utukufu mwanjisi
JF-Expert Member
- Aug 19, 2017
- 2,846
- 2,511
Wengi tulipenda kukuita James bond, akili kubwa,master, Michael scofield,Mr fursa,jasiri mfungua njia,the don,boss ruge na mengine mengi.
Hayo majina yote hapo juu uliendana nayo kutokana na moyo uliokuwa nao namna ulivoweza kusaidia watu katika sekta mbalimbali kwa kuwainua wengi kiuchumi ambao mpaka leo wanaishi kwa busara zako wewe,ingawa juu ya sifa zote hizo wapo baadhi ambao walilalamika juu ya fitina zako juu yao kwa kuwarudisha nyuma kimaendeleo lakini wengi walikuombea mema mana ulisaidia wengi kuliko uliowaumiza.
Karibu mwezi mzima nimekaa nikitathimini yale ambayo uliyasimamia na yalienda vizuri katika kila sekta lakini leo yameanza kupotea na nadhani baada ya mwaka hamna litakalokuwepo kati ya haya;
1.Wasanii wakubwa uliowatengeneza wewe leo wamebaki hata hawaelewi wanaimba nini, wengine wanatoa nyimbo leo wiki hawaeleweki nyimbo zao zimeenda wapi mfano Tanzania one(Nasibu) kwenye muziki amebaki anaimba matusi sio yule ambae ulimtunza wewe akaimba nyimbo zinazoishi mpaka leo na mwenzie Tanzania two(Ally)toka ulipolala kitandani pale Kairuki ndo basi tena wanaishi kwa nguvu za mashabiki waliotengeneza kipindi wapo chini yako.
2.T.H.T kuna siku nilikaa nikamsikiliza Muki wa Makomando aliongelea nidhamu mbovu iliopo pale shuleni kwako baada ya kuondoka wewe na namna wanafunzi wako walivyokata tamaa,kwa hiyo wengi hawaendi tena kujifunza mziki bali wanashinda studio kwa ma producer kutafuta nafasi na kututolea nyimbo mbovu mwisho hawapati hata shoo na kuishia kuwa vibaka tu mtaani sababu ya stress.
3.Ofisi(Clouds) siku hizi limekuwa sio jengo la kushtua tena kama zamani tulivokuwa tunapapalikia kisa kutafuta nafasi ya kuonana na wewe ili utupe njia jasiri wetu,sasa hivi mjengoni tunapaona kama ofisi ya Ebony fm Iringa maana tunajua nafasi za kuingia pale ni nyepesi sio kama kipindi upo wewe kwanza lingine nikuambie huko uliko ofisi sasa hivi hata rangi haipakwi na kila mtu kawa papa kisa hawamuogopi tena Sheba na Tirarira kama kipindi ulivokuwepo wewe.
4.Upcoming artists ambao uliweza kuwatengeneza kila mwaka sasa hivi hawapo tena toka umewatoa Benson na Jay melody ingawa nao washapotea maana nguvu yao ulikuwa wewe,hawajatokea tena zaidi hao upcoming sasa hivi wapo kwenye vigodoro huko wanakomaa na Boss wao Majizzo. Kwa hiyo ule muziki mzuri wa vijana uliowatengeneza hakuna tunasikia tu mitusi kwenye nyimbo za vijana wako WCB.
5.Siasa imebaki kwa rafiki yako kipenzi January tu,hao wengine uliosaidiana nao wamebaki kama waimba taarabu tu mpaka unajiuliza Ruge aliwezaje kukaa na marafiki viazi namna hii au aliwavumilia vipi basi unabaki na jibu kuwa sasa alikuwa mtu wa watu.
6.Fiesta huu mwezi wa saba tena kipindi cha jua mikoa yote lakini naona hata uhamasishaji hamna sijajua kuwa wanauogopa upande wa pili maana kuna monsters uliowatengeneza wewe bila kujua wangekuja kukugeuka na leo ndo wanaisambaratisha tamasha ulilojivunia wewe na uliowaacha hawana nguvu tena ya kushindana na wale uliowapa njia zote.
5.Mwisho wale wanamziki ambao kuimba ilikuwa zero sema uliwabeba hivyo hivyo kutokana na nguvu uliokuwa nayo kwenye industry sasa hivi wanasikiliza miziki yao vyumbani maana hata hatuwaelewi wanaimba nini na wengine sasa hivi wanajishughulisha na shughul zingine kama kuuza vyakula maana wanajua kimziki hawawezi au walikuwa hawajui ila wewe ndo uliwabeba.
NINAYO MENGI YA KUKUONGELEA LAKINI ACHA NIISHIE HAPA. MSALIMIE SANA DR.MENGI