na kufanya watakavyo, tumebakia na siasa tu, kupiga domo kama makamba...
 
Back
Top Bottom