R.I.P Omar Omar

R.I.P Omar Omar

Ino

Member
Joined
Dec 20, 2012
Posts
25
Reaction score
7
Sote tulikupenda ila Mungu kakupenda zaidi, tunakuombea nasi tupo nyuma yako.
 
Mi nitakukumbuka kwa kile kibao cha mbuzi kapewa ndevu, ng'ombe kanyimwa
 
Halafu hizi habari zimekaa juu juu tu, hebu mwenye habari iliyokamilika aanike hapa.
Nini sababu ya kifo chake?
Na pia kama kuna historia yake kwa ufupi iwekwe hapa ili wasiomjua wapate kumfahamu vizuri.
 
kweli kabisa Mr Able, hata mimi sielewi elewi

MSANII nyota wa miondoko ya Mnanda 'Mchiriku', Omar Omar, amefariki dunia usiku wa kuamkia leo baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Habari zilizotufikia ni kwamba, Omar Omar aliyetamba na nyimbo mbalimbali ukiwemo ule maarufu wa 'Kupata ni Majaliwa' alifariki nyumbani kwao Temeke, saa chache baada ya kurejeshwa kutoka Hospitali ya Temeke alipokuwa amelazwa kwa siku kadhaa.


Taarifa hizo zinasema kuwa mara baada ya kurejea nyumbani, msanii huyo alizidiwa na hatimaye kufariki na msiba wake upo nyumbani kwao Temeke Mikoroshini.


Akielezea kifo cha msanii huyo Mkubwa Fella ambaye ni jirani yake amesema marehemu Omari Omari alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa kifua
.

Mwenyezi Mungu Ailaze Roho ya Marehemu Mahali Pema Peponi. Amen!
 
dah..nakumbuka 90's songi lake"eti anaitaka saa yangu"
topaz wamepotea kabisa!!!
r.i.p sela
 
Kama sijaelewa kitu hapa,alikuwa amelazwa then akazidiwa muda mfupi baada ya kurudi nyumbani sasa ilikuwaje akaruhusiwa?
Na alikuwa anaumwa tu kifua?mmh
RIP Omar
 
Rest in Peace kaka may God forgivu u all your sins.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom