Mahakama zipi?Kwenda mitandaoni sio tatizo, tatizo ni kwenda mitandaoni pasipo kwenda na mahakamini.
Mwanasiasa anachokifanya ni lazima aujulishe umma maana umma ndio mwajiri wake hivyo wako sahihi kabisa.
Mahakama zipi?Kwenda mitandaoni sio tatizo, tatizo ni kwenda mitandaoni pasipo kwenda na mahakamini.
Mwanasiasa anachokifanya ni lazima aujulishe umma maana umma ndio mwajiri wake hivyo wako sahihi kabisa.
"Of course, you have to nock the door"
hili wengi tulishaliongelea mara kadhaa humu jamvini lakini walengwa masikio na macho yao ni kama yameingiwa nta na ukungu!Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 Kama zilivo katiba za nchi nyingi duniani hasa zile zinazoendeshwa katika misingi ya kidemokrasia inatanabaisha wazi uwepo wa mihimili mitatu katika nchi, yaani Serikali, Bunge na mahakama, kati ya hiyo Mahakama ukiwa ndo muhimili uliopewa majukumu ya kutafasri sheria(ikiwemo katiba yenyewe maana nayo ni sheria).
Katika kutafasiri sheria mahakama imekuwa ikifanya mambo kadhaa wa kadhaa Kama vile kuzitamka baadhi ya sheria kuwa zipo kinyume na katiba au vipengele kadhaa vya katiba vinakiuka haki za binadamu na mikataba kadhaa wa kadhaa ya kimataifa N.K. na moja yaya mashuj katika harakati hizi za kupambana na sheria na vipengele vya katiba vilivyoonekana kuwa kandamizi basi ni the late Rev. Mtikila (R.I.P) kwa wale waliosoma sheria basi huyu ni moja ya watu lazima utakutana naye hasa kwenye somo la Katiba(Constitutional Law), hapo alipoenda Kambole mzee Mtikila yeye alishafika kitambo akipinga kipengele kinachozuia mgombea binafsi. Narudia tena R.I.P Reverend.
Naam, Reverend Mtikila!! Kwanini nimemkumbuka huyu jamaa? ni baada ya ya Leo kukutana na thread ikionesha kuwa my learned brother Jebra Kambole amefungua kesi kwenye Mahakama ya Haki za Binadamu ya Africa( African Court of Human Right) kupinga kipengele Cha katiba kinachokataza kupinga matokeo ya urais yakishakutangazwa. Mimi sitaki kuingia kwenye logic ya kwanini kipengele hicho kiwepo au kisiwepo kwenye katiba kwani hii ni more jurispudential au philosophical aspect hivyo kila mtu anaweza kuwa na mtazamo wake.
Kilichonisukuma kuja hapa jamvini ni namna ambavyo Leo tunawaharakati lukuki ambao kila siku Instagram, Twitter na Facebook account zao zimejaa malalamiko juu ya sheria wanazodai ni kandamizi zilizotungwa na Bunge au hata watu waliokamatwa kwa kwakuwa wamekiuka the so said tyranical laws na wengi wa Hawa ni wasomi wazuri na wengine ni wanasheria kabisa ambao wanajua haya mambo kuliko hata the late mzee Mtikila.
Ninachotaka kusema mzee Mtikila alitambua kuwa mahakama ndo chombo pekee kwa mujibu wa katiba chenye mamlaka ya kutafasiri sheria na alikitimia ipasavyo kuzichallenge sheria na vipengele vya katiba alivyoamini kuwa vilikuwa kandamizi na kwa kiasi kikubwa alifanikiwa.
Kinachonishangaza wanaharakati wa Leo wamegeuza Instagram, Twitter na Facebook kuwa ndo mahakama zao, Zitto, Nape, Bashe, Maria Sarungi Julius Mtatiro na wengine wengi wanalamika huko, kibaya zaidi hata Rais wa Chama Cha Wanasheria(TLS) mwanamama Fatuma kalume naye analalamika huko. Hawa ni watu wanaofahamu wazi kuwa njia ya kisasa na ya busara ya kupambana na sheria za bunge zinazoonekana kandamizi ni kutumia Mahakama and nothing more, na hii ndo maana halisi ya ya mihimili ya dola ambayo inakamilisha kile kinachoitwa Check and Balance. ushahidi upo wa kutosha kuwa Jambo hili linawezekana, Reveland aliweza, Hawa kina Fatuma karume, Zitto, Maria Sarungi na wengine wanashindwa Nini hadi wanaishia kulia lia kwenye mitandao? Yes mtandaoni maana huko wanajijengea umaarufu na kwao umaarufu ni kitu Cha mhimu kuliko kile alichokifanya Mtikila ambacho mwisho wa siku kinawanufaisha watu wote.Badala ya kupambana na hizo sheria wanazoziona kandamizi watu wanapambana na matokeo, wanasubiri Abdul Nondo akamatwe wajaze mandishi kwenye account zao za mitandao, wanasubiri Mtatiro akamatwe wajaze mandishi kwenye account zao na sio kwenda kuomba mahakama kuzi declare sheria hizo kuwa kandamizi, yes! Mtandaoni! Hko wanajipatia umaarufu na kujijenga kisiasa.
Ndio maana nasema alichokifanya Jebra ni kutukumbusha namna pekee Bora ya kupambana na hicho tunachokiita unjust laws, na ujumbe huo uwafikie wote wanaoshinda mitandaoni kulalamika na kwa upana wake zimfikie mama/Bibi Fatuma Karume maaana amebeba dhamana kubwa katika hili badala ya kushinda mitandaoni akitoa mipasho atumie mda mwingine kuratibu mambo Kama haya anayoyafanya Jebla Kambole.
"The Court is there for some one who nocks the door" njia pekee ya kupinga sheria tunazodhami kuwa ni kandamizi ni kwa kwenda mahakamani na si mitandaoni!!
Asante Rev, asante brother Jebra kwa kutukumbusha.
No, you don't have to nock the door, you have to knock it!"Of course, you have to nock the door"
Nakupongeza sana mkuu kwa hoja yako hii. Siku zote uwa ninawaeleza watu kuwa hapa nchini hatuna cha wanaharakati wala wapinzani. Katika nchi nyingi zenye kufuata utawala wa kisheria, mahakama uwa ndicho chombo pekee kinachotengua na kutoa tafsiri ya vifungu vya sheria ambavyo vina mkanganyiko katika matumizi yake. Bunge lenyewe linatunga hizo sheria na baadaye serikali inazisimamia na sisi wananchi tunazifuata. Sasa, hawa wanaojiita wanaharakati machachari wanashindwa nini kwenda kupinga mahakamani? Facebook, haiwezi kutengua sheria! Siku zote uwa mimi ninampongeza Mchungaji Christopher Mtikila maana aliweza kupigana vita isiyohitaji kuandamana wala kutoa jasho, hakika aliweza kutumia hakili yake na utawala wa sheria vizuri."The court is not your mother..."
Ni kweli huyu mzee alipambana sasa, Hawa wa sikuu hizi wanajitafutia tu umaarufu mitandaoni na kulazimisha wakamatwe ili kuendelea kusikika badala ya kufanya vitu ambavyo matokeo yake ni ya mda mrefu na Yana manufaa kwa jamii nzima!Hata mimi nimemkumbuka sana huyu mzee alikua anaonesha ukomavu wake kwenye Sheria haogopi mtu wala Serikali sipati picha angekuwepo kipindi hiki na kukutana na wanasheria wengine kina Lissu, Kibatala nk
Tuna Mwanasheria wapenda kiki tena kiki UCHWARA. Haiingii akilini jambo la kisheria na ambalo ufafanuzi wake hupatikana mahakamani ukaitisha press au kukimbilia tweeter na kupiga makelele.Wanachokifanya ni kujingea umaarufu UCHWARA ambao mwisho wa siku hautatui ttz lolote lile na shida kubwa ni ujinga wetu wenyewe wafuasi wao,tungekua na AKILI hata huko fb au tweeter tungekuwa tunawahoji kwanini wasiende mahakamani?Zaidi na sisi tunabak tunawashangilia mwisho ndo ishatoka.Nakupongeza sana mkuu kwa hoja yako hii. Siku zote uwa ninawaeleza watu kuwa hapa nchini hatuna cha wanaharakati wala wapinzani. Katika nchi nyingi zenye kufuata utawala wa kisheria, mahakama uwa ndicho chombo pekee kinachotengua na kutoa tafsiri ya vifungu vya sheria ambavyo vina mkanganyiko katika matumizi yake. Bunge lenyewe linatunga hizo sheria na baadaye serikali inazisimamia na sisi wananchi tunazifuata. Sasa, hawa wanaojiita wanaharakati machachari wanashindwa nini kwenda kupinga mahakamani? Facebook, haiwezi kutengua sheria! Siku zote uwa mimi ninampongeza Mchungaji Christopher Mtikila maana aliweza kupigana vita isiyohitaji kuandamana wala kutoa jasho, hakika aliweza kutumia hakili yake na utawala wa sheria vizuri.
Kabisa mkuu, na huko kwenye mitandao wakiona unawachallenge basi kuwachallenge basi wanakublock fasta.Tuna Mwanasheria wapenda kiki tena kiki UCHWARA. Haiingii akilini jambo la kisheria na ambalo ufafanuzi wake hupatikana mahakamani ukaitisha press au kukimbilia tweeter na kupiga makelele.Wanachokifanya ni kujingea umaarufu UCHWARA ambao mwisho wa siku hautatui ttz lolote lile na shida kubwa ni ujinga wetu wenyewe wafuasi wao,tungekua na AKILI hata huko fb au tweeter tungekuwa tunawahoji kwanini wasiende mahakamani?Zaidi na sisi tunabak tunawashangilia mwisho ndo ishatoka.
Ni kweli kabisa. Kesho kutwa kuna uchaguzi mdogo wa jimbo la Buyungu, nimewasikia akina ACT na wengine wakijinadi kuwa wataibuka na ushindi wa kishindo kwenye jimbo hilo na kata kadhaa. Hawahawa juzi ndiyo walikuwa wanalalamika kuwa tume ya uchaguzi haiko huru na kwamba sheria ya uchaguzi ni kandamizi baada ya kumaliza chaguzi ndogo za Siha, Kinondoni na kwingineko. Pale Bungeni alipoulizwa Waziri mkuu kuhusu hizi kasoro za tume ya uchaguzi, alijibu kuwa kama kuna watu ambao wanaona kuwa haki yao imeminywa kwenye chaguzi hizo, basi waende kwenye vyombo vya sheria kutafuta haki yao. Lakini hakuna yeyote ambaye amedhubutu kwenda huko na hajabu leo hii wanaenda kwenye uchaguzi wa kiwa na uhakika wa kushinda kwa kishindo na wakishindwa, wanarudi kulalamika na kuwataka wananchi waandamane. Angekuwa marehemu MTIKILA, siku nyingi sana alishaonana uso kwa uso na Mheshimiwa JAJI ili kupata ufafanuzi wa kifungu chochote ambacho yeye angekuwa anakiona kuwa kinamkwaza ili asifikie malengo yake. Hawa wenzetu sijui wana malengo gani, labda hawana wanasheria wa kuwashauri juu ya mambo ya kisheria! Hata TUNDU LISSU naye hajawahi kwenda mahakamani kulalamikia sheria yoyote anayodai kuwa ni kandamizi, zaidi ya yeye kushitakiwa tu huko mahakamani.Tuna Mwanasheria wapenda kiki tena kiki UCHWARA. Haiingii akilini jambo la kisheria na ambalo ufafanuzi wake hupatikana mahakamani ukaitisha press au kukimbilia tweeter na kupiga makelele.Wanachokifanya ni kujingea umaarufu UCHWARA ambao mwisho wa siku hautatui ttz lolote lile na shida kubwa ni ujinga wetu wenyewe wafuasi wao,tungekua na AKILI hata huko fb au tweeter tungekuwa tunawahoji kwanini wasiende mahakamani?Zaidi na sisi tunabak tunawashangilia mwisho ndo ishatoka.
Kabisa mkuu, na huko kwenye mitandao wakiona unawachallenge basi kuwachallenge basi wanakublock fasta.Tuna Mwanasheria wapenda kiki tena kiki UCHWARA. Haiingii akilini jambo la kisheria na ambalo ufafanuzi wake hupatikana mahakamani ukaitisha press au kukimbilia tweeter na kupiga makelele.Wanachokifanya ni kujingea umaarufu UCHWARA ambao mwisho wa siku hautatui ttz lolote lile na shida kubwa ni ujinga wetu wenyewe wafuasi wao,tungekua na AKILI hata huko fb au tweeter tungekuwa tunawahoji kwanini wasiende mahakamani?Zaidi na sisi tunabak tunawashangilia mwisho ndo ishatoka.
Mkuu yaani hili Jambo linafikirisha Sana, wenzetu tu Kenya hapo wanajitahidi Sana kwenye hilo Hawa wa kwetu cjui wanafikiria nini.Ni kweli kabisa. Kesho kutwa kuna uchaguzi mdogo wa jimbo la Buyungu, nimewasikia akina ACT na wengine wakijinadi kuwa wataibuka na ushindi wa kishindo kwenye jimbo hilo na kata kadhaa. Hawahawa juzi ndiyo walikuwa wanalalamika kuwa tume ya uchaguzi haiko huru na kwamba sheria ya uchaguzi ni kandamizi baada ya kumaliza chaguzi ndogo za Siha, Kinondoni na kwingineko. Pale Bungeni alipoulizwa Waziri mkuu kuhusu hizi kasoro za tume ya uchaguzi, alijibu kuwa kama kuna watu ambao wanaona kuwa haki yao imeminywa kwenye chaguzi hizo, basi waende kwenye vyombo vya sheria kutafuta haki yao. Lakini hakuna yeyote ambaye amedhubutu kwenda huko na hajabu leo hii wanaenda kwenye uchaguzi wa kiwa na uhakika wa kushinda kwa kishindo na wakishindwa, wanarudi kulalamika na kuwataka wananchi waandamane. Angekuwa marehemu MTIKILA, siku nyingi sana alishaonana uso kwa uso na Mheshimiwa JAJI ili kupata ufafanuzi wa kifungu chochote ambacho yeye angekuwa anakiona kuwa kinamkwaza ili asifikie malengo yake. Hawa wenzetu sijui wana malengo gani, labda hawana wanasheria wa kuwashauri juu ya mambo ya kisheria! Hata TUNDU LISSU naye hajawahi kwenda mahakamani kulalamikia sheria yoyote anayodai kuwa ni kandamizi, zaidi ya yeye kushitakiwa tu huko mahakamani.